Mabomu ya machozi Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabomu ya machozi Arusha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Arushaone, Sep 20, 2012.

 1. Arushaone

  Arushaone JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 14,351
  Likes Received: 613
  Trophy Points: 280
  Ni maeneo ya Kwangulelo baada ya jamaa mmoja mwenye gari alipomuua dereva wa pikipiki baada ya kupita gari lake ghafla. (pikipiki ilichomekea gari)
  Mwendesha bodaboda alisimama pembeni ya barabara na kupiga magoti kuomba msamaha kuwa alikuwa anajiokoa kugongwa na gari ligine ila jamaa mwenye gari alichomoa bastola na kumuua hapohapa. Hayo yalijiri juzi
  saa 3 usiku na leo ndio mazishi. Cha ajabu yule dereva pamoja na kuwekwa kituo cha polisi, aliachiwa as if aliua kuku tu. Leo wakati wanajiandaa kwa mazishi yule aliyeua kaonekana akiendesha gari lake na ndipo wananchi na madereva wa bodaboda wakaenda nyumbani kwa yule muuaji na kuchoma nyumba yake na kuharibu kila kitu. Baada ya hayo kujiri wakawa wanaelekea nyumbani kwa wafiwa na kumbe taarifa zimeshafika polisi ndipo wakaja kujaribu kutawanya watu... Wananchi wamekataa wanahoji kisa cha mtu kuua na kuachiwa usiku huohuo. Wakafunga barabara kuu ya Moshi-Arusha. Polisi walipoanza kupiga mabomu ya machozi ndipo wananchi wakabeba mawe na kuiweka gari ya polisi kati kabla hawajaanza kupambana na polisi magari mengine ya FFU yaliyokuwa mahakamani kwenye kesi ya Lema yakaenda kutoa sapoti na ndio kisa cha MABOMU. Magari sasa yanatumia barabara ya Kwangulelo-Kijenge.
   
 2. Ralphryder

  Ralphryder JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 4,588
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Chadema hao!
   
 3. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  waambie waandishi wakae mbali
   
 4. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Nimeshtushwa na jamaa kumuua mwenzake.....!!!
  Yaani anathamini gari kuliko utu...?
  Mtu mpaka kaomba msamaha bado unamshuti dah!!!
   
 5. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Duh! Ama kweli serikali tawala sasa ni dhahiri kabisa inaendeshwa ndivyo sivyo!

  Mtu kaua tena aliyeuawa alikukimbilia na kukuomba msamaha halafu bado ukamtoa duniani tu! Na baada ya hilo bado uko huru baada ya masaa kadha ya tukio! Hakika huyu jamaa aliyesababisha hili hata naye kifo kinamstahili.
  Hili alilotenda halikubaliki kamwe ktk jamii ya Watanzania!

  Ngoja tupate na maoni ya memberz!
   
 6. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #6
  Sep 20, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Huyo aliyeua muangalieni vizuri anaweza kuwa Ighondu, haiwezekani aue halafu awe nje wakati lulu anasota keko kwa kanumba kutishia kujiangusha na akaangukia uchogo wala hajapigwa na "kitu chenye ncha kali"
   
 7. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #7
  Sep 20, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160

  Jinga mtu huyo linapita! Huyo huyo huyo!!
   
 8. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #8
  Sep 20, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Mkuu hali ilikuwa mbaya kama tuko somalia hivi...Moshi wa mabomu ulikuwa umetanda angani...
   
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  Sep 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Wewe ulikuwepo yote yakijiri au umehadithiwa tu, maana hiki kisa chako kimekaa kipaukwa pakawa, kimepambwa kumfanya mwendesha gari ni Shetani mmoja mbaya sana.

  Visa namna hivi huwa siviamni mpaka niipate picha kamili, hii yako siiamini mpaka sasa, sijui baadae.
   
 10. kupe

  kupe JF-Expert Member

  #10
  Sep 20, 2012
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 1,025
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Ndio maisha ya arusha hayo ambako 99% ni chadema.
   
 11. Pendael laizer

  Pendael laizer JF-Expert Member

  #11
  Sep 20, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 961
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ni hata mimi nipo eneo la tukio. Pesa ipo juu ya sheria kwa serikali ya ccm.
   
 12. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #12
  Sep 20, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nchi hii sasa kweli tumefika pabaya. yaani mtu anamtwanga risasi mwenzake ambaye amepiga magoti kuomba msamaha hadharani! Ni vigumu kuamini kwua haya yanatokea Tanzania
   
 13. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #13
  Sep 20, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Huyo aliyeua mwenzake na kuachiwa na polisi ni nani?
   
 14. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #14
  Sep 20, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Hauamini nini sasa?????
  Kama wewe unakatabia ya kurushaga kitu hambacho haujadhibitisha hakika ujue ni wewe tu ndio mjinga!

  Humu jamvini member wako makini zaidi ya ujuavyo (uvikirivyo) na labda ni wewe na lile genge lako ndio mnashindwa kuamini yajirio hapa jamvini!

  Pole kwa kukosa uaminifu!

   
 15. Arushaone

  Arushaone JF-Expert Member

  #15
  Sep 20, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 14,351
  Likes Received: 613
  Trophy Points: 280
  zomba nakushauri kuendelea kusoma hii thread utakuta watu wengine watakaokanusha au kuikubali taarifa hii. Hata kama sio hapa jaribu kusikiliza radio au hata magazeti. Ahsante
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #16
  Sep 20, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  yaani nyan'gau huyu anaona gari lake bora kuliko uhai wa mtu, he he he he he yaani ningempata huyu namfunga makamba halafu namkata kiungo kimoja baada ya kingine halafu nambandika kwenye sufuria halafu naenda kutupia simba au kunguru shenzi kabisa pumbavu. Namlaani kwa maneno yote magumu huku dunia, kila balaa na mkosi vimuandame, kha mtu unakosa utu namna hii hata hao polisi waliomtoa na wenyewe walaaniwe tena kama wamepokea kitu kidogo adhabu yao iwe sawa na ya muuaji
   
 17. F

  FJM JF-Expert Member

  #17
  Sep 20, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kuna uzi mwingine una taarifa ya watu waliopelekwa mahakamani kwa madai ya kumtapeli mke wa Chagonja. Na inasemekana watuhumiwa hapo wapo rumande. Sasa inakuwaje mtuhumiwa wa utapeli anakuwa rumande lakini muuaji anaachiwa huru? Raia wako salama?

  Pili, huyo muuaji anamiliki silaha kihalali? Na aliomba kwa sababu zipi?
   
 18. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #18
  Sep 20, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Nampa hongera sana mleta mada maana amejaribu kuunganisha tukio la juzi na la leo ili kumpa msomaji picha kamili...huu ndio uandishi uliotukuka!
  Bahati mbaya niko kwenye simu ningekuongezea Reputation mkuu wangu.
  Achana na zomba ambaye hata akiona picha anauliza..."imepigwa na nani?"
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #19
  Sep 20, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo unatakaje????

  Acha kutumika kihivyo wewe kijana!
  Iko siku utanyimwa haki yako na utajashangaa na roho yako bila ya majibu!

  Tumia kichwa kufikiri na siyo masaburi yako!
   
 20. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #20
  Sep 20, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  Arusha ilikuwepo, ipo na itaendelea kuwepo
   
Loading...