Kwenye hili Manyerere nakusihi rudi darasani, hili halihitaji akili kubwa kulijua, mtoto ameisha shuhudia hivi, polisi ndio waliompiga risasi, matamshi ya akina Mwigulu na Mwampamba yote yanaonesha hawa jamaa walikua wamejipanga, kama unaunganisha issues za humu, unga na ile iliotoka jana humu, kua magamba hawataki kiti cha meya wa jiji la Arusha kwenda upinzani, so hata hiyo tarehe iliotangazwa, uchaguzi hautafanyika. Kwenye hili ccm na serikali hawawezi kukwepa lawama, lakini mwisho njaomba niseme hivi, kwa umri wako kaka na uzoefu wako wa kua mwanahabari wa muda mrefu, je kuna uhalifu wowote uliowahi kufanyika hapa nchi usiohusisha serikali na wahalifu hao wasikamatwe? Ngoja nikukumbushe kidogo, wizi wa pesa za iliokua Beural De change ya NBC ya zama hizo, Sarah Simbaulanga mwaka 1987, siku 3 tu baadae alikamatwa London Uingereza (Technology ya wakati huo ilikua chini sana na still walimkamata) linganisha na issue ya EPA with this technology we have, nenda tukio la kuauwa kwa RPC wa MWanza juzi, ndani ya siku 18 tayari wote waliohusika walikamatwa, linganisha na issue ya kuuawa kwa pot wako David Mwangosi na sarakasi za polisi (Assume kusingekua na picha za mnato na video) Nenda na tukio la Mwakyembe "sumu" yake and lingenisha na walichokisema akina DCI Manumba?
Naomba ku-conglude hivi, kama polisi hawahusiki, kukamata wahusika ni kazi ya wiki 1 tu, ukiona danadana, weka akili kichwani, kaka, hivi macho na ujasiri wa Nape jana na alichokua akikiongea, mbona saikolojia ilimwonesha kabisa kwamba anacho kiongea sicho anachokiamini? hata hili mzee wangu hukuona!?