Mabomu Arusha: Mtazamo wangu


M

Manyerere Jackton

Verified Member
Joined
Dec 11, 2012
Messages
2,402
Likes
808
Points
280
M

Manyerere Jackton

Verified Member
Joined Dec 11, 2012
2,402 808 280
Ndugu zangu, matukio ya vurugu na mauaji katika Taifa letu sasa yamefikia hatua mbaya. Tararibu, tumeiona amani ya Tanzania ikizikwa kwa nguvu.


Kumekuwapo kurushiana maneno makali tangu kuanza mtiririko wa mabomu katika Jiji la Arusha. Kwenye tukio la Kanisani kukawapo maneno kwamba huenda ni Waislamu, lakini hoja hiyo ikapungua nguvu kutokana na taarifa kwamba kijana mwendesha bodaboda aliyempakia mlipuaji, ni Mkristo. Hapo kidogo mambo yakanywea.


Sasa limekuja hili la mkutanoni. Chadema na CCM sasa wanakaribia kutoana macho. Kila upande unadai upande ule ndiyo uliohusika. Polisi nao wameingizwa kwenye kadhia hii wakidaiwa kwamba walirusha mabomu na risasi za moto. Kuna ushuhuda wa hayo. Mwenyekiti Mbowe, naye hakwenda mbali na nadharia hiyo.


Ndugu zangu, tangu bomu lile la Kanisani, na sasa hili la kwenye mkutano wa hadhara wa Chadema, naanza kuungana na mtoa mada mmoja hapa JF aliyesema inawezekana "mhusika yuko pembeni anachekelea".


Kauli ya mtoa mada huyo ni ya msingi sana.Mimi najiuliza, kwanini mabomu yawe Arusha?


Nashawishika kwenda mbali kidogo na mtazamo wa wengi. Mimi nadiriki kuwatilia shaka ndugu zetu Wakenya kwamba isije ikawa hii ni vita ya kiuchumi.


Mtakumbuka kwamba Kenya wamekuwa mbele sana kuhakikisha Tanzania hatufanikiwi. Ujenzi wa barabara ya Mto wa Mbu-Musoma ni Wakenya waliokuwa wa kwanza kusimama kidete duniani kote kuendesha kampeni ya kuipinga. Wamefanikiwa.


Mtakumbuka suala la uuzaji mano ya tembo. Kenya walihakikisha wanatumia rasilimali zao zote kukwamisha mpango huo. Wakafanikiwa.


Ni Kenya hawa hawa ambao wamepinga ujenzi wa kiwanda cha magadi huku kwetu kwa kigezo kwamba kitaathiri mazingira ya hilo ziwa tulilogawana nao.


Kana kwamba haitoshi, Kenya wamehakikisha muda wote Loliondo haitulii. Wamediriki kuwaleta CNN, Al Jazeera na mashirika makubwa ya habari ndani ya loliondo kuandika kile wanachodai kwamba ni kuhamishwa kwa ndugu zetu Wamasai. Ikumbukwe kuwa kutokuwapo kwa amani Loliondo kunawasaidia kuendelea kunufaika kiuchumi kwa kuingiza mifugo yao na kuendesha mambo wanayoyataka.


Kenya wana hasira wakitaka mpaka wetu wa Ngologonja uliofungwa tangu enzi za Mwalimu, ufunguliwe. Serikali yetu, walau kwenye hili imekuwa imara. Imegoma.


Ndugu zangu, Kenya kwa sasa utalii wao umeathirika sana. Mabomu ya magaidi wa Al Shabab yameharibu sana utalii wao. Wameona watalii wengi wanamiminika Tanzania. Isije ikawa kwamba wameamua kuharibu huku kwetu na wakati huo huo wakiendelea kuvutia watalii kwao.


Ikumbukwe hapa kwamba sasa vyombo vya habari vya Kenya havitoa umuhimu mkubwa kwa matukio ya ugaidi nchini humo licha ya ukweli kwamba kila siku kuna mabomu yanalipuliwa na magaidi.


Ombi langu kwa Watanzania, isije ikawa tunashikana uchawi hapa wenyewe kwa wenyewe, ilhali mchawi mwenyewe yuko pembeni anatucheka.


Nayasema haya kwa sababu uchunguzi wa awali wa tukio la bomu Kanisani, umebaini kuwa bomu na wahusika walitoka Kenya. Taarifa hizi zipo ndani ya vyombo vyetu vya ulinzi na usalama. Pengine hawataki kuziweka wazi kwa hofu ya kuvuruga ujirani wetu.


Bado akili ya kawaida hainitumi kuamini kwamba CCM wamekuwa wabaya kiasi cha kuamua kuwaua Chadema. Tena basi, sidhani kama kweli kuna mwana CCM anaweza kutoa amri kwa polisi kulipua bomu ndani ya mkutano kwa mazingira yake tuliyoyashuhudia.


Isitoshe, napata shaka kweli kuamini kuwa bomu limerushwa na Chadema kwa madai hafifu kwamba waliona wanashindwa kwenye uchaguzi wa udiwani, hivyo walitumia bomu kuahirisha uchaguzi kama njia ya kukwepa aibu ya kushindwa! Haya yote yananipa shida kuyaamini.


Tuwe watulivu na tutumie busara sana kwenye mambo haya. Ushiriki wa Wakenya kwenye sakata hili si jambo la kupuuzwa. Tena tukumbuke kuwa hata M23 ambao tunapambana nao sasa, wanaweza kuwa na mkono wao. Tukianza kulaumiana wenyewe kwa wenyewe tutakuwa tunampa kicheko adui yetu.


Huu ndiyo mtazamo wangu.


Nawasilisha.
 
mbinguni

mbinguni

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2013
Messages
1,988
Likes
236
Points
160
mbinguni

mbinguni

JF-Expert Member
Joined Jan 2, 2013
1,988 236 160
Iko siku tu wasioijua hawa magamba wataondoka na kuwekwa rumande.
 
M

multmandalin

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2012
Messages
1,947
Likes
32
Points
145
M

multmandalin

JF-Expert Member
Joined Sep 8, 2012
1,947 32 145
Huu ukisasa umezidi hata humu jamiini tutumie hadubini!
 
N

Nyumbu-

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Messages
978
Likes
126
Points
60
N

Nyumbu-

JF-Expert Member
Joined May 26, 2009
978 126 60
Manyerere Bana, Si ukae kimya kama huna cha kuandika? Wewe umepataje habari za upelelezi wa Mlipuko wa kanisani wakati ripoti yenyewe haijatoka? Una ushirika gani na hao wapelelezi? Naona umeanza kuhangaika kama ulivyohaingaikia habari za kutekwa na kuumizwa kwa Kibanda!
 
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2010
Messages
47,851
Likes
3,638
Points
280
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2010
47,851 3,638 280
Kuza kidogo maandishi...
 
M

Manyerere Jackton

Verified Member
Joined
Dec 11, 2012
Messages
2,402
Likes
808
Points
280
M

Manyerere Jackton

Verified Member
Joined Dec 11, 2012
2,402 808 280
Manyerere Bana, Si ukae kimya kama huna cha kuandika? Wewe umepataje habari za upelelezi wa Mlipuko wa kanisani wakati ripoti yenyewe haijatoka? Una ushirika gani na hao wapelelezi? Naona umeanza kuhangaika kama ulivyohaingaikia habari za kutekwa na kuumizwa kwa Kibanda!
Siwezi kukaa kimya kana kwamba mimi sina uchungu na hali ya mambo ilivyo sasa nchini mwetu. Kuwa na conclusion kwenye suala la aina hii ya Arusha, ni makosa makubwa. CCM na Chadema wanaporushiana lawama, siku ya mwisho ikawa kwamba kweli adui katoka nje, hii aibu tutaificha wapi? Muda huu si wa kurushiana maneno ya lawama, bali ni kufanya kila liwalo kushikamana na kumjua mbaya wetu ni nani.
 
C

Chikaka Sumuni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2013
Messages
1,339
Likes
5
Points
0
C

Chikaka Sumuni

JF-Expert Member
Joined May 16, 2013
1,339 5 0
Mura waito, hapo umeangukia pua, hayo unayoyasema hayana kichwa wala miguu. Tunachojua ni kwamba ukizoea madaraka sasa ghafla unaona anguko lako linasababishwa na mwingine lazima utajihami. Wewe Manyerere nilidhani wewe ni msomi, mtafiti na mwelewa sasa na wewe unatuletea uzi ambao ni biased bana achana na hii kabisa, hiyo ya Kanisani kwa nini hawaiweki hadharani, waogope kuharibu ujirani wakati watu wako wameuawa uliapa kulinda ujirani au ardhi yako, watu na mali zao?

Acha siasa bana
 
Technician

Technician

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2010
Messages
843
Likes
2
Points
0
Technician

Technician

JF-Expert Member
Joined Mar 30, 2010
843 2 0
Hivi yule mama aliyeshindana na mbunge Godbless Lema yuko wapi vile????????????????????
 
A

asakuta same

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2011
Messages
15,035
Likes
99
Points
0
A

asakuta same

JF-Expert Member
Joined Mar 1, 2011
15,035 99 0
ishauri ccm na mafisadi waache kuua raia wema . acha kuandika kama ulikuwepo eneo la tukio ,wewe utakuwa unafahamu zaidi ya majeruhi waliotoa ushuhuda?
 
A

asakuta same

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2011
Messages
15,035
Likes
99
Points
0
A

asakuta same

JF-Expert Member
Joined Mar 1, 2011
15,035 99 0
Siwezi kukaa kimya kana kwamba mimi sina uchungu na hali ya mambo ilivyo sasa nchini mwetu. Kuwa na conclusion kwenye suala la aina hii ya Arusha, ni makosa makubwa. CCM na Chadema wanaporushiana lawama, siku ya mwisho ikawa kwamba kweli adui katoka nje, hii aibu tutaificha wapi? Muda huu si wa kurushiana maneno ya lawama, bali ni kufanya kila liwalo kushikamana na kumjua mbaya wetu ni nani.
hiyo ni kazi ya vyombo vya usalama na siyo yako wewe au mimi muuza mitumba mkuu, na iweje adui aweze kutoka nje atumie teknolojia ndogo ya bomu la kurusha na mikono bila kukamatwa na hao polisi.? zaidi majeruhi wametoa ushuhuda wa aliyewapiga mabomu na risasi ,otherwise uniambie hao wakenya wanatumia jeshi letu la polisi kutuhujumu.
 
D

duchi

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2012
Messages
1,766
Likes
3
Points
0
D

duchi

JF-Expert Member
Joined Oct 22, 2012
1,766 3 0
Je ni kiongozi chama kipi alisema watahakikisha nchi haitatawalika? je ni kiongozi wa chama kipi alisema wanahakikisha arusha watashinda kwa gharama yoyote? hiyo ni "circumstantial evidence" kuwa mauaji yote ya arusha yanapangwa na chadema ili watu waichukie serikali yao. Kumbuka kesi ya kupanga njama za mauaji iko mahakamani.
 
M

Manyerere Jackton

Verified Member
Joined
Dec 11, 2012
Messages
2,402
Likes
808
Points
280
M

Manyerere Jackton

Verified Member
Joined Dec 11, 2012
2,402 808 280
Hapa siwatetei CCM wala Chadema. Siwahukumu CCM wala CHadema. Changamoto niliyowapa wana JF wote ni ya kujaribu kutumia vichwa zaidi kufikiri na kupata ukweli wa mambo badala ya kukimbilia kuhukumiana. Bado nasema, inawezekana adui yetu huko aliko anajipongeza na kutucheka, maana tumeamua kushikana uchawi wenyewe!
 
Rutunga M

Rutunga M

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2009
Messages
1,646
Likes
348
Points
180
Rutunga M

Rutunga M

JF-Expert Member
Joined Mar 16, 2009
1,646 348 180
Hivi wewe si ni mhariri wa gazeti la Jamhuri? na siku ya kutoka ni Leo? Je kwa nini hukuandika haya kwenye gazeti lako?
 
mdeki

mdeki

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2011
Messages
3,304
Likes
48
Points
145
mdeki

mdeki

JF-Expert Member
Joined Mar 28, 2011
3,304 48 145
Jamani msimshambulie manyerere hayo ni mawazo yake kinachotakiwa ni kumjibu kwa hoja, mi bado natafakari aliyoandika ntarudi
 
M

Mazindu Msambule

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Messages
5,568
Likes
2,905
Points
280
M

Mazindu Msambule

JF-Expert Member
Joined Feb 22, 2012
5,568 2,905 280
Siwezi kukaa kimya kana kwamba mimi sina uchungu na hali ya mambo ilivyo sasa nchini mwetu. Kuwa na conclusion kwenye suala la aina hii ya Arusha, ni makosa makubwa. CCM na Chadema wanaporushiana lawama, siku ya mwisho ikawa kwamba kweli adui katoka nje, hii aibu tutaificha wapi? Muda huu si wa kurushiana maneno ya lawama, bali ni kufanya kila liwalo kushikamana na kumjua mbaya wetu ni nani.
Kwenye hili Manyerere nakusihi rudi darasani, hili halihitaji akili kubwa kulijua, mtoto ameisha shuhudia hivi, polisi ndio waliompiga risasi, matamshi ya akina Mwigulu na Mwampamba yote yanaonesha hawa jamaa walikua wamejipanga, kama unaunganisha issues za humu, unga na ile iliotoka jana humu, kua magamba hawataki kiti cha meya wa jiji la Arusha kwenda upinzani, so hata hiyo tarehe iliotangazwa, uchaguzi hautafanyika. Kwenye hili ccm na serikali hawawezi kukwepa lawama, lakini mwisho njaomba niseme hivi, kwa umri wako kaka na uzoefu wako wa kua mwanahabari wa muda mrefu, je kuna uhalifu wowote uliowahi kufanyika hapa nchi usiohusisha serikali na wahalifu hao wasikamatwe? Ngoja nikukumbushe kidogo, wizi wa pesa za iliokua Beural De change ya NBC ya zama hizo, Sarah Simbaulanga mwaka 1987, siku 3 tu baadae alikamatwa London Uingereza (Technology ya wakati huo ilikua chini sana na still walimkamata) linganisha na issue ya EPA with this technology we have, nenda tukio la kuauwa kwa RPC wa MWanza juzi, ndani ya siku 18 tayari wote waliohusika walikamatwa, linganisha na issue ya kuuawa kwa pot wako David Mwangosi na sarakasi za polisi (Assume kusingekua na picha za mnato na video) Nenda na tukio la Mwakyembe "sumu" yake and lingenisha na walichokisema akina DCI Manumba?

Naomba ku-conglude hivi, kama polisi hawahusiki, kukamata wahusika ni kazi ya wiki 1 tu, ukiona danadana, weka akili kichwani, kaka, hivi macho na ujasiri wa Nape jana na alichokua akikiongea, mbona saikolojia ilimwonesha kabisa kwamba anacho kiongea sicho anachokiamini? hata hili mzee wangu hukuona!?
 
G

Getstart

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Messages
6,257
Likes
781
Points
280
G

Getstart

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2012
6,257 781 280
Jackton

Ukweli ni kuwa siyo CCM au CHADEMA, lakini yaweza kuwa vikundi katika vyama hivi au hata mtu wa nje ya vyama vya siasa kwa manufaa yake anayoyajua. Lakini kinachokera na kutia shaka ya sisi wengine ni jinsi vyama hivi vinavyotoa tuhuma ambazo baadhi yetu tunaona za kitoto. Pia inatia shaka jinsi Serkali inavyoshughulikia kadhia hizi kwa kufikiria kuwa wakitoa matamko yanayoelekea kisiasa wanajenga. Zaidi ni jinsi Polisi au vyombo vyetu vya usalama kwa ujumla wanvyoshindwa katika kila tukio. Hapana wanatupelekea kubaya. Tamko la jana Bungeni lilikuwa la bahati mbaya sana kwani lilichochea chuki zaidi za wananchi kwa Polisi!

Busara ilitakiwa kutumika na Serkali na pia Chama Tawala (ambacho nilifikiri kimejaa watu wa hekima na uzoefu) ili kuwaunganisha Watanzania katika masuala kama haya. Nilitarajia kuwa bahada ya Mwenyekiti wa Chama kuanza kwa kuwapa pole wenzao hawa wengine wangetafuta muda wakakaa pamoja ili kuwatia nguvu wananchi kuwa kitu kimoja katika kukataa matendo haya. Lakini wao wameyatengenezea mazingira ya kisiasa. Bahati mbaya sana kwao wananchi wanafahamu.

hata hivyo si busara kuanza kuwasingizia Wakenya. Tuna matatizo yetu ambayo nafikiri yanatokana na kutokukubali kikamilifu mfumo wa ushindani kwa watu wachache tulionao. Wito wangu ni kuwa ni muda mwafaka vyombo vyetu vya usalama vizinduke vikatae kutumika. Viwe nje ya makundi ya kisiasa na vitende haki; watu watavipa support.
 
bullet

bullet

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2009
Messages
1,003
Likes
129
Points
160
bullet

bullet

JF-Expert Member
Joined Oct 31, 2009
1,003 129 160
"Ndugu zangu, tangu bomu lile la Kanisani, na sasa hili la kwenye mkutano wa hadhara wa Chadema, naanza kuungana na mtoa mada mmoja hapa JF aliyesema inawezekana "mhusika yuko pembeni anachekelea".

Ndugu Manyerere kama hivyo ndivyo, je tusimuamini majeruhi wa bomu aliyesema aliyelipua bomu alipanda gari la polisi? Na je mtoto wa aliyesema alipigwa risasi na polisi? Je polisi yetu inapata order kutoka Kenya?
 
K

kibelaa

Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
95
Likes
3
Points
0
K

kibelaa

Member
Joined Apr 2, 2012
95 3 0
Wahusika na wa hapa hapa nchini,kwani Mwigulu na Nape ni Wakenya?
 
M

Manyerere Jackton

Verified Member
Joined
Dec 11, 2012
Messages
2,402
Likes
808
Points
280
M

Manyerere Jackton

Verified Member
Joined Dec 11, 2012
2,402 808 280
basi, kama kweli hili suala limefanywa na polisi wetu wa tanzania, kuna sababu zote wananchi kuingia mitaani kwa amani kushinikiza livunjwe! kauli za wengi lazima zitakuwa na mashiko! kwa sababu hiyo, nami naanza kufuatilia mtiririko huu wa polisi kurusha risasi na bomu. mungu ainusru tanzania.
Wahusika na wa hapa hapa nchini,kwani Mwigulu na Nape ni Wakenya?
 
D

Deo

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2008
Messages
1,216
Likes
120
Points
160
D

Deo

JF-Expert Member
Joined Nov 10, 2008
1,216 120 160
Mchanganuo hafifu na umekuwa biased (si semi haiwezekani bali unamapungufu sana). Focus uchumi na Kenya peke yake. Explore more on all other facets even within economic, there are other stake holders with their own interests.

Hata hivyo ni wazo linalowezekana, ni muhimukuifanyia utafiti wa kina. Ni sawa na kumwita jirani yako mchawi wakati mtoto wako anautapia mlo kwa uzembe wako

 

Forum statistics

Threads 1,274,226
Members 490,637
Posts 30,505,424