Mabomu Arusha: Mtazamo wangu

Mabomu Arusha: Mtazamo wangu

Manyerere Jackton sifahamu hasa kiwango chako cha elimu lakini sehemu kubwa unadhalilisha hata wenyeji wa Musoma na hasa Butiama.Kweli kwa akili yako unawaza akili ukiwa umekufa au umelala?.Kenya kwa hatua za maendeleo wanatuzidi sana na hawana haja ya kuona wivu kwetu.Taarifa tu ya leo Kenya wanajenga njia za Reli 26 ndani ya Nairobi hadi JKIA kurahisisha miundo mbinu kwa KSH10 BILION.Je Tanzania ina nini cha Kujivunia?, kama siyo uvivu wa kufikiri kama wewe na ufisadi?.Ndugu Yangu MAnyerere ndio maana mie nilikwisha kataa kusoma gazeti lenu la Jamhuri maana mpo shallow minded,myotic na zero mind.Hebu unapopata nafasi ya kutoka ndani ya Tanzania jaribu kuwa inquisitive kuona nchi zingine zimepigaje hatu.Au pengine ndiyo njia ya kutaka kumpamba LOWASA na kashfa ya kuamuru molani kumshambulia Nassari.Kwa hatua zote hizo kwa jambo ili LOWASA amejipaka tope tena katika uso wa wastaarabu na kuzidi kuwa mbali na kikome cha urais 2015.Rudi darsani Manyerere Jackton upate angalau weledi wa kuchambua mambo.
 
Jackton kwa hiyo Kenya walituma polisi wetu kuua raia wao??!! kumbuka kama huamini video zilizopo
basi amini maneno ya mtoto mdogo aliyelazwa hospitali kuwa aliyempiga risasi alivaa nguo za kipolisi'
unataka kusema mtoto anajua sare za polisi wa Kenya!!? shughulisha ubongo tusitafute mchawi wakati
wanga wako ndani ya nchi yetu.
 
kutambua elimu ya mtu ni rahisi tu. moja ya mbinu ni pale mtu anapoamua kumshambulia mwingine bila kujielekeza kwenye hoja. jamhuri linasomwa na watu makini wanaohangaisha vichwa ktk kufikiri. halina wasomaji wa mihemko na jazba. wenye akili wote kwenye matukio ya arusha lazima wake na 5W's + 1H katika kupata nani mhusika. kunishambulia kwa mtazamo wangu ni kuonyesha jazba na majibu ya mkato. jadili hoja, basi.
Manyerere
Jackton
sifahamu hasa kiwango chako cha elimu lakini sehemu
kubwa unadhalilisha hata wenyeji wa Musoma na hasa Butiama.Kweli kwa
akili yako unawaza akili ukiwa umekufa au umelala?.Kenya kwa hatua za
maendeleo wanatuzidi sana na hawana haja ya kuona wivu
kwetu.Taarifa tu ya leo Kenya wanajenga njia za Reli 26 ndani ya
Nairobi hadi JKIA kurahisisha miundo mbinu kwa KSH10 BILION
.Je
Tanzania ina nini cha Kujivunia?, kama siyo uvivu wa kufikiri kama wewe
na ufisadi?.Ndugu Yangu MAnyerere ndio maana mie nilikwisha kataa kusoma
gazeti lenu la Jamhuri maana mpo shallow minded,myotic na zero
mind.Hebu unapopata nafasi ya kutoka ndani ya Tanzania jaribu kuwa
inquisitive kuona nchi zingine zimepigaje hatu.Au pengine ndiyo njia ya
kutaka kumpamba LOWASA na kashfa ya kuamuru molani kumshambulia
Nassari.Kwa hatua zote hizo kwa jambo ili LOWASA amejipaka tope tena
katika uso wa wastaarabu na kuzidi kuwa mbali na kikome cha urais
2015.Rudi darsani Manyerere Jackton upate
angalau weledi wa kuchambua mambo.
 
Last edited by a moderator:
The buck stops with Tanzania Intelligence and Security Service (TISS) and Police.

Hivi vyombo vya ulinzi vimeshindwa kutekeleza wajibu wake wa msingi kabisa kwa raia ambao kodi zao zinatumika kuwaajiri.

Kushindwa kutimiza wajibu wao kunafanya mpaka jamii inaanza kunyosheana vidole kwa mambo ambao vingeupata ukweli.

Ombwe la usalama linawafanya Wananchi kutafuta kafara mpaka inafikia kutazamana wao kwa wao na kuanza kulaumiana.

Kuna uwezekano mkubwa watu wabaya (maghaidi) wa ndani au nje ya nchi walifika kwenye mkutano wa CHADEMA kwa sababu na madhumuni wanayoyajua wao wakiwa wamevaa mavazi ya polisi na siraha mikononi wakati siyo polisi kama inavyotokea mara nyingi Tanzania katika mapoli au bara bara pale majambazi yanapotumia sare za polisi au jeshi kutenda maovu. Hata kupiga risasi ilifanyika kwa makusudi kuwachanganya watu ili waweze kufanikiwa kumtorosha yule aliyerusha bomu.

Matukio mengi ya kighaidi mashariki ya mbali kwa sasa yanafanyika kwa njia hii ya kutumia sare za ulinzi na kufanya mauwaji.

Kama kungekuwa na utendaji makini wa vyombo vya dola na ulinzi wa nchi haya yote yasingetokea lakini kwa sasa tunaachwa kuanza kulaumiana sisi kwa sisi wakati kuna uwezekano aliyetenda yuko pembeni.

Watanzania tunatakiwa tuupe ubongo wetu nafasi ya kufikiri kwa mapana badala ya kupata majibu mepesi mepesi.

Hata wanasiasa wetu kwa sasa hawatutendei haki katika maneno yao. Wengi wao emotions zimewatangulia mbele badala ya fikra mbadala za kiutu uzima kama viongozi.

Vyombo vya usalama wa nchi vinaonekana kushindwa kukabiliana na changamoto za karne ya 21.

Vyombo vya ulinzi vinatembea wakati dunia kwa sasa inakimbia.

TISS and Police has failed Tanzanian.
 
Mkuu Manyerere nashukuru sana kwa uchambuzi wa hayo matukio kama ulivyoainisha katika hii mada.
Sasa swali la msingi inamaana nchi yetu decision makers wake wanatokea Kenya?
Nini kazi ya usalama wa Taifa,je katika usalama wa taifa hakuna kitengo cha Economic Intelligence Unit ?
Kama ipo kazi yake ni nini mpaka ishindwe kukabiliana na hizo propaganda na matukio kama ulivyoainisha?
 
Ng'wamapalala; itoshe tu kusema una akili sana. hii ndo hoja yangu. bahati mbaya kuna watu wanajifanya wasomi wanaoshindwa kutambua hiki ulichokisema. matokeo yake magaidi yapo kando yanatucheka na kutuona tu wajinga. asante sana ng'wamapalala.
 
Hizi ni jitihada zao tu mwishowe watasema Tanzania haina tofauti na sisi ona na wao wanauana.

Tafakari mtanzania mwenzangu.
 
Itoshe tu kusema kuwa 'negative forces' ndani ya nyumba ina nguvu kuliko positive ones...! Itoshe sasa tumtoe 'tembo chumbani'.....!
 
Mimi binafsi nakubali kuwa kweli inawezekana polisi wameshindwa, na hii ni kutokana na recruitment style yao...! Wengi ni wale waliotumia vyeti vya ndugu zao n.k. Lakini vyombo vingine vya ulinzi na usalama uwezo vinao............na vinajua nini kinaendelea.....! Tumepeleka majeshi Congo ili ku-deal na 'negative forces' kule, ni wakati wetu pia kuondokana na hiki kigenge cha wahuni kilichoamua kutumia njia hii ya mauaji na vitisho ili kunyamazisha na kuogopesha watanzania...!
 
Manyerere Jackton,

..mbona mambo mengi uliyosema Kenya wanayapinga ni kwa manufaa yetu sisi wa-Tanzania?

..mimi ni Mtanzania na ninapinga ujenzi wa barabara ya Arusha--Musoma itakayokatiza ndani ya mbuga ya Serengeti. badala yake naunga mkono an alternative southern route of Arusha--Musoma road inayopita nje ya mbuga ya Serengeti. suala hili limejadiliwa kwa kina hapa JF na ilibainika bila shaka yoyote kwamba serikali ya Tanzania walikuwa hawana hoja.


..zaidi, nchi wafadhili, particularly Ujerumani, wameonyesha nia ya dhati kutusaidia kujenga barabara ya Arusha--Musoma itayapita upande wa kusini, nje ya mbuga ya Serengeti. Ahadi hiyo inahusisha pia ujenzi na ukarabati wa mtandao wa barabara za vijijini baina ya Arusha na Musoma.

..Loliondo haitulii kwasababu ya mpango haramu wa kugawa eneo hilo kwa kampuni ya nje, wakati wananchi wenyeji wa Loliondo wanakabiliwa na uhaba wa ardhi ya malisho ya mifugo yao. Kuwalaumu Wakenya kwa makosa ya serikali yetu tuliyoichagua ni kukimbia wajibu wetu. Kwanini serikali isiwapeleke hao wageni maeneo ya Selous, au Katavi, ambako wanaweza kuwinda bila kugombania ardhi na wananchi?? Je, Wakenya ndiyo wanaouzuia serikali isifanye hivyo??

..Umezungumzia Wakenya kupinga mradi wa kuchimba magadi katika ziwa Natron wakijenga hoja za kuhifadhi mazingira. Kwa mtizamo wangu wenzetu wanalinda mazingira yao kutuzidi sisi. Hebu tafuta za mkuu wa mkoa wa Tanga alipotembelea misitu iliyoko Handeni na Kilindi ambayo ipo mpakani na Kenya. Iliripotiwa kwamba wakati wenzetu Kenya wanalinda misitu yao, wa-Tanzania tuko ktk harakati kubwa kabisa za kukata miti kuuza mkaa kwa majirani zetu wa Kenya.

..Wakenya hawana haja ya kutuhujumu, kazi ya kuihujumu Tanzania inafanywa kwa umahiri mkubwa kabisa na utawala wa CCM tuliouchagua sisi wenyewe. Kama huamini, tafuta makala ya Johson Mbwambo " Tumekuwa taifa 'gonjwa Afrika' Mashariki."

cc: Jasusi, Maundumula, Njowepo,
 
Last edited by a moderator:
Jackton kwa hiyo Kenya walituma polisi wetu kuua raia wao??!! kumbuka kama huamini video zilizshughulisha ubongo tusitafute mchawi wakati
wanga wako ndani ya nchi yetu.
Wakati mwingine nasikitika tunaposhindwa kutumia akili zeru vizuri.... Hivi polisi wetu hawa ambao hawajawahi kusikia bomu mitaani wakiwa na silaha huwezi kufikiria akili ya kwanza kabisa kwao ni kwamba wao ndio walikuwa target na kwamba kwa kuwa walikuwa na silaha watakuwa wa Kwanza wao kurusha risasi kama kujilinda? Tumieni akili please acheni kuwa waganga wa Kienyeji!

Kwa sasa hakuna mTanzania wa chama chochote anaweza kufanya yaliyofanyika.
 
Adui yuko ndani ya chama cha sisimu na serikali yao waliyounda na pia inamjua muhusika wa haya mauaji ya kisiasa ndio maana hawataki tume ya kimahakama iundwe kuchunguza. Ukiona penye usiri ujue kuna jambo limefichwa na kwasababu hali halisi yaonesha magamba kuelemewa katika medani ya kisiasa na kiuongozi wameanza kutapatapa na kupoteza mwelekeo.

Nashauri tume huru ya kimahakama iundwe uchunguze na kutoa ripoti yake kwa wananchi (cc bunge na serikali)
 
Wakati mwingine nasikitika tunaposhindwa kutumia akili zeru vizuri.... Hivi polisi wetu hawa ambao hawajawahi kusikia bomu mitaani wakiwa na silaha huwezi kufikiria akili ya kwanza kabisa kwao ni kwamba wao ndio walikuwa target na kwamba kwa kuwa walikuwa na silaha watakuwa wa Kwanza wao kurusha risasi kama kujilinda? Tumieni akili please acheni kuwa waganga wa Kienyeji!

Kwa sasa hakuna mTanzania wa chama chochote anaweza kufanya yaliyofanyika.

Umanena Mkuu.
 
Kuifikiria kenya inahusika ni mawazo dhaifu maana lazma ujue watalii wengi wanaokuja TZ wanapitia hapa Nairobi either on-transit au kwa mawakala wa utalii wa hapa. Kamwe serikali makini km ya kenya haiwezi si kufikiria wala kutekeleza njia hizi za kipuuzi

Adui yuko ndani ya chama cha sisimu na serikali yao waliyounda na pia inamjua muhusika wa haya mauaji ya kisiasa ndio maana hawataki tume ya kimahakama iundwe kuchunguza. Ukiona penye usiri ujue kuna jambo limefichwa na kwasababu hali halisi yaonesha magamba kuelemewa katika medani ya kisiasa na kiuongozi wameanza kutapatapa na kupoteza mwelekeo.

Nashauri tume huru ya kimahakama iundwe uchunguze na kutoa ripoti yake kwa wananchi (cc bunge na serikali)
 
Nadhani wengine wanaochangia humu si watanzania. Pia naamini ninachokidhania ni cha kweli. Nimesha wahi kusema humu kuwa lazima tuwaze tukiwa katikati na siyo kuegemea upande mmoja. Siku zote adui huangalia udhaifu uliopo kati ya adui na adui mwinggine. Hapa ndipo Manyerere anapopagusia na si pengine na kutualika kufanya tafakuri upya. Lakini watu ambao si watanzania wanataka kutuaminisha kuwa hili ni swala la kisiasa na si vinginevyo. Mimi ninachoamini hakuna mwanasiasa mwenye nia ya dhati ya kuikomboa hii nchi kati ya tunaowaona sasa na hivyo wenye nchi twapaswa kujiweka katika hali inayotutaka kufanya kazi kwa bidii na kufikiri kwa mtazamo za zaidi ya siasa au social diferences.

Manyerere mimi nakubaliana na wewe na ndivyo tunapaswa kutafakari vyema. Mmoja amakuuliza kuwa uchunguzi uliofanywa na polisi uliupata? Basi usimpe jibu bali muulize nani aliupata na kama hatuta upata basi tuandamane tupigane kwa mabomu au tupambane kwenye sanduku la kura tupate ladha nyingine? Au swala la kibanda waulize wakupe historia ya kibanda zaidi ya historia ya kisiasa au uhusiano wake na mbowe baada ya kupewa 200milion ya overhaul tanzania daima lakini baada ya miezi miwili aliandika makala gani na kwenda kusaini mkataba na mtu mwingine nairobi? Kingine ni gesi, unadhani ni tajiri gani kama IPTL, Symbion. agreko etc atataka gesi ije Dar mradi wa kuinyonya nchi kupitia wajanja wachache kiulaini hivyo?

Sina nia ya kuanika mambo ya watu humu bali nia ni kuwafungua watu kuwa balanced hasa katika kufikiri, tuanzie zero badala ya kuchukua vitu juujuu na kuanzia 50% up.

Nchi yetu ipo pabaya hasa katika maeneo muhimu, tuache siasa chafu za kupandikizwa tushikamane tuikomboe hii nchi. Manyerere usikate tamaaa.
 
Usitupotoshe. Mkenya avae sare za polisi, auwe raia, then apokelewe na jeshi la polisi na kukimbizwa na gari kutoka eneo la tukio???:heh: Na kwanini kwenye mkutano wa CDM?? Usitake kuharibu mahusiano yetu na jirani zetu, labda ingekuwa Rwanda (maybe)
 
Wakati mwingine nasikitika tunaposhindwa kutumia akili zeru vizuri.... Hivi polisi wetu hawa ambao hawajawahi kusikia bomu mitaani wakiwa na silaha huwezi kufikiria akili ya kwanza kabisa kwao ni kwamba wao ndio walikuwa target na kwamba kwa kuwa walikuwa na silaha watakuwa wa Kwanza wao kurusha risasi kama kujilinda? Tumieni akili please acheni kuwa waganga wa Kienyeji!

Kwa sasa hakuna mTanzania wa chama chochote anaweza kufanya yaliyofanyika.
Kasheshe,

..I dont think it is OK kwamba bomu likilipuka mtaani basi Polisi waongeze maafa kwa kufyatua risasi hovyo na kurusha mabomu ya machozi.

..kwa uelewa wangu bunduki walizokabidhiwa Polisi ni kwa ajili ya kulinda wananchi kwanza. Polisi anatakiwa kumuokoa mwananchi kwanza, ndipo ajiokoe yeye mwenyewe.

..we need a more efficient and disciplined police force kuliko hili tulilo nalo sasa hivi. kwenye nchi za wenzetu wananchi wanajivunia majeshi yao ya polisi. wananchi na polisi wana mahusiano mazuri.

..maafa kama haya yanapotokea ilitarajiwa polisi na wananchi wafanye kazi kwa pamoja, na siyo Polisi kuwatwanga risasi wananchi, na kuua watoto wadogo.

..mwenendo wa jeshi letu la Polisi wakati wa maafa ya Arusha ni AIBU kubwa kwa taifa letu.

NB:

..nimeangalia video inayoonyesha mlipuko wa bomu la arusha. kwa kweli inasikitisha sana kusikiliza sauti ya kijana wa matangazo wa CDM aliyekuwa akipiga mayowe ya kuomba msaaada.

cc: Lilambo, Nguruvi3, Manyerere Jackton
 
Kuifikiria kenya inahusika ni mawazo dhaifu maana lazma ujue watalii wengi wanaokuja TZ wanapitia hapa Nairobi either on-transit au kwa mawakala wa utalii wa hapa. Kamwe serikali makini km ya kenya haiwezi si kufikiria wala kutekeleza njia hizi za kipuuzi

Adui yuko ndani ya chama cha sisimu na serikali yao waliyounda na pia inamjua muhusika wa haya mauaji ya kisiasa ndio maana hawataki tume ya kimahakama iundwe kuchunguza. Ukiona penye usiri ujue kuna jambo limefichwa na kwasababu hali halisi yaonesha magamba kuelemewa katika medani ya kisiasa na kiuongozi wameanza kutapatapa na kupoteza mwelekeo.

Nashauri tume huru ya kimahakama iundwe uchunguze na kutoa ripoti yake kwa wananchi (cc bunge na serikali)

Umenena.. Kenya waharibu arusha then watalii wanaokuja arusha na Kilimanjaro wapiti wapi?? be a great thinker man..
 
Back
Top Bottom