Mabinti wote wa First Year Kuja Hapa: Part 1:

Mabinti wote wa First Year Kuja Hapa: Part 1:

thetruthtobetold

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2018
Posts
509
Reaction score
561
Huu ni wito kwa Mabinti wote wa first year Katika vyuo vikuu na vocational trainings ambao wameeingia kwenye uhuru wa Kujisimamia baada ya Kumaliza Secondary School. Mimi nimeoa na nina mke na watoto kwa hiyo ninaamini nina uwezo wa kuwashauri, mnisikilize kwa makini, mnaweza mkapata kitu cha kuwasaidia.

Mnapoanza chuo mmetoka mikononi mwa wazazi wenu, ni mda ambao mnaufurahia sana, na kuona kama uadui wa kufuatwa na Wazazi umeisha, yawezekana ulikuwa unachungwa sana, hutoki ndani na mambo mengine, kwa hiyo uhuru unaoupata sasa unakupa raha na furaha sana sana!

Kwanza ninataka kuwaambia kwa style yeyote ya Upendo wazazi wenu waliotumia kuwalea ni watu wema sana (KAMA PALIKUWA NA UPENDO), na muwashukuru sana, wengine waliwafungia, wengine waliwapa uhuru, kila mtu na style yake, lakini cha Msingi ni kwamba walikuwa na nia nzuri na nyie sana sana, WASHUKURUNI SANA kwa hayo.

Mnapofika chuoni kwa mara ya kwanza, hii ni fursa ya kuanza kuvuruga au kutengeneza maisha yako. Haijalishi nyuma umekoseaje na umefanya mabaya mangapi, lakini huu ndio wakati wa kurekebisha, na kufanya mambo mazuri ya kutengeneza maisha yako! Kumbuka upo hapo kusoma, na pia kujifunza mahusiano na namna Kaka zenu walivyo (KWA UANGALIFU SANA SANA).

Kwa Leo ninawaambia mambo muhimu ya kuzingatia unapofika chuoni mara ya kwanza au hata baada ya mda fulani:

1. MASWALA YA IMANI NA DINI:


- HAKIKISHA UNAJISAJILI KWENYE KIKUNDI CHA DINI CHA IMANI YAKO:

Hili ni jamboa muhimu sana, sitaki kusema kwamba watu wa dini ni wazuri, hapana kuna mazaifu yao mengi sana, na tena wakati mwingine wana ushawishi mbaya, ila hawawezi kuwa wote. Ni Muhimu sana kuonyesha msimamo wako na wa dini yako. Jisajili effectively kwenye kikundi chako cha dini.

Hii Dunia tunayoishi ina unafuu kwa sababu watu wanaogopa kuna superpower, Imani, na Kwa namna fulani imani zetu zinatuweka pamoja! Ni muhimu sana kwa mwanafunzi kukumbatia kikundi chako cha dini, jiandikishe, kuwa active hudhuria vipindi vya shulenie vya dini (KWA HEKIMA).

- TAFUTA MLINGANO WA DINI NA SHULE:

Jua lengo kuu la kuwa hapo ni kusoma, na Imani is a means to achieve that, ofcourse Imani ni number one, ila kuwa tu na hekima kutafuta balance! Make sure una balance the two! Soma kwa bidii sana, avoid mikusanyiko nje ya campus ya chuo isiyokuwa na lazima (LABDA IWE NA LAZIMA SANA SANA).

- EPUKA UKURUPUKAJI WA KUCHUMBIWA

Huku kwenye makundi ya dini na Imani, vijana wa Ki dini wanapenda sana kuchumbia, na ndio ngono zembe huanzia hapa! Kuwa mwangalifu sana kufikia haya mambo, hauko hapo kutafuta mme, upo hapo kusoma, KITU PEKEE CHA KUFANYA KWENYE SWALA LA KUTAFUTA MME, BE A GOOD AND RESPECTED LADY, hicho tu kinatosha, usikubali kuchumbiwa chumbiwa kirahisi. Hii tabia wanayo sana walokole.

- MWILI HAUNA IMANI WALA DINI, NI ROHO

Ukicheza utaingia kwenye mahusiano ya mapenzi bila kukusudia. Hii nimeiona sana kwa walokole, kukaa na wanaume mda mrefu kwenye mabweni ya wanawake ETI WANAFANYA BIBLE STUDY, bila nidhamu, mnalegeza macho na kuangaliana, ukichelewa utakutwa chupi ishashushwa, na utakuja kujilaumu sana, ni muhimu sana ukaweka mipaka na kila mtu, hata KIJANA ANAYEONEKANA ANA IMANI KAMA MOUNT EVEREST, WEKA NIDHAMU, na usiwe mrahisi.

- MWOMBE MUNGU KWA UAMINIFU SANA:

Kwa imani yako mwombe Mungu akusaidie na akuepushie mahusiano mabaya! Hapa nitaongea kwa mtazamo wa Kikristo maana ndo imani yangu! Mwombe Mungu, na kama umejazwa na roho Mtakatifu omba kwa Lungha, sana, na kama ujajazwa jitahidi ujazwe. Mungu yupo kutusaidia, Mwombe, Mwombe na Umwombe tena........


Itaendelea ........
 
Watakoma, hii ndo part 1[emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Back
Top Bottom