Mabinti wa kisasa hebu acheni uongo usio na maana

Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
13,096
22,621
Habarini wadau. Naandika hii kitu hapa baada ya kukerwa na tabia za baadhi ya mabinti especially hawa wamjini ambao wameanza kurithi tabia zile walizokuwa nazo wanaume za "kuna hela na isikilizia" halafu baada ya dakika kumi utasikia "una elfu tano au kumi ya karibu hapo".

Ipo hivi, kuna wadada kadhaa nimenotice wanahii tabia katika mazungumzo kukuaminisha wao ni watu wa mipango mikubwa. Na hata wanavyojiweka ni as if ni watu muhimu sana hapa mjini but ukweli wa mambo ni wabangaizaji wasio na mbele wala nyuma.

Kuna m'moja ameshakuwa na tabia ya kunicheki kuniomba kuniazima gari akisema ana wageni sijui wanakuja kutoka nje wanahitaji usafiri watakaotumia wakiwa hapa mjini.

Nikamkata nikamwambia twende nitakupeleka safari yako. Nimekwenda mchukua yupo na wenzake wawili, wanasema wanaenda serena kufika hapo serena wanaangaliana yale macho ya tumeumbuka, mimi nikaona wananipotezea muda maana waliniweka zaidi ya nusu saa hapo kwenye kiti sehemu ya kusubiria kisha mwenzake nisie mjua anakuja niomba ufunguo kuwa anaomba aende pale posta ATM mara moja kisha aniletee, nikamwambia ngoja twende sote na mimi nilikuwa naenda huko, tukaenda kufika pale CRDB anatoa toa macho (sidhani kama hata alitoa hela alipoingia kwenye ATM mule). Nikamrejesha serena kisha nikampigia mwenzake nikawaaga nikawaambia nina dharula nitawareje, sikurudi tena.

Mwingine kila nikichekiana nae story zake ni "kuna jamaa tuna contract nae katika ile kampuni yangu, hapa ndio naangalia contract inakaribia kuisha ili nionane nae tukasaini mkataba mwingine" ukimuuliza mnadeal na nini katika kampuni yako, ooooh apartments kwa foreigners, tuna import na kuexport bidhaa etc, halafu hapo hapo anakupiga kibomu cha msosi. Au anaomba umnunulie soda tena anachagua yeye anataka soda gani.

Mwingine nilishapiga hadi mashine, shida ikaja baada ya kumleta maskani. Ni mwanamke ambaye hana impact ndani ya nyumba ukiachia kukuomba hela ndogo ndogo bila utaratibu as if mission yake ni kuhakikisha hauna hata mia mfukoni.

Ukiachia kulala hadi saa nne asubuhi kulala tu kitandani anachat na kupiga simu za kuongea na mashost zake na hakuna la maana wanaongea zaidi ya kupeana umbea wa juzi waliposafiri au bata sijui kumuongelea mtu gani, hawana mazungumzo ya maana.

Ila mtu huyu huyu ukiongea nae anaongelea kuhusu kufanya kazi katika NGO iliyomlipa milioni 2. 7 take home na imefungwa kipindi cha magufuri.

Mara akwambie anasomesha wadogo zake international schools, na anamhudumia mama yake mwenyewe. Mara akwambie sijui anataka ajiajiri anataka kufungua kampuni ya beauty and cosmetic ambayo ataiweka kule masaki au oysterbay na inalipa sana. Mara aseme yeye ni CEO haoni haja ya kuajiriwa.

Ila ukitoka kwenda dukani nje, utaona text kutoka kwake imeingia beib, ukirudi niletee Cadbury bars mbili na maziwa ya asas au utasikia niletee sausages na apple juice ya ceres kubwa. Anaagiza hivi kwa confidence kabisa utadhani mimi ni babake.

Unakuta mpo kwenye foleni barabarani inapita vogue utasikia one day lazima nita own hii gari...... Nina rafiki yangu ana jaguar hii ya 2018 and she's only 25, yaani i must get there....

Sasa huwa nawatazama nasema hivi hawa ni kwamba hawaoni uhalisia wa maisha yao au ni vipi. Watu wana maisha ya kubangaiza, wanatoka katika very common families za kitanzania ambazo wazazi ni wastaafu na hawana hela.

Why mtu usiwe humble na kuishi according to your level requirements wakati unaplan kuwa mkubwa baadae....?!

Why uishi maisha ya kufake fake na uongo mwingi ile hali hauna uwezo na ni tegemezi by 150%?!

Kuna haja gani ya kunidanganya kuwa kuna report naandika mara sijui kuna email muhimu nataka nijibu hapa.... Au unanipigia simu au kunitext whatsapp baada ya kuniona online saa saba usiku halafu unanifix kuwa Atm imemeza card na hauna balance muda huo unaomba nikuazime 50,000 utanirejeshea asubuhi, halafu asubuhi ikifika unapiga kimya naona tu upo online unapost status unakaa kimya wiki, hatimae mwezi na miezi?!

Au unaniazima laptop unasema kuna a very serious work unahitaji kutype (hata haujulikani unajishughulisha na biashara gani mjini). Kisha nakupa tu bila ya kukuuliza swali lolote zaidi ya utaniletea lini, cha ajabu dakika chache baadae baada ya kukupa laptop unanitext kuniuliza file ya movies ipo upande gani?! Unakaa na laptop yangu zaidi ya wiki hadi naanza kuiulizia na hapo bado utanambia sijui kuna mgeni kaja anacheki movie, anamalizia utaniletea!

Why mnakuwa waongo waongo watoto wa kike?!
 
Hayo maisha ya wadada yako mkoa mojawapo nyanda za juu kusini aisee wale ni waongo balaa

Kati wadada 10 2 au 1 ndo anaweza kusema ukweli

Huyu atakwambia ana maduka matatu, Dar anaenda mara 2 kwa wiki kufata mzigo kumbe uongo mtupu, hapo hapo anakupigia kukuuliza uko nyumbani nije kupika, sasa unajiuliza hayo maduka vipi!

Mwingine atakwambia yuko chuo ukimuuliza unasoma chuo gani au unasomea nini aaa utasikia tuache hayo

Mwingine anakwambia ana duka la vipodozi ukimwambia twende nikuchangie utaona chenga zake.

Unabaki kujiuliza kwa uongo unashika kasi kiasi hiki!
 
Me mwanamke sasa hadi nifanane tabia na wanawake?! Halafu sijakwambia hawa ni wanawake ninao date nao. Nimekwambia ni tabia nimeiona kwa baadhi ya watoto wa kike.....

Sio wote wapo hivi!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa mkonk wako umetype kuwa hizo tabia zilikuwa kiumeni😂 kwahiyo Ni wazi na wewe Ni kaongo kaongo tu😂,

Uliowaelezea wote umekuwa nao kingono ama ulitaka kuwa nao kingono

We Ni walewale

By the way tumejua una gari😂😂😂
 
Achana nao hao mkuu fanya mambo mengine.. Ukiwachunguza unaweza kupasuka kichwa ni hawaelewek.
 
Mkuu hao mabinti hawana shida yoyote, shida ni wewe maana mtu timamu na aliye serious na maisha hawezi usingeweza kuombwa na tu binti eti umfate kwake akupigishe route akakukalishe masaa mawili, mara akuombe funguo mara umpeleke bank

Una shida kichwani
 
Kuna watu wanaweza wasiuamini huu uzi mkuu .
Ila wanawake wa hivo wapo kabisa mjini mpaka unashangaa kwanini anakudanganya wakati uwezo wa kumsaidia bila huo uongo wake upo.

Mimi kuna huyo nae ni full mauongo afu hata pesa ya vocha inampiga chenga ila akikwambia miradi yake utamuogopa. Cha ajabu kumbe sio kwangu tu ni wengi anawapiga vizinga vya vocha afu baadae katika story story anawatajia miradi yake ya mamilioni. Sasa unajiuliza huyu ni mfanyabiashara mkubwa wa mchele hapa mjini kwa maneno yake analeta mpaka tani ya mchele kutoka mikoni.

Ni mfugaji mzuri na ana frem ya nguo hapa mjini(maneno yake hayo). Sijui ni miradi iliyo kichwani mwake tu maana ukitaka akuuzie hata kimoja anachodeal nacho anakupiga kiswahili. 😁😁

Daah dunia inaenda kasi sana, bora sisi wanaume target yetu inakuaga ni kupata papuch sasa wao sijui huwa wanatarget nini baada ya kujitapa na kujipa ufahari huo.
 
Kwa mkonk wako umetype kuwa hizo tabia zilikuwa kiumeni kwahiyo Ni wazi na wewe Ni kaongo kaongo tu,

Uliowaelezea wote umekuwa nao kingono ama ulitaka kuwa nao kingono

We Ni walewale

By the way tumejua una gari
Mbuzi kabisa wewe.

Ila ipo hivi, sio kwamba hawa mabinti nina date nao. Nimesema miongoni mwa mabinti nimeshadate nao nilishamuona m'moja ana hii tabia. Lakini wengi wao ni wale wanawake nakutana nao katika social circles zangu huku mjini na mtaani.

So tabia hii naiona sana. Yaani its like mtu anajihami ili asionekane ana maisha ya ajabu au maisha ya kubahatisha.

Ni ile miss independent virus imefikia katika critical stage ya kumdhuru host.

Its okay kwa binti wa secondary, advanced au chuo kuwa na imaginary day dreaming attitude kwa watu wengine ila sio kwa mtu ambaye amemaliza chuo yupo mtaani, hana mahusiano serious wala hayupo katika ndoa. Hii ni hatari sana.
 
Hayo maisha ya wadada yako mkoa mojawapo nyanda za juu kusini aisee wale ni waongo balaa

Kati wadada 10 2 au 1 ndo anaweza kusema ukweli

Huyu atakwambia ana maduka matatu, Dar anaenda mara 2 kwa wiki kufata mzigo kumbe uongo mtupu, hapo hapo anakupigia kukuuliza uko nyumbani nije kupika, sasa unajiuliza hayo maduka vipi!

Mwingine atakwambia yuko chuo ukimuuliza unasoma chuo gani au unasomea nini aaa utasikia tuache hayo

Mwingine anakwambia ana duka la vipodozi ukimwambia twende nikuchangie utaona chenga zake.

Unabaki kujiuliza kwa uongo unashika kasi kiasi hiki!
Umeongea inshu ya chuo umenikumbusha moja hivi
huyu dem nilikuatana nae kwenye harusi tukapiga story mbili tatu nima acquire namba ake ya sim

kipindi tupo harusini alinambia yupo advnc anaingia 4m 6 nikamuuliza comb anayo chukua aksem PCB bas katk kumuhoji masomo yanaendaj kwa kumuuliza baadhi ya masomo nikaona mtu kijasho topic zingine hajui anasm hiyo isha futwa nikampotezea lengo mm ni utelez tyr kaisha nihamisha
nimechukua nmba ake ilikua mwez wa 12 sikuwahi mtafuta km mwezi hv na sehem
feb akja nitafuta mwenyewe tukapiga story kumuuliza wap iyo ksema yupo chuo sikutaka kumkumbushia ya nyuma nikmuuliza upo chuo gani aksema sauti mwanza ohoo fresh bas koz gan apo unachukua ndipo nilipo choka
ansema yupo sauti anachukua Nursing sauti sasa nikamuuluza upo sauti hii ninayo ijua mm au aksem ndio hiyo sasa sikumlazia dam nikwambia sawa upo venue gan nije coz na mm nipo chuoni apa akanikwepa ety lecture kaingia atanitafuta kimyaa hakunijib kimy

mpaka leo
 
wewe huna shughuli?? au ulitaka tujue unao usafiri kafiri!!!.........hakika kuna jamaa kakuambia...ndege wafananao.............................yuko sawa hakii...
Mimi nina shughuli na ina eleweka hata mtu akitaka jua ofisi yangu nampeleka na ananiona kabisa ni muajiriwa na nina shughuli zangu.

Ila hapa kuna agenda ya tabia ya kuongea uongo uongo ili uonekane wewe upo vizuri ile hali uwezo hauna. Why sasa udanganye na kupiga sound?!

Me watu wa hivi akiniomba hata buku simpatii maana nahisi ananichora.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hao mabinti hawana shida yoyote, shida ni wewe maana mtu timamu na aliye serious na maisha hawezi usingeweza kuombwa na tu binti eti umfate kwake akupigishe route akakukalishe masaa mawili, mara akuombe funguo mara umpeleke bank

Una shida kichwani
Soma tena haujanisoma vema mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom