Mkuu mimi nina mtazamo tofauti na wako. Mara nyingi uwa naona mada za mwanamke kuolewa akiwa na miaka fulani, kuzaa akiwa na miaka fulani na mengine mengi ambayo yapo limited according to you guys. Lakini mimi nafikiri wanaume hasa wanapaswa kuwa macho katika suala la muda au miaka.
Sisi wadada mnadai tukifika miaka 28 or more hatupendezi ila si kweli. Hata msichana mdogo ambaye ataolewa mapema unaweza kukuta anafanana na bibi na yule ambaye hajaolewa na 30s yuko poa sana. Hapa nafikiri shida ni aina ya maisha tunayoishi. Maana nikiwahi kuolewa kwamba nitakuwa sivutii maana yake nikiwa kwenye ndoa mume atanichoka nikianza kutomvutia, kesho ataleta wanawake wengine wachanga nianze kupata stress. So hapa niconclude kuwa miaka haimfanyi mtu aonekane mbaya ila maisha anayoyaishi kwa kiasi kikubwa ndiyo yanayomchakaza.
Kwa upande wa wakaka. Mnadai wanaume wanaweza kuoa hata wakiwa 40 au 50. Nafikiri wanaume hasa ndio walipaswa kubeba jukumu la kuoa mapema zaidi ya sisi kuolewa mapema. Sisi tunatoka kwetu na tunahamia kwa mume. Kwa hiyo ni mwanaume ndiye anayepaswa kuanza kujipanga maisha ili aweze kuoa mwanamke anayeendana naye kiumri.
We una miaka 50, unaoa mtoto wa miaka 18 kisa unajipa moyo kuwa mwanaume anaweza kuoa akiwa 50 or more, je mnawaza hata hao watoto mnaopata mtaishi nao muda gani hapa duniani? Maana kufika 50 kwa maisha yetu ni bahati. Na huyo mtoto unayemuoa je kuna upendo wa kweli au yeye naye amekufata kwa kuwa hana maisha? Ndio yale akiwa na agemate wake, mzee uje ujfe kwa presha. Ndio maisha mnayoyaongelea!
All in all, muda sio kitu cha kuchezea. Haurudi nyuma. Si kwa mwanamke au mwanaume. Kila mmoja anapaswa kufanya kitu cha msingi ndani ya muda. Kama ni kusoma soma kwa bidii, kama ni kazi fanya kwa bidii. Ndoa na maisha mengine ambayo yakiwepo au yasipokuwepo yasiwape stress mpaka wadada wakaenda kujibebesha mimba kwa lazima ili kuforce ndoa sababu ya mada za namna hiyo humu jf. Vitu vingine ni baraka toka kwa Mungu.