Mabilioni yakusanywa kumwangusha Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabilioni yakusanywa kumwangusha Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Apr 18, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Apr 18, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,805
  Likes Received: 83,184
  Trophy Points: 280
  Mabilioni yakusanywa kumwangusha Kikwete

  Na Saed Kubenea

  MwanaHALISI~Maslahi ya Taifa Mbele

  RAIS Jakaya Kikwete atahitaji kutumia nguvu mara tatu kukabiliana na “genge” linalotaka kumzuia kugombea urais kwa kipindi cha pili, MwanaHALISI limeelezwa.

  Taarifa zilizopatika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki zilisema, wanaotaka kumzuia Kikwete kugombea urais kwa kipindi cha pili, wamepanga kutumia, na tayari wamekusanya Sh. 2.5 bilioni kwa shughuli hiyo.

  “Hizi si fedha kidogo. Lazima CCM ijipange kutumia mara tatu zaidi (Sh. 7.5 bilioni) kama inataka Kikwete apite,” ameeleza mpasha habari.

  Fedha za wanaompinga Kikwete zinalenga kununulia magari, pikipiki, baisikeli, sare – suruali, fulana, khanga na kapelo; mabango na vipeperushi.

  Nyingine zimepangwa kutumika katika ununuzi wa mafuta kwa ajili ya magari, posho za wapigadebe na “takrima” kwa wabunge ambao wataamua kuwaunga mkono kwa kuchomoka kwenye mkondo mkuu wa CCM.

  Wiki iliyopita, aliyekuwa mwenyekiti wa mkoa wa Dar es Salaam, Hemed Mkali, aliliambia gazeti la NIPASHE kuwa lazima kila juhudi ifanywe “kuzima mahangaiko ya wanaotaka kugombea urais” mwaka 2010 vinginevyo CCM itaangamia.

  Mkali alikuwa akisisitiza hoja ya wastaafu wa CCM ambao siku moja kabla ya kauli yake walitahadharisha mgawanyiko ndani ya chama chao, wakisema utatokana na kugombea urais mwaka kesho.

  Viongozi wengine waliotoa rai ya kuvunja “mahangaiko ya kugombea urais” ni aliyekuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Pancreas Ndejembi, aliyekuwa mwenyekiti wa mkoa wa Iringa, Tasil Mgoda na aliyekuwa mwenyekiti wa mkoa wa Pwani, Jumanne Mangala.

  Akizungumza na MwanaHALISI kwa njia ya simu juzi Jumatatu, Mkali alisema yeye na wenzake wanajua wanachosema na kwamba hawakukurupuka.

  Alipotakiwa kueleza kwa undani msingi wa madai yao kuhusu waliomo kwenye mhangaiko wa urais, kwanza Mkali alisita na baadaye alieleza:

  “Tunawafahamu. Wapo watu wengi. Wengine ni viongozi wa juu serikalini na ndani ya chama. Wengine ni ‘marafiki zake’ wa karibu,” alieleza Mkali.

  Alipobanwa kueleza maana ya “rafiki zake,” na huyo hasa ni nani, Mkali alisema kwa sauti ya kubembeleza, “Ndugu yangu, sasa hivi niko Rufiji; si usubiri nirudi Dar es Salaam ili tuongee?”

  Taarifa zaidi zinasema Mkali na wenzake, baada ya kuongea na waandishi wa habari juu ya dukuduku lao, walikwenda nyumbani kwa kiongozi mmoja mstaafu na kumweleza kuwa walikuwa na ushahidi tosha juu ya kile walichokuwa wakisema.

  Haijafahamika iwapo wastaafu waliagizwa na baadhi ya viongozi wa CCM au serikali ili kuvunja ukimya juu ya kinachoendelea; lakini kwa nafasi yao ya sasa hawakutegemewa kuwa na maslahi ya kuwafanya kuwa mstari wa mbele.

  Wiki moja kabla ya wastaafu kuvunja kimya, makamu mwenyekiti mstaafu na mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu ya CCM, John Samwel Malecela alisema wanaotaka kuchuana na Kikwete kutoka ndani ya chama hicho wanajisumbua.

  Aliwaambia waandishi wa habari, nyumbani kwake Sea View, Dar es Salaam kuwa mgombea wa CCM mwaka 2010 ni Jakaya Mrisho Kikwete.

  Kauli ya Malecela na zile za wenyeviti wa mikoa wastaafu, haziwezi kuwa mlolongo wa porojo mitaani bali majibu kwa kile ambacho kinachemka ndani ya nyoyo na vikao vya siri vya wanachama na viongozi.

  Gazeti hili liliandika Oktoba mwaka jana kuwa kulikuwa na njama za kumg’oa Kikwete. Lilifungiwa kwa siku 90 kwa madai ya wizara ya habari kwa akile kilichoitwa kufanya “uchochezi.”

  Toleo Na. 118 la MwanaHALISI liliandika kuwa watuhumiwa wa ufisadi nchini walikuwa wamejipanga kumg’;oa Rais Kukwete ili asigombee urais mwaka 2010.

  Gazeti lilinukuu taarifa zilizosema wapinzani wa Kikwete walikuwa wanataka kumfanya awe “One-Term President” – rais wa kipindi kimoja, lengo likiwa kumwadhibu kwa kile kilichoitwa kuwasahau wenzake na kutowatetea walipoingia katika matatizo.

  Tangu hapo, vyombo vya habari mbalimbali, yakiwemo magazeti ya serikali na CCM, vimeandika juu ya njama za “kumzuia Kikwete kugombea urais” Oktoba mwaka kesho.

  Mbunge wa Maswa ambaye alijitosa katika kinyang’anyiro cha urais mwaka 2005 na kushindwa katika hatua za awali, John Shibuda tayari ametangaza kumpinga Kikwete katika uchaguzi mwakani.
   
 2. J

  JokaKuu Platinum Member

  #2
  Apr 18, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,098
  Trophy Points: 280
  ..bora tungeelezwa Kikwete alitumia billioni ngapi kuutafuta Uraisi from 95 mpaka 05 alipoupata.

  ..vilevile Kikwete ana mpango wa kutumia billioni ngapi kutetea nafasi yake 2010?
   
 3. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hao wanaotaka kumpinga Kikwete naombea waendelee na dhamira yao hiyohiyo mpaka mwisho tuone kina Malecela watakuwa na ubavu wa kuwazuia.Waache waparuane na kama kugawanyika sisi walalahoi tunasema hewala!
   
 4. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #4
  Apr 18, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,315
  Likes Received: 5,609
  Trophy Points: 280
  Hao wote wanajuana na umeshasikia ni marafiki zake .....sisi tukae kimya??maana watatuwekea fmgombea fisadi au anewabeba mafisadi....kwa kweli kama BWM angekuwa uwezo kuwazuia mtandao...na kuweka mtu wake nadani nchi ingetawalika.mm-la sababu mtandao una nguvu kubwa na pesa....awa jamaa watatuchagulia rais for the next 20 yrs....
   
 5. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #5
  Apr 18, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Upinzani ya ccm unaweza kuja pale tu wachache wataona inawezekana wakauchukua uraisi! Bado navuta pumzi na subira, mpaka hapo nitakapoona majina ya wagombea ndani ya ccm
   
 6. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #6
  Apr 18, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,600
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  Kitu ambacho kimefichwa katika habari hii ni kuwa je ni akina nani hasa?

  1. Je ni mafisadi kama ambavyo kubenea ameshawahi kueleza huko nyuma??
  2. Je ni watu safi ambao wanataka mabadiliko ndani ya CCM?

  Taarifa kama hii inabidi iwe na closer look, kwani mara nyingi nimeshuhudia watu wakisema mafisadi wana njama ya kumwondoa JK , wakati in other hand ni mbinu ya kumfanya Kikwete aendelee na madaraka, kwa kuwadanganya watanzania kuwa JK ni masfi na anawapinga mafisadi, wakati yeye na mafisadi ni baba mmoja na mama mmoja!

  Kubenea may be sijaelewa taarifa yako, lakini acha nichukiwe, kwa hali ya uangalifu sana umekuwa ukimfagilia kikwete, watu wameona na rumors za kuwa hilo gazeti ni la JK, liko kuwakomoa makundi mengine ya mafisadi wakati wao wenyewe ni mafisadi!

  by the way kesi yako imeishaje, polisi haijawapata tu waliokumwagia tindikali?????
   
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  Apr 18, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Waberoya,
  Ukiisoma taarifa kwa makini na fedha walizokwishakusanya jibu litakuwa moja tu: ni mafisadi ambao wanaona mwenzao Kikwete amewatupa au kuwatema. Hii si dalili njema kwa nchi.
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Apr 18, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,805
  Likes Received: 83,184
  Trophy Points: 280
  Waberoya, kwa maoni yangu walio safi ndani ya CCM ni wachache sana na hawana ubavu wowote ndani ya chama hicho maana chama kimeshashikwa na mafisadi. Sasa mafisadi wanapambana wenyewe kwa wenyewe. Inasemekana kuanzia jana kulikuwa na vikao vya juu vya CCM ambavyo vitaendelea hadi J'tatu, kwa maoni yangu hakutakuwa na jipya lenye maana yoyote bali ni USANII MTUPU!!!
   
 9. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #9
  Apr 18, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Naona Kubenea hapa naye ni jitihada ya kuuza gazeti lake kwa kuweka habari ambayo si ajabu haina ukweli kabisa.

  Siamini kabisa kuna kundi la maana ndani ya CCM linataka kumpinga JK hapo 2010.

  Kinachoendelea sasa ni watu kuandika mambo kwa hisia na kwasababu hawawajibiki kutoa ushahidi basi wanaendeleza lile lile gumzo la kwenye vijiwe.

  Ni mambo yale yale ya mwaka 2005 kwamba Malecela kachukua pesa Iran, kabadili dini nk. Baadaye ikaja onekana ulikuwa utumbo mtupu.

  Tusubiri hiyo 2010 na tuone kama hizi habari zina ukweli wowote zaidi ya kuweka vichwa vya habari ambavyo ni rahisi kuuzika mitaani.

  Kwa anayejua jinsi CCM wanavyochagua rais, sioni kwa vipi mtu anayetaka kushinda urais anaweza kumshinda JK kwenye kamati kuu ya CCM?

  Nawasifu thisday kwa kuwa muda wote wanatanguliza facts kabla ya kuja na conclusions, tofauti na haya magazeti mengine ambayo yanajenga hoja kwa foundation mbovu kabisa.

  2010 si mbali na tutajua tu.
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Apr 18, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,805
  Likes Received: 83,184
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo unataka kutwambia kwamba wale waliojiita "Wazee wa Chama" walikurupuka tu walipotoa kauli kwamba "atakayempinga Kikwete 2010 atakiona"? Unataka kutwambia kwamba Chiligati, Msekwa na Malecela nao walikurupuka pale walipotoa kauli kwamba 2010 ni Kikwete tu maana wana Utamaduni wao wa kuachiana Rais akae vipindi viwili?

  Kwa maoni yangu nadhani wanajua nini kinaendelea dhidi ya Kikwete ndiyo maana ikabidi waanze kumpigia debe la nguvu Kikwete, vinginevyo hawakuwa na sababu zozote za kutoa kauli zile.
   
 11. Machiavelli

  Machiavelli Member

  #11
  Apr 18, 2009
  Joined: Oct 3, 2007
  Messages: 74
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  The Kikwete veterans have systematically discovered that every flaw associated in the public mind with their hero turns out to be a defining trait of BWM's regime. I am not a trained psychologist, but some form of projection seems to be at work in the present climate of public opinion, direct defenses of Kikwete have limited appeal, so the Kikwetean's mainly argue by implication.
   
 12. Sura-ya-Kwanza

  Sura-ya-Kwanza JF-Expert Member

  #12
  Apr 18, 2009
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 561
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sababu kuu ya kumuangusaha Mh. Kikwete ni kuwasahau na kutowatetea mafisadi!:eek: Hii kali kuliko.

  Kama hakuna sababu sioni vipi hivyo vichuruku 2.5 bilioni vitaweza kumuangusha Mh. Kikwete.

  Narudia, hakuna mwenye sababu kuu!
   
 13. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #13
  Apr 19, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Wazee wa chama waliposema Mkapa aendelee 2000 kwani kulitokea mtu wa kumpinga? Au hamna hata kumbukumbu nini kilitokea kabla ya uchaguzi wa 2000 ndani ya CCM?

  Naamini haya maneno yanaenezwa na watu ambao hawajui CCM inavyofanya mambo yake au magazeti ambayo yanataka kuuza habari.
   
 14. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #14
  Apr 19, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Wale wazee kumbe wanajibizana na watu. Safari hii hawana EPA?
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Apr 19, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,805
  Likes Received: 83,184
  Trophy Points: 280
  2000 hatukusikia kauli kutoka kwa "Wazee wa Chama" ya "atakayempinga Mkapa 2000 atakiona" lakini mwaka huu tumeisikia ya kuhusiana na Kikwete na nina hakika kabisa kwamba "Wazee wa Chama" wasingekurupuka tu from nowhere na kutoa kauli ambayo inaelekea ilikuwa inamlenga kumtisha mtu mmoja ndani ya CCM au kundi la Watu ndani ya CCM. Pia 2000 hatukusikia kauli za 'Ni Mkapa tu 2000'

  Kuna kitu chini kwa chini ndiyo maana kauli hizi zinatolewa, haiwezekani kauli hizi zitolewe bila sababu yoyote maana siku zote panapofuka moshi hapakosi.....
   
 16. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #16
  Apr 19, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mwaka 2010 ni wananchi kuamua kama wanamtaka JK au, haina haja ya JK kuogopa wapinzania kama anajiamini maana kama hana tatizo hana sababu ya kuogopa kwani wananchi watamchagua.

  Wajibu wa JF na vyombo vya habari vingine ni kuakikisha kuwa wananchi wanatumia nafasi yao ya kula vizuri na kuwapa viongozi wazuri
   
 17. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #17
  Apr 19, 2009
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hamna lolote. Hii ni kuuza magazeti tuu ama watu wanajenga hoja zisizo na miguu wala kichwa. Najua wale wazee wa Zipompapompa sasa hivi wanajipanga kwaaajili ya 2015 ndio maana vikao haviishi ila sasa kinachowaumiza kichwa ni kwamba JK atamkabidhi nani kati yao maana anaweza kuwatosa wote vile vile.
   
 18. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #18
  Apr 19, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Dalili moja kubwa ya kufikia mwisho wa mfumo Dume kama wa CCM ni kuzaliwa kwa mapambano ya ndani kwa ndani.
  Kipimo kile kile walozoea kuwapimia wakulima na wafanyakazi wa Tanzania sasa watapimiana wenyewe na kulazimishana kunywa.

  Zoezi hili tunaliombea lidumu hadi mwisho wa ukomo wa utawala wao wa Kimaruk.
   
 19. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #19
  Apr 19, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Mtu akitupwa nje ya mduara wa Kikwete ni Adui wa nchi??

  Waliomo ndani ya mduara wa MH huyu ni watu Safi?

  Kikwete mwenyewe ni safi??

  CCM ni safi?

  Kundi lipi katika hayo mawili ni safi?

  Hitimisho kwamba hii si dalili nzuri kwa nchi umellifikiaje?

  Ni kwa sababu ya kitendo cha Muungwana kukatiziwa muda wake wa kukaa Ikulu??

  Ni kweli CCM ikitoweka uwepo wa nchi uko mashakani au waliozoea kunyonga watashindwa kula vya kuchinja????
   
 20. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #20
  Apr 19, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,805
  Likes Received: 83,184
  Trophy Points: 280
  Madilu, hapa mimi naspeculate naweza kabisa nisiwe sahihi. Nadhani Jasusi aliandika vile kwa sababu wakati wa mapambano ndani ya makundi yaliyopo ndani ya CCM yakiendelea nchi itakuwa haina uongozi kama tunavyoona sasa. Nguvu zote na mabilioni ya pesa yatakuwa yamehamishiwa katika mapambano hayo makali na kila kundi likitaka kuibuka na ushindi ili waweze kuweka mgombea wao 2010.
   
Loading...