Mabilioni yakusanywa kumwangusha Kikwete

Wazee wa chama waliposema Mkapa aendelee 2000 kwani kulitokea mtu wa kumpinga? Au hamna hata kumbukumbu nini kilitokea kabla ya uchaguzi wa 2000 ndani ya CCM?

Naamini haya maneno yanaenezwa na watu ambao hawajui CCM inavyofanya mambo yake au magazeti ambayo yanataka kuuza habari.

Kwa kumbukumbu zangu, Mama Getrudi Mongera alitangaza nia ya kugombea mapema kabla hata kipyenga hakijapulizwa. Ila nafikiri wazee wa chama walimweka sawa kumpisha mheshimiwa. Maana hakurudia tena wala kuonyesha kung'ang'ania kama alivyofanya mzeji (Bilal) 2005 kwa Karume
 
Last edited:
...nashauri kama kuna michango ta kumsaidia kikwete au kumpinga iwe wazi ...we must be open to the source of our campagne monies.....

Kikwete atashinda lakini atadhalilika sana ..ushindi wa kishindo [wa karatasi za china na israel-chameleon paper]...utageuka ushindi mwembamba .....kwani mwaka huu sidhani kama watamudu kununua zile karatasi za bei mbaya!!!!!.....ndio maana unapoambiwa pesa za epa hazina maelezo ..mjuwe zilinunua nini.....??
Na jk amewageuka mafia ambao kwa pamoja waliamua kutafuta pesa za kununua vitu vya aina hiyo....mwaka ujao mafia watakuwa wanaogopa kuchangia au kujiingiza wakiogopa consequence za kuja kushitakiwa na regime itakayokuja!!!!.......jk atategemea zaidi campagne funds kutoka kwa marafiki wa nje ....kama waarabu wa kemps....na funds za tiss....

Lakini mwisho wa siku jk will retire completely akiwa mnyonge na failure ...without any legacy!!!....he get to pull up his sox......
 
habari haijataja ni kina nani lakini nadhani list tunayo na kila m2 anaijua, kuna mchangiaji mmoja ameongelea kuhusu kuona kama Malecela na wenzie watafanya nini kumsaidia JK, lakini mimi simwamini kabisa bwana Malecela aka jumanne, huyo mzee ni dakika 1 tu anakugeuka yaani hilo kundi la mafisadi likiamua kumsimamisha hata kesho anamkana kikwete hadharani, tuwe makini sana na huyo mzee nina wasiwasi mkubwa sana wa yeye kutumiwa na wapinzani wa JK
 
habari haijataja ni kina nani lakini nadhani list tunayo na kila m2 anaijua, kuna mchangiaji mmoja ameongelea kuhusu kuona kama Malecela na wenzie watafanya nini kumsaidia JK, lakini mimi simwamini kabisa bwana Malecela aka jumanne, huyo mzee ni dakika 1 tu anakugeuka yaani hilo kundi la mafisadi likiamua kumsimamisha hata kesho anamkana kikwete hadharani, tuwe makini sana na huyo mzee nina wasiwasi mkubwa sana wa yeye kutumiwa na wapinzani wa JK


na huo ndio ulikuwa ugomvi mkubwa wa mwalimu na malecela ..the guy is bright ila mwalimu alikuwa anamuona hana msimamo!!

kuna taarifa kwenye ranks kuwa hasira za kitabu cha mwalimu....kuna siri aliongea na malecela ,malecela akamgeuka mwalimu akamueleza mwinyi ....wakati walikubaliana ....yeye malecela awe intergral part kumsaidia mwinyi..,bila kuweka wazi ushauri wa mwalimu,...maana ingekuwa kama kumuingialia kazi mwinyi....,nyerere aliposikia habari iliyokuwa siri imevuja ...alihakamaki kwa malecela na kumlaumu kwa kumchonganisha na rais wake.......mwisho wa siku looser alikuwa malecela baada ya mwinyi na nyerere kukubaliana.....nadhani kama kuna mwenye rekodi nzuri ya hili tunaweza weka historia yetu sawa!
 
Wiki iliyopita, aliyekuwa mwenyekiti wa mkoa wa Dar es Salaam, Hemed Mkali, aliliambia gazeti la NIPASHE kuwa lazima kila juhudi ifanywe "kuzima mahangaiko ya wanaotaka kugombea urais" mwaka 2010 vinginevyo CCM itaangamia.
Mkali alikuwa akisisitiza hoja ya wastaafu wa CCM ambao siku moja kabla ya kauli yake walitahadharisha mgawanyiko ndani ya chama chao, wakisema utatokana na kugombea urais mwaka kesho.
Hiki si kichekesho kingine! kwani akuitokea mtu mwingine akamshinda Kikwete kwenye kinyang'anyiro cha kuwania ugombea, CCM itashindwa? Ina maana kuwa nguvu za CCM ni Kikwete?
Kama ugombea urais unaweza kuleta ugomvi wa kiwango hiki, nini maana ya demokrasia ndani ya cahama hiki kikongwe?
 
wana JF wenzangu, mimi ninachoamini KUBENEA huandika habari zake kuuza magazeti kwa mantiki ya biashara tu, maana yeye hafanyi uchunguzi wa habari anazoandika ila huunganisha tetesi au fikira fulani kuzifanya kama vile ni true story. Gazeti lake halina chochote ukilinganisha na thisday au kulikoni ambayo utaona kinachoandikwa ni kweli kimefanyiwa uchunguzi na ni kweli tupu, siyo kama gazeti la KUBENEA
 
Hiki si kichekesho kingine! kwani akuitokea mtu mwingine akamshinda Kikwete kwenye kinyang'anyiro cha kuwania ugombea, CCM itashindwa? Ina maana kuwa nguvu za CCM ni Kikwete?
Kama ugombea urais unaweza kuleta ugomvi wa kiwango hiki, nini maana ya demokrasia ndani ya cahama hiki kikongwe?

Demokrasia ndani ya vyama vingi vya siasa ikiwemo CCM ni ile ya kuswagwa kimakundi kama mikondoo taahira kuelekea machinjioni.
Mnaswagwa kwa utii huku mmejiinamia bila hata kutumia kwato na pembe zenu kujitetea.
Zaidi midomo yenu inazibwa kwa matonge ya wali na kushindwa kutoa mlio wa Meeeee! kabla ya kufaidi visu kwenye shingo zenu.
Hii ndo Demokrasia ya Viongozi Wazee wa chumvi nyingi ,Maharamia wa nusu karne wenye mvi nyingi vichwani mwao na nyuso za kukunjamana;kuteka na kumirirki kwa nguvu haki za wanachama wa chama chao, ili kujilundikia nguvu na uwezo wa kumsimika nduli mwenzao Ikulu na kudumisha ukoloni wa watu weusi kwa weusi wenzao.
 
Kuhusu credibility ya hii habari ilivyohojiwa, kwangu mimi nishamsikia Malecela akisema live kenye press conference kuhusu hili swala, juzi Ndejembi kasema, kwa hiyo sioni kwa nini hii habari iwe ya ajabu sana.Kwa kweli hata ukiiondoa hii ripoti ya Kubenea consensus miongoni mwa heavyweights wa CCM waliotajwa ni hiyo.Na ukimuondoa Shibuda hamna mwana CCM mwenye integrity na courage ya kulisema hili kama baya, hatujasikia hata mtu mmoja kusema angalau "Mimi namtaka Kikwete lakini sizuii demokrasia, anayetaka kugombea agombee" watu wanatishiwa kwamba wanapoteza hela zao in public, wanachoambiwa in private who knows?


Kwa kusema wazi wazi kwamba hawataki mtu kumpinga Kikwete, CCM pamoja na Kikwete wao wanaruhusu udikteta usiofuata na unaovunja katiba yao (CCM) na ya nchi, udikteta huu haujaruhusiwa popote na wala haujatajwa katika muongozo wowote wa chama.

Kikwete kama kweli ni kiongozi bora, anayejiamini na mpenda demokrasia aanzie kuonyesha hivyo kwenye chama chake mwenyewe kwa kusema kwa uwazi kabisa kwamba ni ruhusa kwa mwanachama mwenye sifa kutumia haki yake ya kikatiba (ya CCM na ya nchi) kugombea nafasi ya uongozi.

Ama sivyo hata Kikwete akichaguliwa tena ataonekana amechaguliwa kwa maguvu, sio kwa hiyari.
 
Last edited:
Back
Top Bottom