Mabilioni ya MCC: Tanzania 'kitanzini' March 28

Mabilioni ya MCC: Tanzania 'kitanzini' March 28

Suala ni kuonyesha mwelekeo na nia ya dhati ya kupambana na ufisadi! Hilo ndilo linalotakiwa! Ni Mdogo Mdogo hata huko escrow Magufuli atafika! Kwa sasa dunia inashuhudia taratibu mathubuti za kuanzisha mahakama ya mafisadi hapa Tanzania! Mafisadi papa waanze kutia MAJI!
Mdogo mdogo kivipi wewe? Watu wanafahamika waliohusika katika ufilisi wa rasilimali za nchi leo unasema mdogo mdogo.Kwanini waonewe watendaji na wanasiasa waachwe ili hali wote wanafahamika?
 
Hakuna aliyedharau fedha za MCC..Zimesaidia miradi mbalimbali na bado zinasaidia...

Wengi wanataka tujiongeze kwenye ukusanyaji wa mapato kupitia vyanzo vyetu vya ndani mfano kodi kupitia TRA..Bandari..Utalii n.k...

Tuondokane na utumwa wa kutegemea fedha za wafadhili zenye masharti ya hovyohovyo...Kama suala ni kupambana na uufisadi tupambane kwa dhamira na si tupambane na ufisadi kwa shinikizo la Wamarekani..Na hata hilo la Zanzibar si lazima walitumie kama kigezo cha sharti la kutoa msaada...

Ingawa bado ufisadi upo lakini kwa kiwango kikubwa serikali ya awamu ya 5 imeonesha ya kupambana nao..

Kuna nchi zinalazimishwa kupitisha sheria ya kubariki ushoga kwa sababu tu ya fedha za misaada kama hizo za MCC..Huu ni utumwa ambao hatutakiwi tuuendekeze..

Bahati nzuri Rais wetu ameonekana kutotetereka na hao wafadhili...Hajasafiri kwenda kuwapigia magoti kuomba watupe fedha za MCC ama kuomba msaada wowote..Zaidi anaonekana kuwa na ndoto ya kuongoza nchi inayojitegemea...Ndoto ambayo ni nzuri kwa mustakabali wa Taifa letu...

It can be done, play your part...
Mkuu @Bantalanda ndoto bila mipango thabiti ni kazi bure. Sawa ana ndoto hiyo lakini mipango iko wapi?
 
kwanini hii idea ya kutengeneza nyavu mnaipata baada ya kuambiwa hamtapewa tena samaki??
kwanini msianze kutengeneza hizo nyavu mapema??

Siyo idea mpya. Wengine tumeisema sana wakati wa mkwere. Muda mrefu Tanzania imekuwa ni laughing stock wakati tuna rasilimali nyingi na tulikuwa hatukusanyi kodi.

Tunahitaji kukusanya kodi. Tunahitaji kupanua wigo wa kodi. Tunahitaji kuondoa misamaha ya kodi ambayo ilikuwa chaka la rushwa.
 
Mkuu @Bantalanda ndoto bila mipango thabiti ni kazi bure. Sawa ana ndoto hiyo lakini mipango iko wapi?
Mipango inaendana na bajeti..Serikali ya Awamu ya tano bado haijaandaa bajeti..Bajeti ndio inaonesha mikakati ya kukusanya mapato na (ikiwezekana) kupunguza matumizi...

Pia Rais ameweza kuwashughulikia wabadhirifu wa fedha za umma na bado anaendelea kufanya hivyo..

Rais Magufuli pamoja na kutekeleza bajeti ya serikali ya awamu ya Nne bado ameweza kufanya jitihada za kuongeza kukusanya mapato na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima...

Ni matumaini yangu hata Bajeti inayoandaliwa na serikali yake kwa mara ya kwanza itajikita katika kuongeza mapato ya serikali na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima...

Tusubiri Bajeti ijayo itakuwaje...Na mipango ya muelekeo wa kiuchumi itakuwaje...
 
Mdogo mdogo kivipi wewe? Watu wanafahamika waliohusika katika ufilisi wa rasilimali za nchi leo unasema mdogo mdogo.Kwanini waonewe watendaji na wanasiasa waachwe ili hali wote wanafahamika?
Kama wewe unawafahamu basi subiri mahakama ya mafisadi itakapokamilika nenda ukawataje na peleka vielelezo, tutakushukuru sana!
 
Mkuu maendeleo ya taifa yanapimwa kwa kuomba misaada??

Kiongozi, kwa nini unakuwa myopic kiasi hiki? Nani kasema tunapima maendeleo kwa kuomba misaada. At what time unafanya evaluation? What do you need for development?

What is development? Unahitaji resources kwa ajli gani? Unazitoa wapi na unahitaji maendeleo ya nini na kasi aina gani?

Tafadhli kama hii agenda ya maendeleo siyo fani yako, unajifunza na siyo kuanika utupu wako hapa kwa kutaka kuchengesha mada tena kipumbavu!
 
Mkuu unalala mlango wazi na kutazamia neema itaingia mlangoni!!
MCC ni chombo chenye malengo ya maslahi na matakwa ya Marekani.
JPM amefanya vema kujikita katika kuondoa taswira ya kuonekana kujikomba kutekeleza matakwa yao.
Na pale wabunge wa Marekani walipokuja bila itifaki aliwatolea nje.
Ni vizuri kama nchi tukawa na moyo wa kujiamini na kujua kile tunachotaka na si kudhalilishwa kwa vimisaada vyenye masharti ya kuondoa heshima ya nchi.

Kimsingi mimi sitegemei MCC kama watabadili maslahi ya nchi yao ili tu walete misaada Tanzania.
Hiyo hela isahau!!!

Hebu tujiongeze kidogo: Hivi tukipewa fedha na kuwaunganishia watanzania umeme kwa asilimia 80% tunakuwa tumepata hasara gani sisi kama nchi?
 
Kiongozi, kwa nini unakuwa myopic kiasi hiki? Nani kasema tunapima maendeleo kwa kuomba misaada. At what time unafanya evaluation? What do you need for development?

What is development? Unahitaji resources kwa ajli gani? Unazitoa wapi na unahitaji maendeleo ya nini na kasi aina gani?

Tafadhli kama hii agenda ya maendeleo siyo fani yako, unajifunza na siyo kuanika utupu wako hapa kwa kutaka kuchengesha mada tena kipumbavu!
Mkuu nafikiri hatuelewani, ila nilichokikusudia si hicho ukifikiriacho Bali , ukweli wa nikiaminicho ,

Kama mleta mada alivyosema kuhusu MCC , Tanzania kuwa kikaangon ?

Pia sichengeshi mada Bali sitaki kuamini , mawazo yasiyo endelevu
 
Magufuli kukusanya pesa nyingi

Inaonekana hufurahii

Magufuli hata afanye nini, bila msaada wa nje kwa sasa, utekelezaji wa malengo yake utakuwa ni ndoto. Mtoto hazaliwi na kutembea.

Namwunga mkono Magufuli katika dhamira ya kujitegemea kama Taifa lakini hilo haliwezi kutokea kwa kulala na kuamka. Tuna utegemezi wa 40%. Namtegemea Magufuli akifanya vizuri, utegemezi upungue kwa sasa toka 40% to 30% mwaka huu. Na mpaka anamaliza miaka yake 5 tuwe na utegemezi wa 0%. Lakini kutegemea kuwa tunaweza kujitegemea ghafla toka kwenye utegemezi wa 40% mpaka 0%, hizo ni ndoto. Kwa kiburi tunaweza kujidanganya ila tujue hakuna miradi mikubwa itakayofanyika.

Tena jambo la muhimu ni kuwa dhamira hiyo ya kujitegemea itakwenda kiurahisi zaidi kwa kujenga maelewano na mataifa mengine na wala siyo kugombana nayo au kujifanya jeuri. Magufuli itabidi amuulize Mugabe. Zimbabwe nchi iliyokuwa na ustawi mzuri na maendeleo, leo hata kununua mkate hela unabeba kwenye mfuko wa Rambo. Nimeenda SA nimewaona walimu wa sekondari, clinical officers wa kutoka Zimbabwe wamekuwa wahudumu kwenye mahoteli. Wanaona aheri kuwa wahudumu kwenye hoteli SA kuliko kuwa walimu nchini Zimbabwe.

Ujeuri unaweza kufanyika lakini mateso yake huwa hayabebeki. Waliokuwepo wakati wa Mwalimu wanajua zaidi.
 
Mipango inaendana na bajeti..Serikali ya Awamu ya tano bado haijaandaa bajeti..Bajeti ndio inaonesha mikakati ya kukusanya mapato na (ikiwezekana) kupunguza matumizi...

Pia Rais ameweza kuwashughulikia wabadhirifu wa fedha za umma na bado anaendelea kufanya hivyo..

Rais Magufuli pamoja na kutekeleza bajeti ya serikali ya awamu ya Nne bado ameweza kufanya jitihada za kuongeza kukusanya mapato na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima...

Ni matumaini yangu hata Bajeti inayoandaliwa na serikali yake kwa mara ya kwanza itajikita katika kuongeza mapato ya serikali na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima...

Tusubiri Bajeti ijayo itakuwaje...Na mipango ya muelekeo wa kiuchumi itakuwaje...
Mkuu msingi wa Bajeti ni mpango ulioletwa bungeni na Dr Mpango. Ukweli mie sina matumaini kabisa. Nimesikitika sana, waweza wewe kuutafuta na kuusona. The same old stories
 
Jumatatu ya pasaka ya tarehe 28 mwezi huu,mkutano wa Bodi ya Wakurugenzi wa Millenium Challenge Corporation almaarufu kama MCC inakutana kuijadili Tanzania. Tanzania itajadiliwa kama ipewe au isipewe mabilioni ya MCC.

Nyaraka za shirika hilo zinaonesha kuwa Tanzania ilipewa masharti mawili ili iyapate mabilioni hayo. Kwanza,Tanzania ilitakiwa kupambana na rushwa pamoja na ufisadi. Pili,Tanzania ilitakiwa kuumaliza mgogoro wa kikatiba na kisiasa wa Zanzibar.

Tanzania itapata mabilioni ya MCC? Imetimiza masharti?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Pemba,Zanzibar)
Kwa ugoro huu wanao uendekeza kisa ccm ishike dola hapo hakuna cha kupata hiyo misaada ya mcc
 
Mzee tulia nani kakuambia tuna shida na pesa za MCC
Hayo ni maneno ya mkosaji na kwa taarifa yenu hakuna kupata huo msaada maana salaam tayari mmeshazipata baada ya jumuia za kimataifa kususia uchaguzi wenu wa ccm
 
Mkuu msingi wa Bajeti ni mpango ulioletwa bungeni na Dr Mpango. Ukweli mie sina matumaini kabisa. Nimesikitika sana, waweza wewe kuutafuta na kuusona. The same old stories
Bado nasema mkuu..Tusubiri bajeti ya kwanza ya serikali ya awamu ya 5...

Mpango uliowasilishwa bungeni na Dk. Mpango ulijadiliwa na maoni yalitolewa na Wabunge..Bado kuna uwezekano wa kuyafanyia kazi maoni/michango ile na serikali ikaja na bajeti nzuri tu yenye mipango/mikakati ya kuongeza mapato na kupunguza matumizi
 
Kweli kabisa hamna shida maana Magufuli kakusanya mapesa mengi na hivi sasa hakuna mwanafunzi anayekaa chini.. Hospitali zote zimejaa madawa na vifaa tiba hata wazazi wako si mafukara tena.
Na hakuna sehemu watu wana kula viwavi kama chakula mbadala
 
Hakuna aliyedharau fedha za MCC..Zimesaidia miradi mbalimbali na bado zinasaidia...

Wengi wanataka tujiongeze kwenye ukusanyaji wa mapato kupitia vyanzo vyetu vya ndani mfano kodi kupitia TRA..Bandari..Utalii n.k...

Tuondokane na utumwa wa kutegemea fedha za wafadhili zenye masharti ya hovyohovyo...Kama suala ni kupambana na uufisadi tupambane kwa dhamira na si tupambane na ufisadi kwa shinikizo la Wamarekani..Na hata hilo la Zanzibar si lazima walitumie kama kigezo cha sharti la kutoa msaada...

Ingawa bado ufisadi upo lakini kwa kiwango kikubwa serikali ya awamu ya 5 imeonesha ya kupambana nao..

Kuna nchi zinalazimishwa kupitisha sheria ya kubariki ushoga kwa sababu tu ya fedha za misaada kama hizo za MCC..Huu ni utumwa ambao hatutakiwi tuuendekeze..

Bahati nzuri Rais wetu ameonekana kutotetereka na hao wafadhili...Hajasafiri kwenda kuwapigia magoti kuomba watupe fedha za MCC ama kuomba msaada wowote..Zaidi anaonekana kuwa na ndoto ya kuongoza nchi inayojitegemea...Ndoto ambayo ni nzuri kwa mustakabali wa Taifa letu...

It can be done, play your part...
Well said, wanakera sana watu wanaopenda vya bure, alimradi wanajua kuomba kuliko kutumia vichwa vyao.
 
Hayo ni maneno ya mkosaji na kwa taarifa yenu hakuna kupata huo msaada maana salaam tayari mmeshazipata baada ya jumuia za kimataifa kususia uchaguzi wenu wa ccm
Jadilini kama taifa na sio kivyama
 
Back
Top Bottom