Mabilioni ya MCC: Tanzania 'kitanzini' March 28

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Jumatatu ya pasaka ya tarehe 28 mwezi huu,mkutano wa Bodi ya Wakurugenzi wa Millenium Challenge Corporation almaarufu kama MCC inakutana kuijadili Tanzania. Tanzania itajadiliwa kama ipewe au isipewe mabilioni ya MCC.

Nyaraka za shirika hilo zinaonesha kuwa Tanzania ilipewa masharti mawili ili iyapate mabilioni hayo. Kwanza,Tanzania ilitakiwa kupambana na rushwa pamoja na ufisadi. Pili,Tanzania ilitakiwa kuumaliza mgogoro wa kikatiba na kisiasa wa Zanzibar.

Tanzania itapata mabilioni ya MCC? Imetimiza masharti?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Pemba,Zanzibar)
 
Kweli kabisa hamna shida maana Magufuli kakusanya mapesa mengi na hivi sasa hakuna mwanafunzi anayekaa chini.. Hospitali zote zimejaa madawa na vifaa tiba hata wazazi wako si mafukara tena.
na ofisi za serikali kwa sasa OC ni za kumwaga.
 
Jumatatu ya pasaka ya tarehe 28 mwezi huu,mkutano wa Bodi ya Wakurugenzi wa Millenium Challenge Corporation almaarufu kama MCC inakutana kuijadili Tanzania. Tanzania itajadiliwa kama ipewe au isipewe mabilioni ya MCC.

Nyaraka za shirika hilo zinaonesha kuwa Tanzania ilipewa masharti mawili ili iyapate mabilioni hayo. Kwanza,Tanzania ilitakiwa kupambana na rushwa pamoja na ufisadi. Pili,Tanzania ilitakiwa kuumaliza mgogoro wa kikatiba na kisiasa wa Zanzibar.

Tanzania itapata mabilioni ya MCC? Imetimiza masharti?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Pemba,Zanzibar)
Mkuu unalala mlango wazi na kutazamia neema itaingia mlangoni!!
MCC ni chombo chenye malengo ya maslahi na matakwa ya Marekani.
JPM amefanya vema kujikita katika kuondoa taswira ya kuonekana kujikomba kutekeleza matakwa yao.
Na pale wabunge wa Marekani walipokuja bila itifaki aliwatolea nje.
Ni vizuri kama nchi tukawa na moyo wa kujiamini na kujua kile tunachotaka na si kudhalilishwa kwa vimisaada vyenye masharti ya kuondoa heshima ya nchi.

Kimsingi mimi sitegemei MCC kama watabadili maslahi ya nchi yao ili tu walete misaada Tanzania.
Hiyo hela isahau!!!
 
Kigezo muhimu ni cha kupambana na ufisadi ambacho Magufuli amekikidhi kwa asilimia 200!
Suala la Zanzibar si kivile maana hiyo ni nchi! na nasikia wamepiga kura Jana kwa utulivu wa hali ya juu!
Vinginevyo watupe zetu za bara!
 
Jumatatu ya pasaka ya tarehe 28 mwezi huu,mkutano wa Bodi ya Wakurugenzi wa Millenium Challenge Corporation almaarufu kama MCC inakutana kuijadili Tanzania. Tanzania itajadiliwa kama ipewe au isipewe mabilioni ya MCC.

Nyaraka za shirika hilo zinaonesha kuwa Tanzania ilipewa masharti mawili ili iyapate mabilioni hayo. Kwanza,Tanzania ilitakiwa kupambana na rushwa pamoja na ufisadi. Pili,Tanzania ilitakiwa kuumaliza mgogoro wa kikatiba na kisiasa wa Zanzibar.

Tanzania itapata mabilioni ya MCC? Imetimiza masharti?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Pemba,Zanzibar)

Kwa watanzania wengi tunaona maigizo tu
 
Hiyo hela wanatupa lkn tutailipa mara kumi yake kwamaana wamesikia ges nyingine imegundulika hapo lazima walushe chambo ndoo watuvue vizuri.
 
Back
Top Bottom