Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 879
- 4,109
January Makamba ameishi maisha mazuri toka utotoni si kwa sababu alikuwa bora kuliko wengine bali baba yake alitumia madaraka yake kumfanya aishi kwa rasilimali za nchi. Tukumbuke familia hii tofauti na kuwa watumishi wa umma wenye mshahara wa chini kabisa wamekuwa wakiishi maisha ya juu bila kujulikana fedha wanatoa wapi.
Kutokana na kuishi maisha ya ulimwengu wa kwanza amejikuta yeye ni waziri na kupitia nafasi hiyo waliomteua kila wanapofanya tathimini wanabaini siyo mtu sahihi kwenye uongozi hasa sekta nyeti.
Mfano gharama alizotumia kuandaa kongamano la TANESCO miezi michache iliyopita hakuna ambaye angeamini kwamba alitumia mabilioni kula na kunywa huku akiona kabisa mgao wa umeme unakuja.
Wao na Maharage wangeweza kufanya zaidi ila siyo kutumia mabilioni kwenye tamasha la viongozi waandamizi wa wizara na mashirika kwa kile kilichoitwa kujadili mafanikio na mikakati mipya.
Kwa kuwa hajawahi kujinunulia kitu chochote kwa jasho lake anaamini yeye amezaliwa kutumia rasilimali zetu huku wanyonge wakiendelea kinyonywa kwa mikodi lukuki.
Alikataa wananchi kuunganishiwa umeme wa REA kwa 27000 then yeye anatumia mabilioni kwenye vikao, ni ukatili tu usio na maana kuwafanya watu waishi gizani huku wewe ukigharamiwa kila kitu.
Jana waziri Mkuu amepiga kelele watumishi wa Kigoma kutumia milioni kumi na moja kwenda kwenye tamasha Tabora, je anafahamu mabilioni wanayotumia watendaji wa wizara na Idara za serikali?
Naamini zipo taasisi menejimenti inaondoka Dodoma kwenda DSM kufanya vikao vya menejimenti ili walipwe posho. Haya mambo yalikwemewa fedha za kukamilisha miradi ya umeme lazima zitapatikana.