Elections 2010 Mabere Marando kuibukia CHADEMA?

Marando kuingia CHADEMA ni Project ya Kikwete kuingia Ikulu bila ya matatizo!! I know something on Kikwete/Marando connection way back in 1998 when marando was fighting Mrema in NCCR mageuzi. Jihadharini Jamani na huyu Mtu.
 
Jamani hata mchawi akishajua wamemtambua mbinu zake hawezi tena kutembeza ulozi wala sumu. Marando watu wamemshtukia na kumsema. Viongozi wa Chadema wameshashtuliwa. Sidhani kama jamaa atakuwa na ubavu wa kuleta madudu yake: kwanza ataogopa kwa sababu wanamjua, pili wenzake watapigia hesabu miondoko yake. Cha maana Chadema wasilale usingizi wa pono.

Then do we need that type? The point ni aende tu hatumhitaji kwa sasa. Alikuwa wapi siku zote
 
Mabere Marando ajiunga na CHADEMA
Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Wakili wa kujitegemea, Mabere Marando akitangaza kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakati wa mkutano wake na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda

Acheni utani jamani Mabere siyo ajenti wa TISS na wala hajawahi kuwa ajenti wa TISS.. kama makumi ya watu ambao wamekuwa wakijipitisha kuwa ni maajenti wa TISS.. ni wale wanaoitwa huku "starving artists"
 
Tunaamini CHADEMA ni chama makini hivyo si rahisi kusambaratishwa na mtu mmoja kama baadhi ya watu wanavyodai lakini pia ni muhimu kuwa makini kwa wote wenye nia mbaya, ingawa huyu jamaa sidhani kama ana nia hiyo. Huwezi kukatalia watu uanachama katika wakati ambao wanahitajika zaidi ila unaweza kuchukua tahadhari ili mambo yasiharibike.
 
Acheni utani jamani Mabere siyo ajenti wa TISS na wala hajawahi kuwa ajenti wa TISS.. kama makumi ya watu ambao wamekuwa wakijipitisha kuwa ni maajenti wa TISS.. ni wale wanaoitwa huku "starving artists"

Mwanakijiji, wengi humu hawamjui Mabere Nyaucho Marando (MNM) wala historia ya NCCR - mageuzi ilivyoanza na vikwazo ilivyokumbana navyo kimojawapo kikiwa ni katika umbo la Augustino Lyatonga Mrema (ALM) akiwa Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani katika serikali ya Ali Hasan Mwinyi (AHM). MNM alikuwa moja wa waanzilishi wa mageuzi na mwenyekiti wa kwanza wa NCCR wakati ALM alikuwa ni kamanda wa vita dhidi ya mageuzi na alikuja kudandia meli baada ya vyama vingi kuanzishwa na yeye kugundua (au alitumwa ?) kuwa hana nafasi tena ndani ya CCM. Itawezekanaje wote hawa, MNM na ALM, wawe ndio walikivuruga NCCR - mageuzi wakati mmoja ni mwanzilishi na mwingine ni mdandiaji tu ? Kama kuna kitu anakijutia Mabere hadi leo ni kumkabidhi chama hilo pandikizi.

Tuliosimama jangwani tukinyeshewa mvua tukimsikiliza Mabere alipokuwa anamnadi ALM katika uchaguzi wa 1995, nakumbuka tulivyopigwa butwaa Mrema alipopewa kipaza sauti na badala ya kuifanyia NCCR kampeni na kuuza sera, alianza kulialia CCM ilivyomtosa. Kitu kimoja ninachokijua kwa uhakika kabisa ni kuwa Mabere ni asset kubwa kwa Chadema na hili viongozi wa Chadema kama Mbowe na Dr. Slaa wanalijua fika. Siyo tu wamewahi kufanya kazi naye, nina hakika amewahi kuwapa ushauri mbalimbali na si ajabu ameshiriki kwa namna fulani katika kupitishwa kwa jina la Dr. Slaa kugombea Uraisi. Mabere ni mwana mageuzi per se na ni mwiba kweli kweli kwa serikali ya Kikwete na anaijua vizuri sana - anayesema vinginevyo hamjui Mabere Nyaucho Marando.
 
I am not sure, ila ninajua kuwa wale waliokuwa usalama wa Taifa wakati wa Nyerere waliondolewa karibu wote wakati wa Mwinyi, baada ya Opiyo kuachishwa ukatibu mkuu wa Rais; Marando ni mmoja walioondolewa. Kutoka pale akaanzisha biashara yake ya unasheria na pia forum ya kudai mfumo wa vyama vingi. Mkutano wa kwanza wa wafuasi wa forum ile uliitwa "The National Convention for Construction and Reform (NCCR)," na ulifanyika kunako mwaka 1989 au 1990 hivi kabla hata vyama vingi havijaruhusiwa. Baada ya mkutano ule, wanachama wa ile forum (ambao wengi wao walikuwa ni wanasheria) waliendelea na harakati za kudai mfumo wa vyama vingi hadi walipofanikiwa na kugeuza forum yao kuwa chama cha siasa walichokiita NCCR-Mageuzi.

Siamini kuwa jamaa huyu bado anaitumikia serikali kwa vile nina marafiki na ndugu zangu waliokuwa usalama wa taifa enzi za Nyerere chini ya Opiyo, ambao leo hii ni walala hoi kama mimi na wewe. Hata Mrema siyo shushushu yule anajidai tu, kinachomsumbua Mrema ni ujinga na njaa. Mrema aliisambaratisha NCCR-Mageuzi kwa sababu chama kile kilikuwa na makosa katika muundo wake wa uongozi, makosa ambayo huviandama vyama karibu vyote vya Tanzania kikiwemo CCM chenyewe. Kwa mfano imekuwa ni vigumu sana kwa vyama vile kuwavua madaraka viongozi wao wa juu wakifanya makosa. Sasa Mrema alikuwa anafanya makosa ya kiuongozi lakini hawakuweza kumkabili. Siamini kuwa eti Mrema alikuwa ametumwa kuivuruga NCCR-Mageuzi, yeye alikuwa na uroho wa madaraka tu. Baada ya kufukuzwa (au kujitoa- kama yeye anavyodai) CCM, hakujua aende wapi na afanye nini, ila kutokana na popularity yake wakati ule, CHADEMA na NCCR walimkaribisha wakitegemea ange-boost popularity za vyama vyao. Mrema akawa na sharti moja, kuwa apewe uenyekiti wa chama na awe mgombea pekee wa urais kwa tiketi ya chama. CHADEMA haikukubaliana na sharti hilo la Mrema kwa vile walidai kuwa walikuwa na mfumo wao wa uongozi ambao ni lazima waufuate, na nadhani CHADEMA kilikuwa hakina haja ya kushiriki uchaguzi wa rais mwaka huo 1995 kwa vile walikuwa bado wanajijenga kwenye grassroots. NCCR-Mageuzi, ilikubaliana na sharti la Mrema ndipo Mabere akamwachia uenyekiti. Tafuta waliokuwa ma-strategist wa NCCR-Mageuzi wakati huo, Masumbuko Lamwai, Prince Bagenda, na Professor Baregu na wengineo watathibitisha kuwa kukubaliana kwao na sharti la Mrema ilikuwa ni strategic mistake kwani ingawa aliboost sana popularity ya NCCR-Mageuzi mwaka 1995 kiasi cha kuikaba koo sana CCM, vile vile ndiye alisababisha migogoro sana ya kiongozi ndani ya chama kile hadi kikafa. Marando hakuhusika kukiua chama ambacho alianzisha mwenyewe.

Lamwai aliondoka NCCR-Mageuzi kwa sababu mbili kubwa, ingawa baba yake naye (ambaye ni kada mkubwa wa CCM) alikuwa akimsukumiza sana Lamwai asiisumbue CCM. Sababu ya kwanza ni kuwa NCCR-Mageuzi haikuwa na mwelekeo tena baada ya kuvurugwa na Mrema, na pili ni kuwa serikali ya CCM ilikuwa imemkalia sana kooni kwenye biashara zake za sheria. Kuna wakati alihamishia ofisi zake Zanzibar; kwa hiyo alijisalimisha kusudi anusuru biashara zake.
 
Mag na Kichuguu mmesema vyema.. Mabere yawezekana sasa hatimaye anaweza kutulia.. .. lakini ningefurahi arudi kugombea Ubunge sijui ilikuwa ni Bunda kule alikowahi kugombea sikumbuki
 
Asante mkuu Kichuguu kwa mchango wako. Tatizo lingine ni kuwa Mrema hakuhamia NCCR peke yake, alihama na kundi la wapenzi ambao walimfuata kama Mrema na hawakuwa na mapenzi ya dhati kwa NCCR kama chama. Ni hawa wapenzi ambao kwa idadi yao kubwa waliweza kumlinda Mrema hata pale wana mageuzi wa kweli kweli walipoanza kumshtukia na kujaribu kumwondoa. Ni watu ambao walikuwa tayari kumlinda Mrema wao kwa hali yoyote ilee hata ikibidi kuiua chama na hivyo umaarufu wa NCCR wa miaka hiyo ulikuwa hasa ni wa bandia. Kama Mrema angeamua kurudi CCM, nina hakika hao wapenzi wake wangehama naye tena kama walivyofanya alipohamia TLP. Lekwama aliyeanzisha TLP naye alikuja kujuta na kujikuta akisema mengi baada ya kumkaribisha Lyatonga Augustino Mrema na kumpa uenyekiti. Mpaka leo hao wapenzi wake utawatambua tu kwa michango yao kila jina la Mrema linapojitokeza, wanaamini kabisa kuwa Mabere ndiye aliisambaratisha NCCR - yaani alianzisha NCCR ili baadaye akisambaratishe ! Sijui watasemaje na Mrema naye leo akijitokeza na kutangaza kujiunga na Chadema !

Mag na Kichuguu mmesema vyema.. Mabere yawezekana sasa hatimaye anaweza kutulia.. .. lakini ningefurahi arudi kugombea Ubunge sijui ilikuwa ni Bunda kule alikowahi kugombea sikumbuki

Aligombea jimbo la Rorya.
 
karibu sana Mabere marando tunahitaji mchango wako......wewe ni mpigania wa kweli na mtu mwenye msimamo,unaloliamini huwa unalisimamia haswa
 
Wanabodi wengi tu humu wanajiandikia vitu kwa kufuata mkumbo, hakuna lolote wanalolijua. Eti Chadema wamkatae Marando...kwa sababu gani hakuna anayeweka hoja zozote zenye akili!!!

Mabere Marando ni Mwana Mageuzi halisi. Amekuwa akipigania vyama vingi tangu mwishoni mwa 1980's.

Watanzania wanashindwa kuelewa kuwa katika chama au jumuiya yoyote ni lazima kuwe na timu inayoweza kuendesha chama katika mapinduzi mbalimbali bila ya kuangalia maslahi ya mtu binafsi. NCCR walikosea hapo, walipoangalia maslahi ya Mrema badala ya chama mambo yote yakaenda kombo...hakukuwa na Timu tena kulikuwa na watu wachache wanao angalia maslahi yao.

Naamini kabisa Marando ni asset kubwa sana kwa Chadema na upinzani Tanzania hasa katika kulipigania jimbo la Rorya lilirudi upinzani. Mabere angejitosa tu kugombea tena Rorya, alishinda 1995 tena kwa kura nyingi tu...itakuwa leo. Mbunge wa sasa wa Rorya Prof Sarungi ameshajichokea.

Chadema ni chama makini na kina muelekea mzuri sana wa kuwa chama imara mbadala.

Jambo moja tu linaloonyesha wana utaratibu mzuri wa kuongoza Chama chao. Hebu jiulizeni ni nani ndani ya Chadema aliyewahi kugombea uraisi zaidi ya mara moja?
 
Mag na Kichuguu mmesema vyema.. Mabere yawezekana sasa hatimaye anaweza kutulia.. .. lakini ningefurahi arudi kugombea Ubunge sijui ilikuwa ni Bunda kule alikowahi kugombea sikumbuki

Alikuwa mbunge wa jimbo la Rorya kwa kipindi cha miaka 5 kuanzia 1995 mpaka 2000. Tangu mwaka 2000 linashikiliwa na Prof Sarungi, na amechukua tena fomu mwaka huu. Lakini nina hakika Mabere akiamua kula sahani moja na Prof Sarungi anaweza kushinda. Pamoja na hayo, alihitaji kuanza mapema kuandaa mikakati kama alikuwa na nia ya kugombea Ubunge mwaka huu.
 
siasa mchezo hatari saana, jamani ni kwa sababu ya milioni mia moja? Cku zote walikuwa wapi hawa? Au ndo kuhaha kwenyewe?
 
Mag na Kichuguu mmesema vyema.. Mabere yawezekana sasa hatimaye anaweza kutulia.. .. lakini ningefurahi arudi kugombea Ubunge sijui ilikuwa ni Bunda kule alikowahi kugombea sikumbuki

Ninahisi kuwa kuhamia kwake CHADEMA, ni njia ya kutaka kwenda tena kugombea ubunge kule kwao Rorya, ambako ninajua akienda atashinda kwa urahisi sana; Profesa Sarungi hawezi kufurukuta kabisa mbele ya Marando.
 
Namkumbuka Marando alipotuhamasisha kuandamana kwenda ikulu toka viwanja vya jangwani, nakumbuka tukiwa mstari wa mbele huku tumeshikana mikono tulipofika maeneo ya DIT iliyokuwa Dar Tech FFU waliokuwa wamejipanga mbele yetu barabara ya Bibi Titi wakatoa kitambaa chekundu. Nakumbuka vizuri baada ya mabomu kupigwa tulivyoruka lile geti la Dar Tech na Marando tukajikuta tumo ndani ya uzio wa Dar Tech.

Namkumbuka tena Marando kule Laskazone Tanga alivyoamlisha taa zizimwe na meza ya Mwenyekiti wakati huo Mrema Ikabinuliwa ili uchaguzi uvurugike. Nikiunganisha na sakata lake la kuwania Ubunge wa EAC alivyopigiwa kampeni la nguvu na CCM, mmhuu sijui labda mimi ndiye simwelewi vizuri huyu jamaa.

Lakini all in all sina tatizo na Marando kujiunga Chadema kwa vile naelewa ndani ya Chadema kuna watu makini watakuwa wameangalia pros and cons. Namjua Marando ni mwanamageuzi halisi aliyepotea, atulie aonekane anakijenga chama kama alivyotulia Lwakatare, vinginevyo kama atakuja na lake atajulikana muda si mrefu, Chadema huwa haichelewi kumwonyesha mtu mlango.
 
Chama kilichojengwa katika misingi imara ya kidemokrasia ni vigumu sana kukisambaratisha.Sijui CHADEMA imejengwa kwa misingi gani.
Mtakumbuka kuwa vugu vugu la vyama vingi lilianzishwa na hawa akina marando. Kosa kubwa walilofanya ni kutaka kuingia madarakani kabla ya kujiimarisha vema. mrema alipohamia NCCR alikwenda na kundi lake kama msemaji mmoja alivyonena hapo juu. Kundi hili likadhani kuwa linamamlaka ya kutwaa chama kwasababu ya mrema. Chama kikawa Mrema na si NCCR. Akina marando wakazidiwa nguvu.
Tunakumbuka kuwa mrema aliandaliwa mambo mazuri katika mdahalo[sera],lakini kwa vile alijua kuwa ni maarufu eti ana mtaji wa watu akaongea upupu wa kukamata dhahabu.
Mrema akawa dictator akitaka fulani awe kiongozi na iwe hivyo,chama kikafa kwa ubinafsi wa mrema ambao hauna shaka kwa mtu mwenye akili timamu. Hebu fikiri,eti ni mwenyekiti wa TLP halafu anasema CCM haikamatiki siku ya pili yake anakwenda kusimamia uchaguzi wa chama chake kwa mgombea urais!!1. Huyu anataka uenyekiti aendeshe maisha lakini hana lolote lile la maana.
Marando alinitia shaka alipopitishwa na wabunge wa CCM kugombea ubunge EA.Baada ya hapo hatukumsikia tena. Lakini hii haiondoi ukweli kuwa ni mtu makini. Kujiunga na Chadema sioni tatizo, anakaribishwa sana. Jambo la muhimu ni Chadema kuelewa kuwa yeye ni kama mwanachama mwingine yoyote na kuwepo kwake ni kuimarisha chama na si kama ngazi. Asipewe ''special treatment'' lakini pia asinyimwe haki zake.
Chadema iongozwe kwa ''principles'' na si kwa matakwa.
Kuna watu wamejitoa sana Chadema,hawa wabaki na heshima zao na si kwasababu eti fulani kaja basi kesho yake ni makamu au katibu mkuu.
Kama chama kitafuata misingi imara ya sheria na taratibu mtu mmoja hawezi kukisambaratisha.
Leo hii watu wangesikia Warioba, Sitta au Msuya wamejiunga na Chadema wangefurahi kwa kisingizio cha upinzani halisi utatoka CCM, vipi Marando awe tofauti!!!
Kama hatutakubali mawazo mbadala na changamoto zinazotokana na demokrasia tutakuwa tume via kimawazo. Kama watu wataogopa dhana ya chama kusambaratishwa na mtu mmoja basi ni wazi kuwa chama hicho hakipo tayari kupewa mamlaka.
Leo hii tumesimama imara kama taifa si kwasababu ya umaarufu wa Mwl Nyerere,bali misingi ya utaifa aliyoijenga. Vivyo hivyo Chadema kiwe ni chama chenye misingi ya kisheria na taratibu na umaarufu wake uwe kwa chama na si kwa mtu au kikundi cha watu, hakuna wa kukisambaratisha.

Ahsanteni
 
Ubunge wake kule EALA sikuona tatizo kabisa kwa vile kilikuwa na kiti cha upande wa upinzani, na kwa vyovyote wabunge wa CCM hawakuwa na jinsi; ni lazima wangemkubali mpinzani mmoja - wakaamua kukamkubali Marando. Ninadhani kuwa sababu mojawapo ya kumkubali marando haraka haraka vile ilikuwa ni namna ya kuudhalilisha uongozi wa upinzani (hasa CUF) ambao walikuwa wanataka kuteua mtu wao hasa kwa vile CUF ndicho chama pekee cha upinzani ambacho kina wabunge wengi. Inawezekana pia walikuwa wakitaka kumnyamazisha asije kuwarudi katika kesi mbalimbali za uchaguzi.
 
Back
Top Bottom