Na mkiendekeza propaganda kama hizi hamtakaa muendelee hata siku moja - kila siku mtakuwa hamuaminiani na hamtaweza kuwa na mshikamano kama taifa
Kwa chama kinachokuwa kushindana na dola ni vyema kuwa na wasiwasi. Lakini hata kama Marando huyu mnayemfahamu akiondoka Chadema bado kama dhamira ya kuisambaratisha ipo itakuwepo (Na mimi naamini ipo), lakini mfumo wa Usalama huwa hauchezi bahatisha kwani wanaweza kumtumia mtu mpya kabisa na hata wale ambao waliopo na wanaoaminika kwenu Chadema.
Tofauti na mnavyodhani mie ninaemwona msambaratishaji wa Chadema ni Zitto na wala siyo Marando. Lakini kwa kuwa hofu hii ni kubwa naomba nitoe ushauri huu.
Kazi ya Usalama ni ukusanyaji wa Taarifa na uzuiaji wa Taarifa za uvunjaji wa siro za serikali kuvuja ambapo katika hili wakitekeleza kwa mfumo wan chi yetu ni lazima wakilinde chama tawala. Na kwa vile kazi yao ya mwisho ni kuendesha mapambano ya kisiri basi mapambano ya kusambaratisha vyama yapo na Chadema kwa sasa inalengwa kusambaratishwa.
Kuepuka njia hiyo kwa sasa Chadema inapaswa kupitia idara yake ya ulinzi na usalama kuwa na timu ya wataalamu ambao watafanya kazi hizi;
1. a).Ukusanyaji wa taarifa za kijasusi dhidi ya CCM.
2. b).Kuzuia mipango ya uvujishaji siri za Chadema (counter espionage).
3. c).Kuendesha Mapambano ya kisirisiri (covert operations).
Ki msingi kama chama hakiwezi kujiendesha kwa kufanya haya, kwa mfumo wa CCM na serikali itakuwa ni kazi bure kufanikiwa kushinda kwa vile utapokea wanachama mamluki na kuwaona ndiyo wanaofaa wakati hawafai na huku ukiwatimuwa wale wanaofaa ukidhani hawafai.
Nina amani Chadema wanaweza kuwa na kitengo hiki, nah ii ndiyo sababu hata E-mail za Zitto ziliweza kupatikana wakati wa vuguvugu la kuwania uongozi ndani ya Chama na hata sababu za Kafulila na wenzake kutimuliwa.
La Marando:
Kwa kawaida usalama wa Taifa akishajiingiza katika siasa anapaswa kuandika barua ya kukoma majukumu yake ya kazi na ila inakuwa mara mbili.
1. Kuacha kazi
2. Kusimama kazi kwa muda wa kipindi Fulani
Anaweza kuandika kuacha kazi, hii ikiwa na maana kuwa analipwa haki zake na mafao yanayostaili kwama mtumishi yeyote, lakini katika njia hii inaweza kuwandaliwa mpango maalum wa mtumishi kuacha kazi na akatangazwa kuwa katimuliwa au kaacha kazi lakini akawa anatumika kwa kazi maalum nab ado akawa mtumishi wa Idara.
Lakini pia anaweza kuchukua likizo ya muda maalum hata kama ni miaka 5 ua zaidi na akeleza kuwa bababu anaingia katika siasa na kule akawa anapwe Assignment maalum.
E.G: Kufuatilia mwenendo wa vyama na mipango yao kwa maana ya kubaini iwapo katika mikakati yao wanao mpango wa kupindua nchi ama kuua viongozi. Mfano katika kundi hili wapo Wabunge kama Mdhihiri, Ernest Mabina n,k ambao baada ya kuukosa ubunge na kwa umri wao wanarudi kupewa kazi tena Idarani.
Lakini wakati wakitoka hao wanapishana na wengine kama Bw. Masele (DSO) wa Geita ambaye anachukua majukumu ya Mabina kwa kuingia bungeni kama Mbunge wa Mbogwe. Kai yao ni moja kufuatilia nyendo za wabunge.
Kumbuka hao wanafanya kazi kwa siri kujua nini kinapangwa na wanajadili vipi serikali na nani wana mikakati mzizito zaidi dhidi ya serikali lakini wamejivisha miamvuli ya Ubunge na kumbe ni Usalama wa taifa na wameandika ofisini kwao kuacha kazi.
Sasa inawezekana Marando akawa aneacha kazi kweli, lakini akawa pia anaendelea na kazi hiyo,
dawa ya Chadema ni kuwa na kikosi chake kama nilivyoeleza hapo juu, kwani hiyo inaweza kusaidia kupunguza MASHAKA kwa wanacham KIRUSI lakini pia kusaidia KUPATA TAARIFA ZA WAPINZANI WAO na kupanga mambo kwa kuangalia mwelekoe wa CCM huku nao wakipanga mambo kuibomoa CCM.