Du..Maswali mazito kwelikweli haya!..pia nina wasiwasi baadhi yake yanamhitaji yeye mwenyewe ayajibu kwa usahihi, vinginevyo utalishwa sumu hapa!Marando amesema mwenyewe kuwa alikuwa mwajiliwa wa usalama wa taifa, sasa ni vipi aliacha kazi hiyo? Alifukuzwa? Kwa nini alifukuzwa? Alistaafu? Na alikuwa na wadhifa gani wakati anatoka huko? Je, si bado mmoja wao?
Marando amesema mwenyewe kuwa alikuwa mwajiliwa wa usalama wa taifa, sasa ni vipi aliacha kazi hiyo? Alifukuzwa? Kwa nini alifukuzwa? Alistaafu? Na alikuwa na wadhifa gani wakati anatoka huko? Je, si bado mmoja wao?
UWT watu wanastafuu na kuruhusiwa kufanya shughuri nyingine. Mwiko kwake ni kutoa taarifa za ndani kwa wakati ule alipokuwa anafanya kazi. Kuna wabunge wengi ndani ya CCM walikuwa UWT, mfano Dr Kitine tena aliwahi kuwa bosi pale, na alikuwa mbunge wakati wa Mkapa, sasa kuna kosa ngani marando kuwa Chadema?
Mabere Nyaucho Marando alikuwa mwajiriwa wa UWT tangu enzi za Mwl Nyerere.Mabere Marando alikuwa ni miongoni mwa watu wa mwanzo kudai mfumo wa vyama vingi kabla ya mfumo huo kuruhusiwa rasmi.
Marando alikuwa mwenyekiti wa mwanzo wa NCCR Mageuzi kabla hajampisha A L Mrema mwaka 1994.Marando alibakia na nafasi ya katibu mkuu wa NCCR Mageuzi na mbunge wa Rorya na baadae mbunge wa Afrika mashariki.Marando alishiki kwa kiasi kikubwa kuisambaratisha NCCR Mageuzi kwa kuhakikisha mkutano mkuu wa NCCR Mageuzi unashindwa kufanyika,alishikiri kuandaa vijana kuanzisha vurugu ndani ya mkutano hali iliyosababisha Mwenyekiti wake Mzee wa Kiraracha kujificha chini ya meza.Marando alizawadiwa ubunge wa EAC na CCM kama malipo ya kuisambaratisha NCCR Mageuzi.
Mabere Nyaucho Marando mwanasheria na kachero wa juu alishiriki vita vya kumwangusha idd Amin wa Uganda.Alitumia taaluma yake ya ukachero kuingia ndani ya nchi ya Uganda kabla majeshi yetu yaliyokuwa yakiongozwa na kamanda David Musuguri hayajatia mguu Kampala.
Taaluma ya ukachero si mbaya kama baadhi ya watu wanavyodhani inategemea inavyotumiwa na
Nchi zilizoendelea na zinazoinukia kiuchumi kitengo cha ukachero pamoja na mambo ya usalama kinatumiwa kuangalia maslahi ya kiuchumi zaidi.Dunia ya leo uchumi mzuri na wenye nguvu ni usalama tosha kwa taifa lolote makini.UWT haina habari ya uchumi wa nchi ndiyo maana baadhi ya maofisa wake walishiriki bila hofu yoyote kwenye ufisadi uliofanyika BOT.UWT haioni ubaya madini yetu ya Tanzanite yakiuzwa kama malighafi India.UWT haina hofu raia wa nchi za kigeni wakiajiriwa kwenye makampuni mabali mbali nafasi ambazo zingekuwa za raia wa Tanzania.UWT imeshindwa kuishauri serekali kwamba ingetakiwa kuwa mbia wa migodi yote ya madini ya dhahabu.UWT imeshikilia kazi moja kubwa ya kulinda serekali ya CCM isiondoshwe madarakani.
Mkuu nimeikubali hiyo post yako marando bado haeleweki... ila DOKTA SLAA ni mtu makini pamoja na chama chake hivyo kama marando ni mamluki atatimuliwa kama ilivo kua kwa KAFULILA
Mkuu nimeikubali hiyo post yako marando bado haeleweki... ila DOKTA SLAA ni mtu makini pamoja na chama chake hivyo kama marando ni mamluki atatimuliwa kama ilivo kua kwa KAFULILA
yeye kama raia mwingine wowote ana uhuru wa kushiriki shuguli mbalimbali za kijamii kwa maslahi ya tanzania , kushiriki shuguli za kisiasa ni kwa interests za taifa pia hata huko kwenye vyama kuna watu wa usalama wa kutoa taarifa na kuwashauri viongozi maswala mbalimbali kwahiyo msiogope sana - usalama wa taifa wako kwa maslahi yetu ni wananchi wa kawaida kama nyie sema utafauti uko kwenye utendaji wa kazi ni sawa na dereva wa basi na konda wake wote wana majukumu kutokana na mkataba wao wa kazi
Theories!
Haufahamu ulichoandika hapo juu (red/bold)... Inawezekena umesoma Ukurasa wa kwanza wa "Mission Statement ya TISS"!
sasa hapo utasema juu ya zitto tena kungombe uongozi na bosi wake. kama hajui hilo liko wazi. kwakuwa myenyekiti wake yupo bungeni ndie anaongoza bunge -upinzani