Mabegi wanayobeba watoto wa shule siku hizi yatawadumaza

Jamani watt wanateseka mnoo
Kuna siku mwanang akanambia mamy muulize Mwalim nibebe madaftari kiasi naumia bag zito
Karoho kaliniuma nkampiga kiswahili akaondoka
 
Wanachoka sana...

Hiyo yote ni kwa sababu hizo shule hazina (locker's) kwa ajili wa wanafunzi kufungia/Kuhifadhi vitu vyao ambavyo hawavitumii kwa kipindi hicho...

Na pia waalimu ambao hawazingatii ratiba za vipindi, inapelekea wanafunzi kila siku kubeba kila kitu, kwa sababu hawana uhakika...

cc: mahondaw
 
Yaani ingefaa kuwe na special lockers wanafunzi wawe wanahifadhia madaftari yao na vifaa vyao huko kama shule za ulaya...

Bongo unakuta mtoto mdogo kabeba begi lina uzito wa haja
Shule za ulaya wao kila mwanafunzi ana locker yake mchezo umeisha. Ni kweli wangeanzisha system hizo ingesaidia. Una kufuli yako basi .hiyo kazi kila siku unaenda na mzigo unarudi na mzigo
 
Shule za ulaya wao kila mwanafunzi ana locker yake mchezo umeisha. Ni kweli wangeanzisha system hizo ingesaidia. Una kufuli yako basi .hiyo kazi kila siku unaenda na mzigo unarudi na mzigo
ILA TENA KWA KUWA NI BONGO NDIO UNAVYOONA MKUU
 
Haya mabegi sijui hata huwa wanabeba nini unakuta katoto kadogo kana peck kama ya komando kwene maonesho ya siku ya uhuru, imekua ni kero kwene mwendokasi asubuhi na jioni unakuta watoto wanapata shida na ma peck yao
 
Hizi English medium shida sana watoto wanabeba mzigo mpaka unapata hofu Vitabu madaftrari matatu matatu kama sio school bus MOI pangejaaa watoto
 
Nyie mnaosema shule ziwe na locker hampo serious kbs...vyoo vyenyewe ni mtihani kujengwa hizo lockers si ndio anasa kbs.

Cha muhimu ni kufuata timetable tu lkn hata hivyo bado mzigo utakuwa umepungua kiasi maana madaftari ukijumlisha na vitabu.
 
St. Kayumba bila shaka....tuliteseka sana aisee hata ss, mm watt wangu sitaki wasome hizo shule kabisa
St kayumba gani hiyo wanabebeshwa hivo!!
Sijawahi kuona st kayumba anabeba begi lenye uzito wa kilo kadhaa..

Wanachobeba wao sanasana ni mifagio, maji kwenye vidumu japo vimepungua sikuizi hawabebi naona mashule mengi yana visima na mabomba.

Enzi zangu nasoma hukooo mitaa fulani ya nzasa tulikuwa tunabeba hadi mbolea, kila mtu na bustani yake na lazima istawi.

Hii mizigo ni hizi shule wanazodai ni bora walimu wake ni wahindi, wazungu pamoja na masista ndio wanabeba sana mizigo msizisingizie shule zetu za white&blue bwana o_O
 
Haya mabegi sijui hata huwa wanabeba nini unakuta katoto kadogo kana peck kama ya komando kwene maonesho ya siku ya uhuru, imekua ni kero kwene mwendokasi asubuhi na jioni unakuta watoto wanapata shida na ma peck yao
 
Me nilikuwa nakunja daftari naweka mfuko wa nyuma!! Class siingii kila siku,halafu mlango wng ulikuwa dirisha la nyuma,dawati moja masela kibao!! Ticha akija kutembeza stiki me nsharuka dirisha kitambo muda wa mapumziko ukiisha mpaka naingia darasan nshaingia la tatu b kumsalimia juma,ntaingia c kumcheck mwanang hamiss tukitoka clas kuwinda ndege
 
Kayumba hawana mizigo ya kipuuzi daftari tu chache wengine wanakunjia mfuko wa Nyuma
Huyo unayesema ww nichimbo huyo daftari moja masomo yote anaandikia English akitoka mwalimu huo ukurasa uliyoandikiwa unachanwa linaandikiwa science
 
Back
Top Bottom