Mabegi wanayobeba watoto wa shule siku hizi yatawadumaza

Salamu, Uniq.

Maamuzi sahihi yanatanguliwa na Elimu sahihi. Right decision is proceed by right knowledge.

Uhuru wa kuchagua hutanguliwa na utashi. Na utashi hutanguliwa na elimu juu ya suala hilo.

Lazima tusanisi, tudadisi, tusaili na kadhalika. Lazima tuwe REST-LESS..

Unadhani ni sahihi mwanafunzi kufundishwa, kusoma masomo zaidi ya 14 kwa siku?. Nadhani tungeanzia hapa.

Karibu..
Kwangu mimi naona sio sahihi kabisa. Maana hakuna mtu anaeweza kupoke vitu vipya zaidi ya 4 kwa siku.
Mimi ningetamani kuona mwanafunzi wa shule ya msingi asome vipindi sio zaidi ya sita kwa siku. Then apate muda wa kucheza na kutuliza akili na kufanya mazoezi na kujisomea alicho fundishwa siku hiyo.
Elimu yetu ya Tanzania mtoto anapewa vitu vikubwa sana kuliko umri wake.
 
St. Kayumba bila shaka....tuliteseka sana aisee hata ss, mm watt wangu sitaki wasome hizo shule kabisa
Mkuu hizi shule za private za english medium kwa kubebesha watoto wetu lundo la vitabu na daftari ndio wenyewe.
Mimi nimeomba timetable kwa ajili ya mtoto wangu grade 3 lakini yenyewe haijasaidia, unakuta kwa siku masomo sita hadi saba. Vitabu 6 + Counter books 6 (Quire 3) + Maji ya kunywa ni mzigo mzito almost 7kg.

Hii sio shule moja, karibu shule 3 tofauti nimeona hilo tatizo.
 
Me nilikuwa nakunja daftari naweka mfuko wa nyuma!! Class siingii kila siku,halafu mlango wng ulikuwa dirisha la nyuma,dawati moja masela kibao!! Ticha akija kutembeza stiki me nsharuka dirisha kitambo muda wa mapumziko ukiisha mpaka naingia darasan nshaingia la tatu b kumsalimia juma,ntaingia c kumcheck mwanang hamiss tukitoka clas kuwinda ndege
 
Hahaha hakuna chakula cha shule anabeba jiko na mtungi wa gas, sufuria, na makorokoro ya kupika, kwani kunakusoma, walimu bado wanahakikiwa vyeti.
 
Elimu yetu ya Tanzania mtoto anapewa vitu vikubwa sana kuliko umri wake.
Tukiondoa uvivu tutajifunza mambo mengi sana. Kwa kusoma.

Tunampatia mtoto/mtu elimu kulingana na umri wake au darasa analosoma/anachokisoma?.

Unafahamu hisoria ya Elimu (Epistemology, reasoning, questioning) kuanzia Mashariki ya mbali, Uropa na Asia?.

Naomba walau mifano kadhaa, Jedwali la umri-elimu apaswayo kupewa mtoto. Tafwadhali.

Nb; Jibu likisadifu swali, shaka huondoka- Shaaban Robert.

Elimu ni Nuru.
 
Mkuu hizi shule za private za english medium kwa kubebesha watoto wetu lundo la vitabu na daftari ndio wenyewe.
Double standards.

Hivi unafahamu kuwa uliyemkopi anazungumzia shule zisizo za private?.

Hili suala ni abstract. Nadhani pilipili tuso-ila isituwashe. Zungumza na mwanao kama ni adha kwake uchukue hatua za kitaaluma. Kame siyo, msihi asome na uache kumuingilia.
 
Double standards.

Hivi unafahamu kuwa uliyemkopi anazungumzia shule zisizo za private?.

Hili suala ni abstract. Nadhani pilipili tuso-ila isituwashe. Zungumza na mwanao kama ni adha kwake uchukue hatua za kitaaluma. Kame siyo, msihi asome na uache kumuingilia.
Yeye nimemuelewa sana mkuu, nahisi wewe ndio hukunielewa lengo langu kumjibu vile yule mdau.
Mimi nilikuwa namkatalia sio hizo St. Kayumba pekee bali hata hizi Private schools za English Medium nako kuna tatizo kama hilo.

Nashindwa kupata mantiki ya kusema "Double standards" ukihusianisha na ushuhuda wangu juu ya hilo tatizo.
Kwangu hilo limekuwa tatizo kubwa sana, nimewahi jaribu kulilalamikia ktk vikao vya shule na wazazi.
Nikaungwa mkono na wazazi wengi tu tena shule tatu tofauti unakutana na same problem.

Au wewe ni kati ya hao waalimu au waandaaji wa hizo time table au syllubus zenye kusababisha tatizo hilo? Hadi sasa sijajua tatizo syllubus au time table. Labda utusaidie kwa uzoefu wako na tujue nani wa kumpelekea maoni au malalamiko yetu.

Kama tatizo ni mtaala basi shule zitafute utaratibu wa kununua vitabu kwa ajili ya kutumia wanafunzi wakiwa shuleni navyo ni mali ya shule, na wazazi wanunue vitabu kama hivyo ambavyo vitabaki nyumbani hivyo mtoto atakuwa anabeba daftari tu. hapo mzigo utapungua karibu 48% ya mzigo wa sasa.
Kama wewe ni mwalimu basi jaribu kupokea maoni kutoka kwa "third party". Afya ya mtoto ni muhimu pia.
 
Jamani mie shule walikuwa wananiita ''Sir Isaac Newton'' nilikuwa na kadaftari kamoja kameandikwa masomo yote, mie ilikuwa kupita kwenye magroup ya discussion nawasovia maswali yaliyowashinda basi.
 
Ila haya mabeg ya benten ni shida unalinunua jumamosi jumanne zipu mbovu sijui tfda waanze kuyakagua manake tbs kazi zimewazidi
 
Mwanabodi, Titicomb .

Umeandika kwa weledi na uzoefu. Hongera kwa uumini bora wa uwajibikaji. Pia samahani kwa sintofahamu hapo juu. Hukumkatalia, ulizungumza as one-self. Ulizungumzia Private school's na si Gov'nt school's.

Leave about that. Mimi si lolote Tanzania wala katika mfumo wa Elimu. Siyo Mwalimu, Afisa ugavi, Mwa-ndaaji na kadhalika. Ni suala la ku-negotiate, kaeni chini mtatue.

Sina basis yeyote zaidi ya kuandika Taharihi kwa maelfu humu Jamii Forums. Sina la kushauri zaidi.
 
Back
Top Bottom