Jane Lowassa
JF-Expert Member
- May 10, 2016
- 5,009
- 9,206
Mmiliki wa Sauli buses siyo mbungeYaap
Mmiliki wa Sauli buses siyo mbungeYaap
Hio ni sehemu ya bonde kuu la ufa la afrika mashariki.Hvi likichomoka jabali hko juu itakuwaje aisee
Looo mkuu nilipita hapo usingizi wote ulikata nikaana kukaa kama abiri wa kwenye boda boda.Hio ni sehemu ya bonde kuu la ufa la afrika mashariki.
Mawe huwa yanaporomoka na kuziba hiyo njia hasa msimu wa mvua.
Hata hivyo huo mlima ulichongwa na kampuni moja ya ujenzi ili barabara ikae vizuri kama inavyoonekana sasa.
Kabla haijachongwa hiyo njia ilikuwa mbaya sana na gari ilitumia muda mrefu kupanda au kushuka huo mlima.
Watuondolee hivyo vi speed governor vinatumalizia ladha.
Watuache tu Mbeya tuwe tunafika saa saba









Ongeza na Dar to Bukobadar to kigoma au mwanza and musoma tuiteje?
KILIMANJARO expHiyo nyuma gari gani
Pooooooti??unakumbusha mbali kikoloNa makasokela/ makatapera
Chai hiimiaka ya nyuma Mwaza-Mbeya kabla ya vingamuzi vya spidi havijafungwa kwenye mabasi kuna dereva aliendesha spidi mpaka basi zima wakatapika kasoro mimi tu na dereva.


Lilikuwa linapita Iyunga saa 8:20 ilikuwa ni roho mkononiUmenikumbusha enzi za miaka ya 1998 hadi 2000 kulikuwa na basi la masia, lilikuwa inafika Tunduma saa 9:00 mchana kutoka Dar... Chini ya dereva mahiri Deo Kapelege, aisee ilikuwa balaa
Dereva wa masia alishakufa lkn cio kwa ajari...ligi ya mabasi ya mbeya dar ni balaa mkuuLilikuwa linapita Iyunga saa 8:20 ilikuwa ni roho mkononi
Watuondolee hivyo vi speed governor vinatumalizia ladha.
Watuache tu Mbeya tuwe tunafika saa saba
Hekima sa tisa jioni siku tuko ubungo mataa pale licha ya foleni,na ilitoka tunduma nilidandia uyole.yule dereva kimbaumbau hivi ye anapiga fegi tu na gia hewani balaa sikupata hata lepe la usingizi njia nzima machine inapepea tu pale mafinga ndo aliuaKama ukiwa muhenga kama mie miaka hiyo tulikua tunakujabkusalimia huko mbeya usiniambie eti mabasi sasa hivi yanakimbia miaka 9+ to 20 kulikua na wamba saa 10 umefika (KISWELE.MTEMA BEACH.M-SLEEPING COACH.TAWAQAL.HEKIMA)nk.ila tawaqal kulikua na dereva anaitwa kabulu mwenye kujua zaidi aje atujuze saul al-saedy zinapita saa 12 jioni mlandizi useme zinakimbia huo ni utani
Ni kweli kabisa, miaka ya 99 bus kama la Embakassy lilikuwa linaingia stand Mnazi mmoja saa 12:45 jioni kutoka Mbeya, na hilo ndio lilionekana kuwa slow kuliko yote!
Huko mbali 2008 tu hapo natoka songea nakuja dar, kibaha tumeingia saa 12 iv jua linawaka mpaka 2.30 iv nipo, so kwa sasa safari hazina raha masaa kibao barabaraniNi kweli kabisa, miaka ya 99 bus kama la Embakassy lilikuwa linaingia stand Mnazi mmoja saa 12:45 jioni kutoka Mbeya, na hilo ndio lilionekana kuwa slow kuliko yote!
Bujibuji umenikumbusha hii nikiwa home SIMIKE nikisikia makelele tu kona ya META najua TAWAQAL hiyo imetoka DAR.
Sijui haya magari yaliundwa vipi.Mwaka 98 nilipanda TAWAQUAL ya Kaburu tulitoka Ubungo- Majisaa 12.15 asubuhi. Ndani ya basi kulikuwa na mzee mmoja anahubiri neno alipandia Morogoro, ngoma wakati inakata kona za IYOVU mzee aliacha kuhubiri akaenda kumchungulia dereva, alirudi kimya na INJILI ikaishia pale. Saa 5 hivi tuko Iringa pale Ipogoro. TRAFIKI akatuhoji safari ikoje wahuni wakajibu "poa". Kumbuka hapo kuna basi iliingia mtoni mazima huko Tanga.
Tuliingia Mbeya saa 9 hivi. Nikaulizwa umekuja na JENEZA (Mwamahapa- M Sleeping Coach)? Nikawajibu hapana, hiyo ngoma ilitua nusu saa kabla yetu.