Mabasi ya abiria yagongana Tabora

Consigliere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
12,037
24,595
Ajari ya mabasi mawili ya abiria imetokea leo asubuhi katika daraja la Igombe mkoani Tabora, ajari hiyo imeyahusisha mabasi ya Muro na Sia Bus.
Mashuhuda waliopo eneo la Tukio wanasema kuwa mabasi hayo yaligongana wakati wakupita katika daraja hilo ambalo lina uwezo kupitisha gari moja kwa wakati. Dereva wa bsi la Muro aliokolewa baada ya watu kufanikiwa kumnasua kwe usukani wa gari aliokuwa amenaswa.
Habari kuhusiana na waathirika watukio hilo na wameathirika kwa kiasi gani nitawaeletea kwa kadiri nitakavyoendelea kupata taarifa toka eneo la tukio.

Wakati huo huo

Mtu mmoja mwanaume amefariki dunia usiku wa jana katika hospitali ya mkoa Kitete, mtu huyo alifariki dunia baada ya kukatwa mapanga kwa kufumaniwa na mke wa mtu. Taarifa zinasema mtu huyo alifumaniwa na mume wa mke huyo baada ya kurudi nyumbani kwa dharula, wakati mke akijua kuwa yupo safarini.
Jamaa akiwa hajui hili wala lile kuhusiana na mchezo wa mke wake ndipo alistaajabu kumkuta mke wake akiwa na mtu mwingine chumbani mwake.
 
Back
Top Bottom