Mabango katika Maandamano Kumpinga JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabango katika Maandamano Kumpinga JK

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kaniki1974, May 19, 2009.

 1. Kaniki1974

  Kaniki1974 JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 352
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tumeusema sana Utawala wa Kikwete. Hauna dalili yoyote ya kubadilika. Sasa ni time for action. Hatutaki kusubiri 2010. Wengi wanasupport maandamano yetu Kuupinga Utawala wa Kikwete kama ilivyojitokeza ktk thread iliyopita. 'Watanzania si mabwege tena'.

  Sasa tunakusanya mawazo ya mabango tutakayobeba. Please, toeni maneno ya kuandika katika mabango hayo. Maneno yawe machache yenye ujumbe usiojificha na mkali kwa mfano: 'Viongozi Mnatusababishia Umaskini'

  Mawazo yenu pse.
   
 2. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Tukifaulu kuandaa maandamano, maneno ya kwenye mabango yatakuja tu! Mbona yako mengi tu? Tufanikishe maandamano kwanza maana hayo hata bila kubeba bango lolote wahusika watapata salamu zetu!!
   
 3. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2009
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Mimi nimekuwa nikingojea hilo la JF kuvuka kutoka kuwa kukwaa la mawazo na porojo tu na kuwa jukwaa la vitendo. Jambo muhimu la kujadili ni jinsi JF inavyoweza kuwa pro-active kupitia hatua dhahiri kama maandamano, makongamano, kutoa elimu ya uraia, nk. Hii maana yake ni kwamba sura za wanaJF (siyo mawazo tu) zitatambulika kwa jamii pamoja na kwa mahasimu wa jukwaa hili. Hiyo ndiyo changamoto. Tufanye nini?
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,427
  Likes Received: 22,349
  Trophy Points: 280
  kwani handsome boy kisha rudi toka usa??
  tutaandamana tu wala usijali, sisi tunabeba mabango wao wanabeba marungu na mabomu ya machozi, na gari lao litabeba maji ya kuwasha.
  watatuumiza lakini ujumbe utakuwa umefika mahala pake
   
 5. Mateso

  Mateso JF-Expert Member

  #5
  May 20, 2009
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 244
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  ccm 2010 basi katafuteni kazi nyingine hambebeki
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Wee Mateso, ni kivipi watatoka sasa?

  Tupe japo mkakati binafsi wa jinsi ya kufanya katika kuunganisha nguvu, kuanzia kwako, kwa jirani yako na kwa Danganyika Nzima.

  Mimi nina watu kama 200 hapa Ofisini, na wote wanachanachana makadi ya sisiemu muda huu!
  Si ni hatua tosha? Kwa hapa Arusha Mjini, na kwa njia hii, huyu BUBU Mrema hatopona!
   
 7. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #7
  May 20, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  Hawezi kurudi mapema hivi, bado anaongea na google jinsi ya kwanasa 'Ze utamu wa kujitafuna'! Si umesikia kuwa kaitembelea google?
   
 8. Comrade Mpayukaji

  Comrade Mpayukaji Senior Member

  #8
  May 20, 2009
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jamani kuna nchi ya kibabe kama china? Mbona wale wanfunzi walikubali kupigwa risasi za moto pale Tianmen Square na leo tunaona mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kijamii katika jamii ya china leo. Elimu bora, maisha bora na idadi ya matajiri wa kichina imeongezeka. Sio demokrasia ucharwa tunayopigiwa kelele kwamba ipo Tanzania. Jamani vyama vingi sio demokraisia. Mijitu inakaa wizarani inaiingia mikataba ya kuuza nchi na wanachi walio wengi hasa vijijini hawafaidiki na utajiri Mungu aliotujalia. Wenzetu Niger Delta wanaendeleza mapambano dhidi ya watawala wanaochukua utajiri wao na kuwaachia umaskini. ni wangapi kati yetu wako tayari kufa ili kuikomboa nchi yetu dhidi ya makabaila hawa wa kitanzania walio vaa ngozi ya kondoo? Tuaache porojo kama ni noma na iwe noma. Tunataka mapinduzi ya kiuchumi na kijamii sio siasa uchwara ambapo kila mtu anakuja kutujaribia theory zake ambazo hazijazaa matunda. Mapinduzi ya kilimo yatakuja vipi kama mfumo wetu wa elimu ni utitiri wa shule ambazo ni bora elimu?
   
  Last edited: May 20, 2009
 9. J

  Jafar JF-Expert Member

  #9
  May 20, 2009
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Bango lingine "Tanganyika itafufuka hata ikipita miongo kadhaa"

  ..sincerely I always dream that one unkown day Tanganyika will rejuvenate. Sio kama natoka nje ya mada bali ninafafanua bango langu hapo juu.
   
 10. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #10
  May 20, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Jamani naunga mkono hoja ya maandamano kuupinga utawala huu wa ombaomba.Ndugu zangu unaweza ukajitolea maisha kwa ajili ya vizazi vijavyo kama Babu zetu walivyofanya kuuondoa ukoloni wa Mzungu,sasa nasi tujitolee kuuondoa ukoloni huu wa Mtu mweusi Mtanzania.Wageni wanachuma rasilimali zetu tunaangalia tuu.Ardhi inauzwa kwa wageni kama KIGAMBONI,MBUGA ZA WANYAMA na MIGODI tunakaa kimya haiwezekani tuamke jamani.
   
 11. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #11
  May 20, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ni kweli kabisa Tanzania inahitaji mapinduzi ya kimaadili kama yaliyotokea CHINA.Kama mafisadi yangehukumiwa kunyongwa ufisadi ungekoma kabisa Tanzania.
   
 12. J

  Jafar JF-Expert Member

  #12
  May 20, 2009
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hawawezi kuhukumiwa kunyongwa kwa kuwa atakae hukumu au atakayesaini wanyongwe wote ni mafisadi.
   
 13. J

  Jafar JF-Expert Member

  #13
  May 20, 2009
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hakimu na JK wote ni mafisadi - kwa hiyo hawawezi kuhukumiwa kunyongwa
   
 14. Ngaramu

  Ngaramu JF-Expert Member

  #14
  May 20, 2009
  Joined: May 7, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Bango lingine "TANZANIA BILA UFISADI INAWEZEKANA - MWANANCHI CHUKUA HATUA"

  na "UFISADI NI UUAJI"
   
Loading...