"Mabala wa mabalaa" Ni Nani?

avatar18566_7.gif
BADO UNA SWALI Katavi?
Sina swali nimemfahamu sasa. Asante
 
Kumbe ndiye aliyeandika Mabala the farmer!!
Pia ni mwandishi wa makala katika gazeti la Mwananchi Jumapili...??

Pia ni malenga hodari mno.
Marehemu Prof. Mwaikusa alikuwa mwanafunzi wake.

Anapatikana FaceBook kwa jina la Richard Mabala
 
Yeah..Anaitwa Richard Mabala...ni Muingereza nafikiri,alioa Mtanzania na hivyo akaamua kubadilisha jina lake la Ukoo na kuchukua hilo la Mabala...Ni Mtaalamu wa Literature,ameandika articles nyingi lakini ni maarufu sana kwa vitabu vyake ambavyo vimetumika sana kipindi fulani cha 90's kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza katika somo la kiingereza,vinaitwa Mabala the farmer na Hawa the Bus driver....
nilianza kusoma article za richard siku nyingi akiwa na gazeti kama sikosei la mipasho ,hili gazeti lilifungiwa kutokana na mipasho yake ni mwandishi mahiri mzungu nikawa nimepoteza machoni hadi nilipo muona kwenye gazeti la mwananchi ni mwandishi nguli pamoja na henri mdimu walikuwa pamoja kwenye gazeti moja hivi.suala la uraia wake namuelewa kama ni mtanzania mwenzetu .binafsi napenda makala zake na jinsi anavyowasilisha ujumbe kwa kipenzi chake hidaya wa uzitoni ,ingawaje mara nyingine hidaya huwa anampa misukosuko kwa umahiri kabsa hidaya hutulia .na kumuandalia mzee wa uzitoni juice
 
Anajulikana kama Mr. Squint katika makala za kiingereza hasa katika The Citizen.
 
...Hili sina uhakika nalo nitaomba mwenye uhakika nalo atujuze. Mwaka huu mwanzoni ama mwaka jana mwishoni nilipata taarifa za kusikitisha kuwa alikuwa amefiwa na Mkewe. Mwenye uhakika, tafadhali...
 
Richard Mabala, aliyeandika kitabu cha Mabala the farmer, ailkuwa ni mwalimu wa secondary Mzumbe kama sikosei na baadaye akaacha, na kuwahi kuajiriwa UDSM, sikumbuki vema alikuwa idara gani na sasa nafikiri anafanya kazi na mashirika mbalimbali ya kiuana harakati. Ni mzungu aliyezaliwa na kukulia bongo (Tabora kama sikosei - mnyamwezi wa kizungu), ana uraia wa bongo na anayeipenda Tanzania kuliko nchi ya babake.
Hakuzaliwa bongo,alizaliwa uingereza ila sasa ni mtanzania baada ya kubadiki uraia wake

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Richard Mabala, aliyeandika kitabu cha Mabala the farmer, ailkuwa ni mwalimu wa secondary Mzumbe kama sikosei na baadaye akaacha, na kuwahi kuajiriwa UDSM, sikumbuki vema alikuwa idara gani na sasa nafikiri anafanya kazi na mashirika mbalimbali ya kiuana harakati. Ni mzungu aliyezaliwa na kukulia bongo (Tabora kama sikosei - mnyamwezi wa kizungu), ana uraia wa bongo na anayeipenda Tanzania kuliko nchi ya babake.
Umenena vyema mkuu.
 
Back
Top Bottom