Mabadiliko yajayo ya Ma-RC namuona Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam kama RC mpya

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
1,502
4,408
Suala la soko la Karume kuungua moto ikiwa ni muda mfupi tu baada ya soko la kariakoo kuungua moto linaweza kuja na taswira mpya ya baadhi ya watendaji kuwajibishwa.

Moja ya watendaji ambao naona wakiwajibishwa ni RC wa DSM ikiwa ni njia ya kuponya majeraha ya maumivu kwa machinga.

Naona pia wenyeviti wengi wa mikoa wakiwa wakuu wa mikoa mbalimbali
 
Labda kama hayopo nao. Ila dalili za wazi ninkuwa huyu kawekwa na wakubwa kusafisha uchafu wa maskini waliokuwa wamefurika kila kona ya Dar.

Huyu hafukuzwi kamwe. Na hata hao unaowapigia chapuo hawatakalia hiyo nafasi. Wa Dodoma au mkoa wowote usio na madhara anaweza kuondolewa. Siyo wa Dar.
 
Hilo haliwezekani.
Pengine hamkuona uozo uliokithiri wa kuyafanya masoko kuwa magulio ya mateja,mama lishe, chinga na uozo mwingi.
Sasa ukimuweka kada wa CCM ndio unaingiza siasa kwenye uendeshsji wa miji, kosa kubwa alilofanya Magufuli.
Kuna mkuu wa mkoa sio kada wa CCM? Yaani kabisa unataka kusema Amos Makalla sio kada?
 
Alikuwa na mkopo Bank alikimbia kulip deni alijifanya anakwenda kulima mpunga mbeya na akafeli mwisho wa siku walitaka kupiga mnada mashine zake za mpunga na Lodge mvomero aliomba sana washikaji zake wakaqa wanamchamgia kulipa bi mkubwa akapelekewa jina ili amnusuru kijna ndio akapewa u RC WA DSM NDIO PONA PONA YAKE kajaza mashavu na kalimati
 
Kwa kweli Rc Makala mi nampongeza sana tena namupmba aongeze kasi atusafishie mji kabla maji hayajapoa. Dsm tunahitaji wahuni wote waliojenga kuzidi mawe ya viwanja vyao iwe ni fremu, maduka, pub, ukuta, baa wabomolewe na magreda ya jiji. Service road zimeluwa ndogo sababu ya wahuni kuzidisha mawe.

Eneo kama Kawe linatakiwa kubomolewa nyumba zilizozidi barabarani mapema kabisa ili wasahau na uchaguzi ukija wachague tena CCM. Sinza na maeneo mengine yote
 
Makala is the best amefanya vyema sana, jiji limependeza sema Kariakoo ndo bado watendaji wa chini wanamhujumu ila jamaa ni mfuatiliaji mzuri sana. Jiji la Dar na majijini yaliharibiwa sana na ufanyaji holela wa bihashara.
 
Kuna mkuu wa mkoa sio kada wa CCM? Yaani kabisa unataka kusema Amos Makalla sio kada?

Enzi ya Mkwere, Amos Makalla Ingawa alikuwa hana utaalam wa hesabu ndio alikuwa mweka hazina wa CCM!! Kwahiyo wana siri kubwa sana na Vasco Dagama.
 

Yaani mkuu wa mkoa ana husika vipi na moto! Watu hawajazoea walitaka mkuu wa mkoa ambaye ni legelege huyu jamaa ni jembe hatolewi
 
Si ajabu ukakuta we ni swahiba wake wa karibu unamuanika mshikaji wako jamvini
 
Wahuni nchi hii kila siku ni ubaya tu.

Kila mtakayeletewa ni mbaya tu.

Kila litakalopendekezwa ni kupinga tu.

Ni Tanzania
pekee ambapo kila mwenye simu janja kupitia mitandaoni.
Basi ujuaji wa sheria,uhasibu,wizi,siasa yaani kila mtu ni mshauri.

Serikali ikikaa inawasikiliza team ROHO MBAYA.
Mambo yatakuwa ni umbeya na visasi tupu.

Mfano huyu mleta Topic tayari yeye anawaza kupanguliwe safu ya RC'c.

Hivi unazijua gharama zinazoendana na hizo pangua pangua?

Kumekucha nenda katafute riziki acha ujinga mitandaoni.

Dar es salaam ni jiji la waswahili kiasili na ukiwaendekeza hakuna kazi itafanyika bali itakuwa majungu repeatedly!

Makalla endelea na kazi,jiji walau sasa linakuwa na muonekano kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…