Mabadiliko ya vifurushi: Ninadhani tunamuonea Dkt. Ndugulile. Je, wabunge kazi yao ni ipi?

RECEIPT

JF-Expert Member
Nov 6, 2013
284
198
SIONI SABABABU YA KUMLAUMU MHE DKT FAUSITE NDUNGULILE

Na Elius Ndabila

0768239284


Baada ya mabadiliko ya vifurushi vya mitandao jana kubadilika Watanzania wengi walilalamika kuwa vifurushi hivyo havijaja kuwasaidia bali kuwaumiza. Pamoja na maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Viongozi wa TCRA, bado wananchi walionyesha kuwa ni vifurushi vya kikandamizaji na kuomba msaada kwa Mhe Rais awasaidie. Usiku serikali kupitia msemaji wa TCRA walitangaza kuendelea na vifurushi vya zamani na kustisha hivi vipya huku msistizo ukiwa ni kwa vifulishi vya internate tu.

Lakini Wananchi wengi wameonyeshwa kukasirishwa na utendaji kazi wa Waziri wa Mawasiliano Dkt Ndungulile kuwa ndiye alitufikisha hapo. Wanasema kwa nini Ndungulile alipeleka mabadiliko ya sheria hizo kandamizi?

Ili sheria itungwe lazima ipitie kwenye muswada. Muswada ni mchakato unaopitia hatua nyingi kabla haujatungwa kuwa sheria. Na process za muswada wa serikali zinafahamika.

Ielewe kuwa muswada wa sheria wa serikali huwasilishwa bungeni kwa takwa la kisheria chi ya kanuni ya 80(2) na 81(1) ambapo Waziri au Mwanasheria huwasilisha.

Wazo la kuandaa muswada wa serikali linaweza kutolewa na Waziri husika au maelekezo ya Baraza la Mawaziri ikiwa ni mkakati wa kutekeleza sera au jambo Fulani ambayo ipo katika mipango ya saerikali kupitia Wizara. Baada ya jambo kuibuliwa, Wizara husika kupitia kwa Wanasheria na Wataalamu wengine hufanya utafiti kuhusu jambo linalohitaji kutungiwa sheria kwa lengo la kuhakikisha kwamba mambo yanayohitajika kutekelezwa, yanazingatiwa ktk Sheria inayokusudiwa kutungwa. Baada yah apo kuna Waraka wa Baraza la Mawaziri, Kibali cha Baraza la Mawaziri, Muswada kutangaza kwenye gazeti la serikali na baadaye hupelekwa bungeni kwa hatua mbalimbali ikiwepo kuuchambua na kuutungia sheria.

Kutokana na sheria za nchi yetu, jambo lolote likisha ungwa na wengi kwenye Baraza la Mawaziri linakuwa ni jambo la wote hata kama kule ndani ulilipinga lakini ukitoka nje lazima uliuunge mkono. Hivyo sina uhakika kama sheria iliyozuiwa jana na serikali kama ilipitia process hizi, kama ilipitia basi hili si la Dkt NDUNGULILE Bali tuwaulize Wabunge wetu ambao ndio level yetu kwa maana ya uwakilishi walipokuwa wanatunga hii sheria walitazama merits zake? Je, walijadili au walikubuwa busy kujenga kwanza hoja za Rais kuongezewa miaka?

Binafsi ninadhani ni haki na wajibu kuwalalamikia Wabunge wetu ambao ndio walipaswa kuwa watu wa kwanza kuhoji kabla ya Wananchi wanyonge hawajapiga kelele. Nini kiliwafanya Wabunge wakae kimya? Au wao waliona ni sahihi? Lakini swali la mwisho, kwenye utetezi wa baadhi ya maofisa wanasema bando za mwanzo wananchi walikuwa wanaumizwa, sasa kama watu wanataka zile ambazo nyie mnadhani waliumizwa si muwaache kwa kuwa hizi mpya wao wanaona ndio maumivu?
 
Hapa lawama ni kwa Jiwe na Ndungulile,wabunge wengi ni vilaza walibebwa na Jiwe kwenda mule ndani.

MTU kama Msukuma,Kijababji hata maana ya neno MB hawajui-si utawalaumu bure.
Kwakweli. Enzi za mwendazake bunge lilikuwa halifanyi chochote ila ndiyooooo
 
Mdogo wangu Ndabila kama ulisikia zile tambo zake namna atakavyoboresha vifurushi ndiyo maana analaumiwa, kule kijijini kwako Ibaba nani ataweza kumudu hizi bundles?
 
Ina maana walivyosema wanaboresha hawakujaribu kwa kikokotoo chao inakuwaje? Huu ni usumbufu kwa mitandao na kwa wananchi. Waziri ajiuzulu
 
Katika hiko kilinge kilichokaa kikao hakuna ambaye TSh.3,000 ni tatizo kwake sababu kuna wanaoipata mara 100 ya hio pesa kwa siku kama posho ya tako!

Inaskitisha sana hatma ya maskini kuamuliwa na tajiri. Walau wangevaa viatu vyetu hata kwa week 1 tu wangeona moto wake. Waporwe kadi zote za benki, waende maofisini au bungeni kwa daladala no boda au bajaji na balance ya mkononi iwe elf 15 per day. Kula, kunywa, vocha na nauli kisha wakitoka hapo ndio wakakae kwenye kikao cha maamuzi yao uone kama wangeafikiana kuweka bei ya 1GB kwa sh.3000!
 
Ndugulile alitoa mpya.....

"USICOMMENT, USILIKE............."

Tukipata maNdungulile wengi , basi Taifa litakuwa la mabubu na viziwi.
 
Wabunge wengi sana wamepewa bure au kwa hisani hizo nafasi unategemea wanaanzaje kufungua midomo yao dhidi ya mfadhili wao?
 
Mdogo wangu Ndabila kama ulisikia zile tambo zake namna atakavyoboresha vifurushi ndiyo maana analaumiwa, kule kijijini kwako Ibaba nani ataweza kumudu hizi bundles?
MATAGA wanasema hii ndiyo ilikuwa ni dawa ya wakosoaji wa ccm
 
MATAGA wanasema hii ndiyo ilikuwa ni dawa ya wakosoaji wa ccm
Ni mjinga pekee anayeweza kusupport hilo.....kuna watu wanafanya online business kuendesha maisha yao.....faida za mitandao nikubwa kuliko huu ujinga unaowazwa.....kama unakosea utakosolewa tu
 
Back
Top Bottom