Mabadiliko ya Sheria yanaweza kusaidia kupunguza kutokuelewa baina ya watendaji

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
1,502
4,408
Kwako Mhe.Rais wa JMT,

Nakusalimu kwa jina la JMT...kazi iendelee.

Awali ya yote ninapenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutujalia afya njema na tumeweza kufika muda na wakati kwa neema zake Mwenyezi Mungu.

Pia, nichukue nafasi hii kukupongeza kwa utendaji kazi uliotukuka na juhudi mbalimbali serikali inazotumia na maboresho mbalimbali yanayofanyika katika kuhakikisha maendeleo yanapatikana.

Mhe.Rais ,ninakupongeza kwa kuhakikisha kazi zinafanyika bila kuwepo kwa migongano ya "kimaslahi" , ya" kiutendaji" na "kimaono" baina ya watendaji na umebainisha wazi migogoro inaweza kuwa ni chanzo Cha kazi kutofanyika.

Mhe.Rais, suala hili la migongano baina ya watendaji serikali, nimejaribu kulitafakari kwa undani na nimegundua ni mfumo wa kuwapata hivyo ninashauri yawepo mabadiliko ya kisheria.

Jambo la kwanza Mhe.Rais, Jambo hili linasabaishwa na "superiority and inferiority complex". Siku zote panapokuwa na wateule wawili ambao mamlaka zao za nidhamu na uwajibikaji ikawa ni moja na ikatokea mkuu kimadaraka Kati ya hao ana Elimu ndogo kuliko aliye chini yake ni lazima kuwe na migogoro.

Nimefanya uchambuzi wa kina na nimeona hili. Kwa mfano waziri akiwa na Elimu ndogo kuliko katibu mkuu wake atajihisi "inferior" huku katibu mkuu atajiona "superior" kuliko waziri wake kwa sababu mamlaka yao ni moja.

Pia, ikitokea waziri ameteuliwa kwenye eneo ambalo sio fani yake na katibu mkuu wake ni mbobezi kwenye fani hiyo ,maana yake katibu mkuu anaweza kumdharau waziri na migongano ikatokea.

Mhe. Rais ,kwa hakika hizo "scenario" mbili ndio chanzo Cha migogoro baina ya watendaji wako na ndio maana naona mabadiliko ya Sheria ndio yatakuwa ni suluhisho.

Kwanza, mabadiliko ya Sheria yawepo ili kifungu kisemacho waziri lazima awe mbunge kiondolewe. Wabunge wanachaguliwa kwa mapenzi ya Wananchi bila kujali Elimu zao na kifungu kinachosema waziri lazima awe mbunge kinatulazimisha kumteua waziri miongoni mwa wabunge wenye sifa ndogo kuliko makatibu wakuu hivyo migogoro kutokea.

Mawaziri wakiteuliwa nje ya wabunge inakuwa ni rahisi kupata mawaziri waliobobea kwenye fani husika.

Kwa heshima na taadhima naomba kuwasilisha Mhe. Rais
 
Pia kuna mida sisi wenyewe tunalazimisha mambo. Unakuta wizara ina manaibu waziri 2. Au makatibu wizara 2 wote wanafanya kitu kile kile reason behind ni kua wizara ni kubwa inaitaji attention

Wizara ikishakua kubwa maana yake opportunity ya wizi ni mkubwa. Na hapo ndio wanapoanza kugombana. Kila mtu anawai deal kabla ya mwenzake
 
Pia kuna mida sisi wenyewe tunalazimisha mambo. Unakuta wizara ina manaibu waziri 2. Au makatibu wizara 2 wote wanafanya kitu kile kile reason behind ni kua wizara ni kubwa inaitaji attention

Wizara ikishakua kubwa maana yake opportunity ya wizi ni mkubwa. Na hapo ndio wanapoanza kugombana. Kila mtu anawai deal kabla ya mwenzake
Upo sahihi haya ni majangili tupu
 
Back
Top Bottom