Mabadiliko ya Profesa Kabudi kwenye sheria ya madini yanalitesa Taifa. Nini kifanyike?

Inakuwa Kama umerogwa, Nani kakuambia migodi nchi hii iko mitatu tu? Kwa taarifa yako hela inayovunwa na serikali kupitia soko la dhahabu la Geita Ni zaidi ya mapato ya hiyo migodi unayoitaja,
Migodi ya dhahabu Tanzania ipo mingapi? Na nje ya hiyo migodi ya makampuni niliyoyataja, hiyo mingine inazalisha kiasi gani? Kwa maana ya migodi hasa, mgodi nilioacha kuutaja ni wa Shanta Mine, uliopo Chunya, ambao ni wa kati. Iliyobakia, mingi ni workings, na watu wanaoprocess tailings.

Jiulize tailings zinatoka wapi? Workings nyingi zinafanyika kwenye maeneo yaliyofanyiwa utafiti na nani? Nje ya hawa niliowataja, wengine wote, hakuna mzalishaji anayetoa hata 10% ya hao wazalishaji wakubwa.

Nakuuliza sustainability ya production lakini unatoa majibu ya kejeli. Basi, endelea kuamini kuwa makampuni yote yanaweza kuacha uzalishaji na bado uzalishaji na mauzo ya dhahabu utaendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka.
 
Uzalishaji umeongezeka toka ounces ngapi mpaka ounces ngapi kwa mwaka? Hatuzungumzi kwa kubahatisha bali kwa uelewa.

Kinachofanyika sasa ni sawa na mkulima aliyeacha kulima lakini wakati anaacha kulima, ndani ya nyumba ana magunia mawili ya unga. Lakini kwa vile ugali unaendelea kuonekana mezani, wewe unafurahia kuwa kuacha kulima hakuna madhara mbona tangu aache kulima ugali bado upo.

Tunakueleza kuwa Bulyanhulu, uchimbaji umesimama tangu mwakajuzi. Buzwagi uchimbaji umesimama tangu mwakajana. Buzwagi kinachofanyika kwa sasa ni kuprocess ore iliyochimbwa kabla ya kuacha uchimbaji. Bulyanhulu wanaprocess tailings (kwa lugha ya wachimbaji wadogo ni kuwa wanaprocess marudio). Kwa Barrick, uchimbaji unaoendelea kufanyika ni North Mara tu, ambako nako LoM imepunguzwa baada ya kupandisha cutoff grade ili kuendana na ongezeko la gharama za uzalishaji.

Katika hali hiyo, kuna sustainability ya mapato ya sasa?

Soma hapa, 7% mrahaba kwa Barrick/Accacia sio kitu, hizi data utazipata ukienda BOT au wizara ya Madini huko, pengine mnazo ila hamtaki ili kupindisha ukweli.
 
Nakuunga mkono.Sasa hivi tunavyojadili jambo hili makusanyo ya maduhuli kutokana na Madini yameongezeka kwa zaidi ya 100%.
Mabadiliko ya sheria yamesaidia kuongeza mapato hayo na manufaa mengine mengi kutokana na biashara za Madini.

Umeandika maelezo mengi lakini umeshindwa kuweka takwimu kabla ya mabadiliko ya sharia, sekta ya madini ilikuwa inaliingizia taifa kiasi gani cha fedha za kigeni na mara baada ya mabadiliko hayo ya sharia ya madini taifa limeingiza kias gani cha fedha.
 
Nimejifunza mengi hapa. Hii mada fikirishi.

Ila kama kumbukumbu zangu zipo vizuri, nakumbuka mabadiliko ya sheria za madini yalikuja mara tu baada ya msomi wa juu kabisa tena aliyebobea katika sekta ya madini , Prof. Nehemiah Ososro na timu yake nzima kuandaa ripoti mbili za kitaalam ambazo zilieleza wazi kabisa na kwa undani jinsi tunavyopoteza mapato na namna gani tunavyoibiwa na tulivyoibiwa kama taifa na makumpuni makubwa ya uchimbaji madini.

Sasa unavyoelekeza lawama zote kwa Kabudi bila hata ya kumtaja msomi mwenzako Prof. Nehemiah Ososro na timu yake inanifanya nibaki nashangaa maana maamuzi yote yaliyofuata yaliyokana na maoni na ushauri wa ripoti zile mbili za Prof. Osoro.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tena kwa miaka mingi tumekuwa tukilalamika kuwa report na tafiti za wasomi zinapuuzwa/hazifanyiwi kazi Kaja kiongizi kazitekeleza nzima nzima JPM hajasoma sheria Wala hajasomea madini anafuata shauri za kitaalamu za wasomi/profesa wetu
 
Sijamtaja Rais mahali popote, wala kuzielekeza lawama kwake. Si kufanya hivyo kutokana na sababu uliyoitoa kuwa Rais siyo mwanasheria, siyo mchumi, siyo mtaalam wa madini, japo kwa elimu yaje ya PhD anao uelewa wa kuchambua uthabiti wa taarifa au ushauri anaopewa na wataalam.

Mfahamu pia hata kule wizarani kuna wataalam. Na hawa wataalam ndio wanakuwa wa kwanza kuulizwa na sisi wataalam wenzao tulio nje ya serikali. Na hawa pia wanaeleza wasiyoridhika nayo. Hawa wataalam hawakushirikishwa kikamilifu katika mabadiliko ya sheria, tofauti na ile sheria mpya ya madini ya 2010, ambapo wote tulishirikishwa kikamilifu.

Kwenye sheria mpya ya 2010, walishirikishwa wanasheria, wataalam wa wizara, wachimbaji wakubwa na wa kati, watafiti, watunga sera, wachimbaji wadogo, mawaziri na balozi za nchi ambazo makampuni yao yamewekeza nchini kwenye sekta ya madini.

Unalotakiwa kujua pia ni unaweza ukaona tatizo mahali lakini namna ya kulitatua ukakosea na kusababisha tatizo kubwa zaidi.

Nafahamu kuna makosa ambayo waliyafanya na wanajua walifanya makosa. Kinachohitajika ni kutoka na kufanya marekebisho kikamilifu kuliko kufanya nusu nusu.

Mabadiliko yale ya sheria yaliegemea kwenye taarifa ambazo siyo sahihi zilizotolewa na timu ya Prof. Mruma. Kwa kiwango na uelewa wa Prof. Mruma na wale maprofesa wengine wa geology, siamini kama makosa yale yalitokana na upungufu wa weledi. Kama haikuwa matokeo ya upungufu wa weledi, ni nini kiliwasukuma kuudanganya umma kiasi kile? Swali jingine, upo wapi ujasiri wa wataalam wa kutetea weledi? Mambo yaliyoandikwa na timu ile ya Prof. Mruma ni sawa mwalimu wa hesabu akaandika kuwa 1+1 = 50,000! Kwenye hali hiyo ni ngumu sana kuelewa kwamba mwalimu huyu ana upungufu wa weledi maana hata akipungukiwa weledi, haiwezi kuwa kwa kiwango hicho na siyo kwa hesabu rahisi kiasi ya namna hiyo.
 
Sijampata Rais mahali popote, wala kuzielekeza lawama kwake. Si kufanya hivyo kutokana na sababu uliyoitoa kuwa Rais siyo mwanasheria, siyo mchumi, siyo mtaalam wa madini, japo kwa elimu yaje ya PhD anao uelewa wa kuchambua uthabiti wa taarifa au ushauri anaopewa na wataalam.

Mfahamu pia hata kule wizarani kuna wataalam. Na hawa wataalam ndio wanakuwa wa kwanza kuulizwa na sisi wataalam wenzao tulio nje ya serikali. Na hawa pia wanaeleza wasiyoridhika nayo. Hawa wataalam hawakushirikishwa kikamilifu katika mabadiliko ya sheria, tofauti na ile sheria mpya ya madini ya 2010, ambapo wote tulishirikishwa kikamilifu.

Kwenye sheria mpya ya 2010, walishirikishwa wanasheria, wataalam wa wizara, wachimbaji wakubwa na wa kati, watafiti, watunga sera, wachimbaji wadogo, mawaziri na balozi za nchi ambazo makampuni yao yamewekeza nchini kwenye sekta ya madini.

Unalotakiwa kujua pia ni unaweza ukaona tatizo mahali lakini namna ya kulitatua ukakosea na kusababisha tatizo kubwa zaidi.

Nafahamu kuna makosa ambayo waliyafanya na wanajua walifanya makosa. Kinachohitajika ni kutoka na kufanya marekebisho kikamilifu kuliko kufanya nusu nusu.

Mabadiliko yale ya sheria yaliegemea kwenye taarifa ambazo siyo sahihi zilizotolewa na timu ya Prof. Mruma. Kwa kiwango na uelewa wa Prof. Mruma na wale maprofesa wengine wa geology, siamini kama makosa yale yalitokana na upungufu wa weledi. Kama haikuwa matokeo ya upungufu wa weledi, ni nini kiliwasukuma kuudanganya umma kiasi kile? Swali jingine, upo wapi ujasiri wa wataalam wa kutetea weledi? Mambo yaliyoandikwa na timu ile ya Prof. Mruma ni sawa mwalimu wa hesabu akaandika kuwa 1+1 = 50,000! Kwenye hali hiyo ni ngumu sana kuelewa kwamba mwalimu huyu ana upungufu wa weledi maana hata akipungukiwa weledi, haiwezi kuwa kwa kiwango hicho na siyo kwa hesabu rahisi kiasi ya namna hiyo.
Mkuu hebu jibu kwanza hoja ya huyu mchangiaji SNAP J kwanza. Huyu Bams unakuwa kama unamuonea maana yeye ametilia mkazo zaidi hoja ya SNAP J hapo juu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi nikuulize, uliona sahihi Brady Gordon na mwenzie Geleta kuwafukuzs wafanyakazi wazawa 1600 wa Bulyanhulu ili kupisha wazungu 200 wa bynacut kutoka Australia ambao wakilipwa Mara kumi ya hao wazawa 1600 na uzalishaji wao ulikuwa nusu ya hao waafrica. Huo sio utakatishaji fedha huo? Unafikiri barrick Ni wajinga kuhakikisha kwa gharama yeyote acaciamining anaondoka? Wewe unaakili kuliko huyo myahudi?
 
Kwanini vitalu waendelee kukaa navyo hata kama hawana mpango wa kufanya mining?
The best way ni kukaa nao hao wadau na kupeana za uso. Lazima wafanye investment au waondoke
 
Katika awamu hii kuna sekta nyingi zimeharibiwa badala ya kuboreshwa ili ziwe na mchango chanya kwenye uchumi na maisha ya Wananchi.

Kusipofanyika mabadiliko ya haraka, kadiri tutakavyoenda, kila mwananchi, hata mwenye mwenye akili ya kawaida kabisa, atapata jibu kama tupo kwenye njia sahihi au tunaelekea shimoni.

Kati ya sekta zilizoharibiwa sana ni sekta ya madini. Hii sekta kabla ya uharibifu ilikuwa inaongoza kwa ukuuaji na uingizaji wa fedha za kigeni. Sekta hii iliharibiwa zaidi na mabadiliko ya sheria ya madini yaliyoandaliwa na kusukumwa kwa kiasi kikubwa na Prof. Kabudi, ambayo aliyafanya bila ya kushirikisha wadau wa sekta na wataalam wa Wizara ya madini kikamilifu.

Kabla sijaenda kwenye makosa yaliyofanyika, napenda nieleze wazi kuwa mimi ni mtaalam mwanasayansi kwenye sekta hii ya madini wa kiwango cha kimataifa ambaye nimekuwa nikijishughulika na usimamizi, uendeshaji, upatikanaji wa miradi ya madini katika nchi nyingi. Lakini pia nimekuwa nikishiriki kwenye upatikanaji wa mitaji kutoka soko la mitaji la Australian Securities Exchange (ASX) kwaajili ya uwekezaji kwenye miradi ya madini. ASX ndiyo soko kubwa kabisa Duniani kwaajili ya upatikanaji wa fedha za kuwekeza kwenye miradi ya madini. Ni kwa kupitia soko hili, matajiri wa mataifa kama Singapore, Hong Kong, Japan na Malaysia, huweza kuwekeza katika miradi ya madini iliyopo Afrika. Kwa hiyo ukilikosa soko la Hisa la Australia, utakuwa umekosa mitaji kutoka mataifa mengi, na siyo Australia pekee yake.

Madini yapo mataifa mengi Duniani. Na kila wakati madini hugundulika. Leo hii hata mataifa ambayo hapo awali hayakuwahi kufikiriwa kuwa na dhahabu, kutokana na teknolojia kukua ugunduzi wa migodi mipya umekuwa ukipatikana katika mataifa hayo.

Tanzania hatuna madini ya aina yoyote ambayo hayapatikani mahali pengine Duniani. Madini pekee ambayo tumekuwa tukizungumzia kuwepo Tanzania tu ni Tanzanite lakini kitaalam huwezi kusema kuwa madini ya Tanzanite hayapo mahali pengine Duniani. Tanzanite ni sapphire ambayo tofauti na sapphire nyingine, yenyewe ndani yake ina vanadium. Na wala Tanzania, katika uzalishaji wa dhahabu, hatuyakaribii mataifa kama ya China, Australia, South Africa, Peru, Mexico, Brazil, US, Russia au Indonesia. Nimeyasema haya ili Watanzania, na watu wengine kama akina Prof. Kabudi wajue kuwa hatupo pekee yetu Duniani wenye madini, na wala Dunia haiwezi kusimama kwa sababu hawatapata madini toka Tanzania.

Kutokana na uwepo wa madini katika mataifa mbalimbali Duniani, mataifa yote yamekuwa yakinyang'anyana wawekezaji wale wale wakubwa waliopo Duniani - New mont, Barrick, Anglogold, Kinross, Newcrest, Freeport, Polyus na Goldcorp. Ili uweze kuijenga sekta yako ya madini, kama Taifa, ni lazima uwe na wawekezaji wakubwa kwenye sekta ya madini, na hawa kwa Dunia nzima hawazidi makampuni 15 hivi. Utafiti ni gharama kubwa, na risk ya kupoteza pesa ni zaidi ya 95%. Ni hawa wenye mitaji mikubwa tu ndio wanaoweza kugharamia utafiti. Hawa ndio hufanya utafiti, na pale wanapopata resources ndogo, huziacha kwaajili ya makampuni madogo, na kwa hapa Tanzania maeneo hayo mara nyingi huvamiwa na wachimbaji wadogo.

Kuna watu kutokana na kukosa uelewa wa sekta hii, hudiriki hata kusema kuwa makampuni yamekuwa yakiwafuata wachimbaji wadogo, wakati ukweli ni kinyume chake. Huwa hawaujui ukweli kwa sababu huwa hawajui makampuni yalianza utafiti kwenye maeneo husika wakati gani. Na kwa vile mchimbaji mdogo anapovamia tu huanza kuchimba, watu humtazama anayechimba bila ya kumtazama aliyetafiti alianza lini. Kwa hiyo usipokuwa na makampuni makubwa, makampuni madogo hufa, na sekta ya uchimbaji mdogo nayo hufifia kabisa maana wao hawafanyi utafiti, na hawatapata mahali pa kuvamia.

Makosa aliyoyafanya Kabudi Kwenye Mabadiliko ya Sheria:

1) Masharti Magumu ya Kufanya Utafiti
Utafiti ni risk kubwa. ndiyo maana dunia nzima anayefanya utafiti wa madini hubembelezwa na siyo kumburuza. Kabudi kwenye mabadiliko ya sheria ameweka utaratibu wa kutosafirisha sampuli za madini kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine bila ya kibali cha afisa wa madini mkazi. Maabara ya madini inayotambulika Tanzania ipo moja tu kwa sasa, SGS. Mara ya kwanza maabara za madini zilikuwa kama 4 hivi, na zote zilikuwa Mwanza. Zote kwa sasa zimeondoka, imebakia 1. Unapofanya utafiti kama wa drilling, unahitaji activities continuity, na hivyo samples hutakiwa kupelekwa maabara wakati wote, usiku na mchana. Kuisimamisha rig kusubiria majibu ya maabara, gharama yake huwa ni dola 400 kwa saa. Kabudi anataka usipeleke samples maabara usiku wala siku za mapumziko kwa sababu huwezi kupata kibali. Maana yake ulipe zaidi ya dola 9,000 kwa siku kwa kusimamisha rig. Lakini hiyo sheria ililenga nini? Najua yeye alifikiria kuwa madini yanaibiwa kupitia samples. Jambo ambalo kwa mtu anayejua kinachofanyika, fikra hizo ni za kijinga kabisa maana ni jambo lisilowezekana. Ufafanuzi wake unaweza kuwa makala nyingine.

2) Kufuta Reetention Licenses
Kufuta Retention licenses, nao ulikuwa ni upuuzi wa hali ya juu. Serikali iliweka aina hii ya leseni ili kuyapa nafasi makampuni ambayo yamefanya utafiti na kufikia muda wa kuanza kujenga migodi lakini muda wa leseni zao au umeisha au ni mfupi kiasi cha kutotosheleza kufanya taratibu za kupata leseni ya uchimbaji. Leseni hizi zilitolewa kwa kipindi cha miaka 2 tu na ziliweza kurudiwa kwa kipindi kimoja tu, baada ya hapo ni ama unaanzisha mgodi au unalirudisha eneo serikalini. Serikali ilipendelea zaidi kutoa leseni hizi kuliko kutoa extension kwa sababu annual rent ya leseni hii ilikuwa dola 2,000 kwa kila square kilometre kwa mwaka, ukilinganisha na dola 100 kwa square kilometre kwa mwaka kwa leseni za utafiti. Leseni nyingi za retention zilikuwa na ukubwa wa kati ya square kilometre 10 - 30. Hivyo makampuni yalikuwa yakilipa kati ya dola 20,000 - 60,000 kwa mwaka kwaajili ya leseni tu. Mwekezaji amepewa leseni ya awali, ametumia mamilioni ya dola kufanya utafiti, umempa Retention License, tena mara nyingi kwa kumshahwishi, amekuwa akilipa ada zote, wengine walibakiza miezi tu Retention Licenses zao ziishe, ghafla unafuta leseni ambazo zilikuwepo kwa mujibu wa sheria yenu, unawanyang'anya haki yao uliowapa, na kwa mujibu wa sheria yako hawajavunja sheria yoyote - hiki ni nini, kama siyo ujambazi katika biashara na uwekezaji? Kutokana na tendo la kuwanyang'anya wawekezaji leseni zao bila haki yoyote, na kuzuia usafirishaji wa makinikia kwa sababu za uwongo kuwa kulikuwa na dhahabu inayoibiwa, Tanzania kwenye soko la hisa la ASX, ilitajwa rasmi kama siyo mahali salama kwa uwekezaji wa mitaji ya nje. Leo hii huwezi kupata fedha kwenye masoko makubwa ya fedha Duniani kwaajili ya kuja kuwekeza Tanzania. Unaweza kupata fedha kidogo kutoka kwa matajiri binafsi lakini siyo kutoka kwenye masoko ya fedha.

3) Utaratibu Sumbufu wa Kupeleka Sampuli Maabara za Nje
Kabudi kwenye sheria mpya, aliondoa utarattibu wa zamani ambao maabara za maandalizi zilikuwa zikiandaa sampuli zinazotakiwa kwenda nje ya nchi na kufuata taratibu za customs kwaajili ya kuzipeleka nje. Kwa sasa, ni lazima kwanza zipitie GST halafu ziende customs. Hizi samples, zile kwaajili ya Fire Assay au Aqua Regia (sample pulps) kila moja huwa na uzito wa 50 - 100gm; na zile kwaajili ya MET huwa kati ya 2 - 20kg kila moja. Lakini kwa nini uweke huo utaratibu mgumu? Maana kila ukiritimba unaouweka unaongeza business cost. Sababu ni ujinga ule ule kuamini kuwa kuna wizi wa madini unafanyika kupitia sampuli za madini. Ni fikra za kijinga kabisa za mtu asiyejua nini huwa kinafanyika kwenye suala la samples. Ni mada nyingine, kuna wakati nitaelezea.

4) Kodi za Ajabu
Hapo awali tulikuwa tunatoza mrabaha wa 3%, corporate tax ya 30%. Kikwete alikuja kuongeza mrabaha kwa kupitia majadiliano rafiki, mpaka kufikia 4%. Kabudi akapandisha kwa ubabe bila majadiliano mpaka 7%. Kwa nini alifanya hivyo? Nadhani aliamini kuwa 4% ni ndogo mno. Lakini nchi nyingine zinatoza nini? Mataifa karibu yote Mineral Royalty ni 0 - 5% tu. Ni Zimbabwe pekee yake ndiyo inayotoza 7%. Na hii inatozwa kwenye gross production value, haijalishi umepata faida au hasara. Kama mataifa mengine yanatoza kati ya 0 - 5%, kwa nini sisi tuliokuwa tunatoza 4% tuone kuwa tumekuwa tunaibiwa? Kwenye corporate tax, nchi nyingi zinatoza 20 - 30%. Zimbabwe wanatoza 28%. Kwa nini sisi tuliokuwa tunatoza 30% tuone kuwa tulikuwa tunaonewa? Naamini tuliongozwa na ujinga zaidi kuliko weledi.

5) Kufuta Usafirishaji wa Makinikia (Mineral Concentrate)
Kabudi kwenye mabadiliko ya sheria alifuta usafirishaji wa concentrates. Kwa nini alifuta? Naamini pia ni kwa sababu ya ujinga na kutotaka kushirikisha wataalam wa sekta hii. Kwanza hakuna kampuni inayopenda kusafirisha concentrates. Aina ya ore material, hasa inapokuwa na sulphides, humlazimisha mchimbaji kutafuta njia ya kuchenjua dhahabu inayokuwa imebanwa kwenye sulphides, na ambayo haitoki kwa njia za kawaida zilizozoeleka. Unatoa dhahabu huru (free gold), na ile iliyokuwa locked in, unafanya floatation kwa nia ya kutengeneza concetrates zitakazokuwa na dhahabu nyingi (mara nyingi ni kati ya 100 - 300g/ton, na siyo ule upuuzi walioutaja watu wa bandari kuwa concetrates zilikuwa na dhahabu 90%). Hiki ni kitu kinachofanyika Duniani kote. Zambia, Canada, Indonesia, Australia, Mali, Ghana, Brazil, etc, wote wanapeleka concentrates zao, hasa Japan. Kama hawa wote wanasafirisha concentrates, ni sababu gani inayotufanya sisi pekee yetu tuamini kuwa hawa wengine wote hawaibiwi isipokuwa sisi tu? Athari ya sheria ile mbaya ya Kabudi, deposits zote zenye refractory gold hazitaweza kuja kuwa migodi. Siku zote, kazi ya serikali inayoongozwa na watu wenye hekima ni kujenga mifumo na kuweka taratibu zinazorahisisha na kupunguza gharama za uwkezaji na biashara huku ikiangalia faida pana ya wadau wote.

6) Data Zote za Utafiti Kupelekwa Serikalini
Kabudi kwenye sheria yake ya mabadiliko, anayalazimisha makampuni yote yanayofanya utafiti nchini, kupeleka data za utafiti GST. Jambo hili halipo Duniani kote. Utafiti ni risk kubwa na ni gharama kubwa, na pia ni confidential information. Kampuni ya utafiti wa madini, asset yake kubwa ni data za utafiti. Ni hizo data ndiyo zimeifanya kampuni kutumia mamilioni ya dola. Wewe unasema wafanye utafiti, data wakupe wewe!! Haijawahi kusikika. Utaratibu uliopo mataifa mengi Duniani, kampuni hufanya utafiti, wakiamua kuanzisha mgodi, data zinaendelea kuwa zao, Wakiamua kulirudisha eneo serikalini, wanarudisha eneo, na wanaipatia serikali data zote. Kuyataka makampuni kukabidhi GST raw data ni kati ya hitaji la ovyo kabisa kuwahi kuwepo katika ulimwengu huu.

Makosa haya makubwa yaliyofanywa na Prof. Kabudi yana athari zifuatazo:

1) Taswira Mbaya ya Mazingira ya Uwekezaji ya Nchi Yetu
Leo huwezi kuwapata wawekezaji wakubwa kuja kuwekeza Tanzania. Katika kipindi chote cha awamu hii, hakuna mwekezaji mkubwa (>U$500m), aliyeweza kuwekeza Tanzania, awe wa ndani au wa nje.

2) Kifo cha Makampuni
Makampuni yote ya madini yaliyowekeza Tanzania na ambayo yanafanya biashara kwenye masoko makubwa ya fedha, kutokana na mabadiliko yale ya Kabudi yalipoteza kati ya 30 - 60% kwenye capitalization ya makampuni kwa sababu yamewekeza kwenye mazingira hatarishi ya mitaji. Kupoteza capitalization ya kiasi hicho ni kuua kampuni. Makamuni haya yote, kwa kiasi kikubwa yameondoka Tanzania na mengine yamebakia tu kwenye vitabu vya serikali lakini kiuhalisia yameondoka na hayafanyi chochote nchini

3) Kulipa Fidia
Makampuni yote yaliyonyang'anywa maeneo kwa kufutiwa Retention Licenses zao, karibia yote yatataka kulipwa fidia na serikali au kufungua kesi za fidia kwenye mahakama za kimataifa. Tayari makampuni mawili yameipelekea notice serikali. Hata kwa mimi nisiye mwanasheria, nina uhakika wa over 99% kuwa serikali itashindwa katika kesi zote zitakazofunguliwa, na hivyo kutakiwa kulipa fidia

4) Kupungua kwa Mapato ya Serikali
Makampuni makubwa yanayochimba dhahabu kwa sasa, yataendelea kuwa hayo hayo. Lakini makampuni hayo yana uwezekano mkubwa wa kufunga migodi yao mapema zaidi kuliko muda uliotarajiwa kutokana na kuongezeka kwa gharama. Makampuni haya imebidi kuweka cutoff grades mpya ili kuendana na gharama za uzalishaji zinazochangiwa na kodi na tozo kubwa zaidi kuliko ilivyokuwa. Na wala hakutakuja kuwa na miradi mikubwa mipya.

5) Kudumaa kwa Technology Transfer
Ujio wa makampuni makubwa kabisa yanayotumia teknolojia za kisasa kama Barrick na Anglogold, ulifanya watanzania wengi kupata teknolojia ya juu na ya kisasa kabisa Duniani. Leo hii, nchi zinazoongoza katika utaalam wa madini Afrika, ni South Africa, Ghana kisha Tanzania. Leo hii Watanzania wapo kwenye nafasi za juu kwenye miradi ya madini katika mataifa mbalimbali. Kuondoka kwa makampuni haya makubwa, kutalifanya Taifa kwenda kwenye udumavu wa maarifa kama ilivyokuwa zamani. Katika utaalam, wataalam wa Tanzania kwenye sekta hii, wapo juu maradufu kuzidi wataalam kutoka mataifa kama vile China. Mimi binafsi nimekuwa nikizunguka, pamoja na kazi nyingine, lakini nimekuwa nikitoa mafunzo kwa wataalam wa sekta hii. Wakati mmoja nilipokuwa nikitoa mafunzo kwenye mgodi mmoja wa Waingereza, nilikuwa na wanafunzi 84, na kati ya hao Waafrika walikuwa 29, Waingereza 34, Wairan 2, Waaustralia 2, Wacanada 3, Wachina 3, Wavietinam 5, Waindonesia 6

6) Athari nyinginezo
Nyingine ni zile za kawaida ambazo kila mwenye ABC ya uchumi anazijua - kama vile kupungua kwa ajira, business interactions, na uchangamshashaji wa uchumi, kupungua kwa fedha za kigeni (sekta hii na ya utalii ndizo zinazoingiza fedha za kigeni nyingi kuliko sekta nyingine zote)

NINI KIFANYIKE
1) Kufutwa kwa Mabadiliko
Sheria ile mpya ya Kabudi ifutwe. Na kama kuna haja ya kufanya mabadiliko, yafanyike kwa kushirikisha wadau wote, na yafanyike kwa njia ya maelewano

2) Retention Licenses Zirudishwe
Wamiliki wa Retention Licenses warudishiwe, na wapewe muda wa ama kujenga migodi au kuyarudisha maeneo wanayoyamiliki kwa serikali. Hata wauaji hupelekwa mahakamani kujitetea, lakini Retention License holders, walinyang'anywa rights zao bila ya kupewa sababu, kupewa nafasi ya kurekebisha, kama kweli kulikuwa na makosa.

3) Majadiliano Rafiki
Wamiliki wa Retention Licenses wanaokusudia kuifikisha serikali/nchi kwenye mahakama za usuluhishi za kimataifa ili kulipwa fidia waalikwe kwenye mazungumzo ili wasifanye wanachotarajia kukifanya. Serikali ikiri ilifanya kosa, na iombe ikubaliwe kutolipa fidia yoyote kwa wawekezaji walioathirika na uamuzi wa kuwanyang'anya leseni zao kinyume cha sheria.

4) Wadau Wataalam Watoe Muongozo
Kama nilivyoeleza, sekta hii ina Watanzania wataalam waliobobea, na walioenea Duniani kote, wao kwa kushirikiana na wataalam wa Wizara, watoe mwongozo kwa serikali namna ya kuihuisha sekta hii baada ya kuidumaza kwa miaka hii minne kutokana na mabadiliko Kabudi. Wataalam hawa watumike kufikisha kwenye masoko ya fedha Duniani na taasisi mbalimbali za kimataifa, kufutwa kwa mabadiliko yaliyoiharibu sekta. Jambo hili siyo geni. Huko Australia, kuna Waziri mkuu mmoja alianzisha Mining Super Profit Tax. Mwanzoni wananchi walimshangilia. Baadaye madhara yalipoanza, wananchi walimchukia Waziri Mkuu na kumwondoa madarakani. Waziri Mkuu mpya akaifuta hiyo kodi, na baada ya muda sekta ya madini ilirejea kwenye utengamano.

JUMUISHO

1) Kuwa msikivu na hekima, siyo unyonge au udhaifu, sawa kama ilivyo, kuwa katili siyo ushujaa

2) Hakuna nchi hata moja iliyowahi kuendelea kwa kuwategemea watu wake tu. Mchangamano wa watu, makampuni na taasisi za mataifa mbalimbali ndiyo hujenga Taifa ka kasi. Mfano mzuri wa karibu ni Dubai, South Africa, Nigeria, Botswana. Kwa upande mwingine, tujifunze toka China. China chini ya kiongozi wao Mao, na mfumo wao wa Maoism, uchumi wao ulikuwa wa kujifungia. Miaka yote waliendelea kuwa Taifa duni, hata nguo wakivaa zenye viraka magotini na makalioni. Mwishoni walirejewa na akili, wakaufungua uchumi wao kwa Dunia. Makampuni ya America na Ulaya, yakawekeza huko kupindukia, hata kuufanya uchumi wa China kupaa. Ni uwekezaji huo ndio ulioingia na teknolojia ambayo Wachina mpaka leo wamekuwa wakiiga kwa kasi kubwa. Japo makampuni makubwa yaliyopo China hayamilikiwi na Wachina, lakini makampuni hayo yameifanya China kukua kwa kasi kiuchumi na kitekinolojia.
una la kuongeza baada ya makubaliano ya ikulu leo?
 
Wewe umetumwa siyo bure. Nchi hii imeibiwa sana. It's better tuwe na masharti. Magumu ili nchi inufaike Coz madini yanaisha. Tumeshaibiwa sana kwa sheria mbovu.
 
Kipindi tunaibiwa nchi hii ilikuwa inaongozwa na serikali ya chama kipi ?
 
Sijasoma yote ila maelezo yako mazuri na yapo kitaalamu na yanavutia.Shida hao viongozi na wananchi watakuambia umetumwa! Something has to be done hata kwa nguvu, otherwise we are falling to the dark side
 
Laizer wa Tanzanite amefunga hii thread technically.
Effects zote nullified
Recommendations zote ziko diluted.
 
Weka usahihi wa kitakwimu mwanzoni kabla ya sheria mpya amabayo ulioanza kumshambulia Professor Kabudi kutumika tulikuwa tunaingiza kiasi gani na baada tunaingiza kiasi gani?

Bila kuleta mahesabu itakuwa unatumika(puppet) wa mabeberu.
 
Back
Top Bottom