Mabadiliko ya Profesa Kabudi kwenye sheria ya madini yanalitesa Taifa. Nini kifanyike?

Bams,
Kumbe bado tuna watanzania wenye akili namna hii? Nimekuelewa sana. Only a fool will argue otherwise.
Lakini takwimu za serikali zinaonyesha hapo kabla tulikuwa hatupati chochote japo uzalishaji ulikuwa juu kitakwimu. Faida yote walikuwa wanaondoka nayo.
 
Lakini takwimu za serikali zinaonyesha hapo kabla tulikuwa hatupati chochote japo uzalishaji ulikuwa juu kitakwimu. Faida yote walikuwa wanaondoka nayo.
Usidanganyike. Ongezeko na thamani ya mauzo, kwa kiasi kikubwa limetokana na ongezeko la bei ya dhahabu Duniani.

Hapo mwanzo kulikuwa na makampuni ya nje zaidi ya 150 yaliyokuwa yakifanya utafiti wa madini Tanzania. Sahizi hakuna kampuni hata moja inayofanya utafiti. Maana yake ni kwamba migodi inayozalisha sasa, ikifungwa hakutakuwa na migodi mipya. Maana yake hakuna sustainability ya industry.

Buzwagi inategemea kukoma uzalishaji mwaka huu. Bulyanhulu mpaka sasa hakuna uchimbaji. Tulawaka waliachiwa STSMIGOLD, uzalishaji wao ni wa kusuasua licha ya kwamba walipewa kila kitu bure na Barrick. Replacement ya migodi inayofungwa ipo wapi?

Makubaliano kati ya Tanzania na Barrick yana mengi yaliyofichika. Barrick ni kampuni ambayo haijawahi kupata hasara tangu ianzishwe. Hiyo ni kutokana na umahiri wa watu wake. Mtazamo wa Barrick ni tofauti sana na wengi wanavyofikiria. Barrick hataanzisha mgodi mpya hata mmoja Tanzania kwa mazingira ya sasa. Anachofanya ni kuhakikisha anaendelea kutunza record yake ya kutopata hasara mahali popote anapowekeza.

Ebdelea kukumbuka nadharia inayoongoza Barrick kuhusiana na watu wake: EVERY BEST PERSON MUST WORK WITH BARRICK. Ndani ya Barrick kuna vichwa, siyo hivi vya akina Kabudi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Weka usahihi wa kitakwimu mwanzoni kabla ya sheria mpya amabayo ulioanza kumshambulia Professor Kabudi kutumika tulikuwa tunaingiza kiasi gani na baada tunaingiza kiasi gani?

Bila kuleta mahesabu itakuwa unatumika(puppet) wa mabeberu.
OP a nakwambia yalikuwepo makampuni mengi zaidi ya 150 ya kufanya utafiti wa madini.

Lakini hataki kusema mapato yalikuwa ni kiasi gani na mgawanyo ulikua vipi.

Hao wote waliokuwa wanajifanya wanatafuta walikua hawanalizi tafiti zao miaka nenda rudi. Kwa sababu walikua wanachimba na kuuza so called samples. Na wengine ni madalali wa maeneo yetu yenye madini. Asilimia kubwa ya watu hao wako Australia na Canada.
 
Akina Lisu bado wanaendelea kuzaliwa! Mwalimu aliwahi sema vitu vya thamani namna hii siyo vya kugawa kama zuzu hivi! Akaendelea kusema mna haraka gani kwani madini yanaoza? kama hayaozi, acheni vijana wazawa wawe na uelewa wachimbe kizalendo kuliko kutegemea wawekezaji. Naona ndugu unatetemeka sana na wanyonyaji wa dunia, samahani wawekezaji!. Hawa hawana nia ya kukuendeleza wewe, nia yao ni kupata faida kubwa kwa wajinga wasiojua thamani ya dhahabu! kwa taarifa yako sasa hivi wachimbaji wadogo/wazawa wanalipa kodi kubwa Serikalini kuliko hao jamaa unaowapigia debe hapa! Na mapato ya madini yameongezeka. Sijasema hujui ila naona una shida ya kuelewa uchumi wa dunia unavyoendeshwa, umesoma madini sawa lakini uchumi yaani ni jinsi gani nchi zenye mitaji zinanyonya nchi zisizojitambua hujalielewa hilo! Kama kweli wewe ni msomi nakushauri isaidie nchi yako kujitegemea na siyo kutegemea watu wengine wenye nia ya kupata faida kubwa!. Nashauri Serikali ianzishe benki ya madini wazawa tutakopa na tutachimba, maana elimu, maarifa na nguvu ya kufanya haya ipo.
 
..serikali imetusaliti kwa kuwasamehe Barrick deni la usd 191 billion na badala yake wakakubali kishika uchumba cha usd 300 million.

..hiyo ni pesa kubwa sana kuisamehe hivihivi tu bila maelezo ya kutosha na yenye mantiki.

..Timu iliyokwenda kujadiliana na Barrick ilijumuisha pia wajumbe wa tume mbili za uchunguzi ambazo walibainisha wizi huo wa usd 191 billion.

..Tulikwama wapi? Nini mantiki ya kuachia fedha zote hizo? Na baada ya hapo tunakwenda kukopa World Bank kwa ajili ya elimu.
 
Back
Top Bottom