Mabadiliko ya kweli yanaonekana Muhimbili

Shukuru malaika wa mwanao waikua pamoja nae na akawaandaa watu lakini kuna some weeks was having Mgonjwa pale mambo hayakua mazuri bado nyodo bado zipo.So shukuru Mungu tu ndugu ndo kamwokoa.

Sema na wewe ulikuwa na bahati mbaya, mi nimeenda muhimbili huuma niliyopewa nikatamani kuwapa fedha nikawa nawaaangalia usoni pengine wanidai chochote lakini wala hawakuonyesha dalili. Kila mmoja alipomaliza kazi yake ali nipost sehemu nyingine, hiyo ni emergency! Yaani acha tu, labda kama wewe ulikwenda na 'attitude'
 
Kuna watu wanakesha wakiomba mambo yaende vibaya kila mahali wapate pa kumkosolea Magufuli.
Yani wanaomba hata huduma za hospitali zizorote wagonjwa wapoteze maisha ilimradi tu wapate cha kukosoa hata kama maombi yao yanazaa mauti kwa binadamu wenzao.
 
wapendwa wachangiaji, katika hoja yangu sikuzungumzia gharama nimezungumza huduma tu kwani hapo zamani pamoja na hela yako bado huduma haikuwa nzuri. Kuhsu gharama nilifanya malipo ya kufungua faili, vipimo vya xray na CT Scan pamoja na gharama za kulazwa kule MOI.

All in all mabadiliko kuhusu huduma yapo ila kuhusu gharama no comment nawaachia wao wenyewe.

Ulikuwa na bahati na Mungu aliamua kukuonyesha first impression yako Kwa muhimbili iwe hivyo. Ukienda Kwa Mara ingine utajiuliza hivi ni muhimbili hiyo hiyo jitahidi usije pata mshtuko maana hapa tunajitahidi kukuandaa kisaikolojia. Tunashukuru pia Kwa mtoto kutibiwa na kuendelea vizuri kuna mzazi mwenzetu anaomba msaada kupitia Chanel ten kwa sababu mtoto amekatizwa matibabu muhimbili kwa sababu hana hela na ameonekana amembeba mwanae hawezi kutembea anatia uchungu sana ajabu muhimbili hiyo hiyo waliokuchamkia wewe hadi umejisikia faraja. Unaweza kufikiria hadi ukadhani ni ndoto siyo kweli utasemayo. HIYO NDIYO MUHIMBILI NDUGU consistency hakuna
 
Wiki tatu zilizopita mtoto wangu alipata ajali mbaya na nikampeleka hospitali binafsi (siitaji) wakasema hawawezi kumtibu kwani hali yake ni mbaya sana na nikapewa rufaa nikaenda M`nyamala na mishowe muhimbili. Nilipofika muhimbili mtoto alipokelewa kwa kasi ya ajabu na madaktari zaidi ya wanne walikuwa wanamhudumia kwa pamoja na kwa kweli baada ya saa moja hali ya mtoto ilianza kutengemaa na baada ya masaa mawili hatari ya kupoteza maisha ilipungua sana ndipo nikaambiwa sasa nianze taratibu za kufungua faili.

Aidha, huduma ya vipimo vya X-ray, CT scan nk ilikuwepo 24hrs na majibu yanatoka hapohapo. Baada ya kutoka emergency nilihamishiwa MOI nako huduma ilikuwa ya kiwango cha juu sana kwa siku zote hadi mtoto alipata nafuu na kuruhusiwa.

Jana ikiwa ni 14 days baada ya kuruhusiwa madaktari wa emergency wamenipigia simu na kuulizia mgonjwa anaendeleaje baada ya kuruhusiwa, changamoto nyingine anapata na maswali mengineyo mengi kuja afya na maendeleo wakashauri hatua za kuchukua.

Huu ni muujiza na kweli MUHIMBILI IMEBADILIKA. Watanzania tutambue kuwa kiongozi mkuu akiwa serious walioko chini wote watabadilika. Nawashauri na wengine mgonjwa anapokuwa serious Muhimbili is the best. Nawaomba muhimbili muendelee na maboresho ya huduma mliyokwishayaanza.

VIVA MAGUFULI
Mkuu mwogombe Mungu kwa uongo wako mi nilikiwa na mgonjwa hapo muhimbili kama wiki imepita sasa huduma siyo kabisa.
Dah nchi hii jmn acha jana nimeangalia mzee mmoja kaenda chanel ten kuomba msaada wa matibabu ya mwanae dah mtt kiukwel hali yake mbaya ameshindwa gharama za hospital muhimbili anadai laki 7 na mtt hali yake mbaya sana mzee hana uwezo mtt alipata ajali nikisoma maelezo ya hii thread dah nachanganyikiwa sasa je mzee anatumia njia mpya kuomba na sio ya zamani kukaa barabarani pls nyie matajiri acheni utani watu wanakufa kwa kukosa uduma bora andika cha ukwel
 
Shida ninayoiona kwa wananchi wetu ni kufikiri kuwa matibabu na vipimo ni bure....thubutu!...kata bima au uwe fedha ya natibabu acheni porojo...huduma haziwezi kuwa bora kama mnataka dezo!...Period!
 
Ulikuwa na bahati na Mungu aliamua kukuonyesha first impression yako Kwa muhimbili iwe hivyo. Ukienda Kwa Mara ingine utajiuliza hivi ni muhimbili hiyo hiyo jitahidi usije pata mshtuko maana hapa tunajitahidi kukuandaa kisaikolojia. Tunashukuru pia Kwa mtoto kutibiwa na kuendelea vizuri kuna mzazi mwenzetu anaomba msaada kupitia Chanel ten kwa sababu mtoto amekatizwa matibabu muhimbili kwa sababu hana hela na ameonekana amembeba mwanae hawezi kutembea anatia uchungu sana ajabu muhimbili hiyo hiyo waliokuchamkia wewe hadi umejisikia faraja. Unaweza kufikiria hadi ukadhani ni ndoto siyo kweli utasemayo. HIYO NDIYO MUHIMBILI NDUGU consistency hakuna

Wewe huelewi nini kimeongelewa hapo umekurupuka,sasa kukosa pesa za matibabu na kuimalika kwa huduma hapo muhimbili kuna uhusiano gani???mtoa mada kaeleza ni jinsi gani huduma zilivyo ok ukilinganisha na zamani hata ukilipia ilikuwa nado mizinguo mingi kuliko sasa!kwa kifupi hakuna cha bure,amekosa huduma yuyo mtu kuna utaratibu wa kufata kupatiwa huduma,...sio unakurupuka tu hapa!
 
wapendwa wachangiaji, katika hoja yangu sikuzungumzia gharama nimezungumza huduma tu kwani hapo zamani pamoja na hela yako bado huduma haikuwa nzuri. Kuhsu gharama nilifanya malipo ya kufungua faili, vipimo vya xray na CT Scan pamoja na gharama za kulazwa kule MOI.

All in all mabadiliko kuhusu huduma yapo ila kuhusu gharama no comment nawaachia wao wenyewe.
we nawe peleka huko story za kutunga na propaganda za kijinga unasifu nini cha ajabu hao unaowasifia ni wajibu wao tunawalipa mishahata.watu tuliopevuka kiakili huwa hatutoi sifa ovyo hovyo
 
Huu Uzi Uongo Mtupu! Ulitumia hela (Hongo/Rushwa) tu kufanya Shotkati mambo yako ikisha unatoa sifa za kusadikika!!
 
Wewe huelewi nini kimeongelewa hapo umekurupuka,sasa kukosa pesa za matibabu na kuimalika kwa huduma hapo muhimbili kuna uhusiano gani???mtoa mada kaeleza ni jinsi gani huduma zilivyo ok ukilinganisha na zamani hata ukilipia ilikuwa nado mizinguo mingi kuliko sasa!kwa kifupi hakuna cha bure,amekosa huduma yuyo mtu kuna utaratibu wa kufata kupatiwa huduma,...sio unakurupuka tu hapa![/

Wewe umeandika Kwa kutulia kabisa hongera sana kwa utulivu wa maandiko yako
 
Back
Top Bottom