Wiki tatu zilizopita mtoto wangu alipata ajali mbaya na nikampeleka hospitali binafsi (siitaji) wakasema hawawezi kumtibu kwani hali yake ni mbaya sana na nikapewa rufaa nikaenda M`nyamala na mishowe muhimbili. Nilipofika muhimbili mtoto alipokelewa kwa kasi ya ajabu na madaktari zaidi ya wanne walikuwa wanamhudumia kwa pamoja na kwa kweli baada ya saa moja hali ya mtoto ilianza kutengemaa na baada ya masaa mawili hatari ya kupoteza maisha ilipungua sana ndipo nikaambiwa sasa nianze taratibu za kufungua faili.
Aidha, huduma ya vipimo vya X-ray, CT scan nk ilikuwepo 24hrs na majibu yanatoka hapohapo. Baada ya kutoka emergency nilihamishiwa MOI nako huduma ilikuwa ya kiwango cha juu sana kwa siku zote hadi mtoto alipata nafuu na kuruhusiwa.
Jana ikiwa ni 14 days baada ya kuruhusiwa madaktari wa emergency wamenipigia simu na kuulizia mgonjwa anaendeleaje baada ya kuruhusiwa, changamoto nyingine anapata na maswali mengineyo mengi kuja afya na maendeleo wakashauri hatua za kuchukua.
Huu ni muujiza na kweli MUHIMBILI IMEBADILIKA. Watanzania tutambue kuwa kiongozi mkuu akiwa serious walioko chini wote watabadilika. Nawashauri na wengine mgonjwa anapokuwa serious Muhimbili is the best. Nawaomba muhimbili muendelee na maboresho ya huduma mliyokwishayaanza.
VIVA MAGUFULI