Sir John Roberts
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 12,601
- 23,252
Hii hospitali kama serikali na uongozi hautachukua hatua za haraka watanzania wengi wataendelea kufa kwa uzembe wa madaktari wanafunzi ambao hawasimamiwi ipasavyo na wakuu wao kazi.
Nimeshuhudia mgonjwa wangu akiambiwa hana tatizo lolote la nyonga baada ya kumpeleka akiwa amepata ajali na daktari ambaye ni mwanafunzi kusoma vipimo akatuambia mgonjwa aendelee na dawa alizopewa ( tulianzia matibabu hospitali ya wilaya kabla ya kwenda hapo mloganzila)
Tulipata mashaka na tukarudi tena kuomba uchunguzi zaidi ndipo daktari msimamizi wa mwanafunzi huyo alipokuja nadhani alikua kikaoni na baada ya kupitia tena vipimo alibadilika ghafla na kuwa mkali sana na kumfokea yule daktari mwanafunzi kuwa kwanini hajaona tatizo la nyonga kuvunjika? Na ni eneo hatari sana kwa mgonjwa? Japo alikua akimfokea kwa kiingereza ila tuliweza kujuwa kuwa daktari mwanafunzi alizembea katika matobabu ya ndugu yetu.
Nashukuru tumepangiwa tarehe ya operesheni. Ila nimeondoka na maswali mengi kichwani je ni wagonjwa wa ngapi wanaopitia hali kama tuliyopitia sisi?
Naomba serikali na uongozi mzima wa hospitali ya taifa ya Muhimbili (mloganzila) kuchukua hatua za haraka kuokoa maisha ya watanzania.