Mabadiliko katika jamii yana faida na hasara zake

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Zamani haikuruhusiwa binti kuzaa nje ya ndoa. Ikitokea binti amepata ujauzito kabla ya ndoa, wazazi walimlea mpaka anajifungua na akisha jifungua mtoto anatolewa kwenda kuasiliwa.

Wazazi wengine waliwapeleka watoto wao kwenye nyumba za watawa. Kule mabinti walifanya kazi ya kufua nguo, kuanzia shuka za wagonjwa hospital mpaka shuka za mahotelini. Wakati huo hakukua na mashine za kufulia. Mabinti hawa wote wakishajifungua wanawatoa watoto wao kwa familia zilizo kwenye ndoa ili watoto wapate malezi mema.

Mabinti hawa waliaswa watulie ili wapate wachumba wa kuwaoa. Dawa za kuzuia uzazi zilitolewa kwa wanawake walio kwenye ndoa tu. likizo ya uzazi ilitolewa kwa wanawake walio kwenye ndoa.

Siku hizi binti anapata ujauzito nje ya ndoa na jamii inaona ni mambo ya kawaida. Mabadiliko makubwa yalisababishwa na vita. Wanaume waliofia vitani wake zao walibaki kama single parents.

1614091891808.png

Huyu mama alimtoa mtoto wake kuasiliwa. Sasa hivi anamtafuta.
 
Back
Top Bottom