Mabadiliko Jeshi la Polisi: IGP Sirro ampeleka Kamanda Mambosasa Dodoma, Wambura amrithi kanda maalum Dar

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
SACP CAMILIUS WAMBURA KAMANDA KANDA MAALUM DSM

===


INSPEKTA Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro amefanya mabadiliko madogo kwa baadhi ya viongozi ndani ya Jeshi la Polisi ambapo amemhamishia Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Lazaro Mambosasa kutoka kuwa kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam na kwenda kuwa Mkuu wa Operesheni Dodoma.

Katika barua iliyosainiwa kwa niaba yake na Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu, imeeleza kuwa IGP amemwamisha pia aliyekuwa Mkuu wa Operesheni Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Camilius Wambura kuwa Kamanda wa Polisi Dar es Salaam.

Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Daniel Shillah amebadilishiwa kituo cha kazi kutoka kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara na kuwa Mkuu wa Upelelezo (ZCO) Kanda Maalum Dar es Salaam huku nafasi anayoaacha Mara ikichukuliwa na Kamishna Msaidii Longinus Tibishibwamu.

Pia IGP amembadilishia majukumu Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Optatus Maganga amehamishwa kutoka OCD wa wilaya ya Makete na kuwa Kamanda wa Polisi Njombe wakati Mrakibu wa Polisi (SP), Vitus Marekani.


POLISI.jpg
 
SACP CAMILIUS WAMBURA KAMANDA KANDA MAALUM DSM

View attachment 1788935
Safi sana Poti wangu mkubwa kutoka Mkoani Mara (Musoma) kwa Shavu hilo Kubwa. Hii nafasi ilikuwa inakusubiria Kitambo tu na najua huyu aliyetolewa alikuwa akikufitinisha sana na Wakubwa zako ili Yeye asitolewe hapo kwa Kulindwa Kwake na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

Kiukweli sikuwahi kuona Jipya la Kiutendaji kwa Mambosasa zaidi tu ya Ubabe, Ukatili, Vitisho na Roho Mbaya yake aliyoambukizwa vyema na Rafiki yake Paul Makonda aliyekuwa Mkuu wa Mkoa mbovu kuwahi kutokea katika Mkoa wa Dar es Salaam.
 
Back
Top Bottom