Nchi yetu haitawaliki tena kutokana na Uongozi mbovu. Ukisoma kwa makini madai ya madaktari utajua makosa yako ktk muundo mzima wa AFYA nchini lakini nina hakika wananchi hawako tayari kukubali ukweli kama wanavyomshabikia Lowassa arudi madarakani. Bunge linaloshindwa kuwaita viongozi wahusika wa mgomo huu bungeni kujibu ama kutafuta suluhu kwa sababu ya kanuni ambazo hazikutegemea dharura kama hii ni mfano mzuri sana kuonyesha kwamba Katiba nzima ya Tanzania inatakiwa kutazamwa Upya...
Pengine nikubali kwamba huu mgomo wa madaktari unaweza kuwa mwanzo wa anguko la CCM lakini kama kweli wamekubali kukutana na kamati ya Bunge ili wapate kuongezewa posho, bima na kadhalika wakati wananchi na watumishi wengi nchini hawana posho wala bima hizi ni mwanzo wa kuivuruga nchi kwenda bila dira, sera na ilani...
Nitarudia kusema kama daktari haridhiki na kazi au mazingira ya kazi alo ajiriwa anatakiwa kuandika barua ya kuacha kazi na atafute sehemu nyingine..Lakini hili haliwezekani kutokana na kwamba vitengo vyote vya Afya nchini vinalindwa na mfumo mmoja ambao ndio tatizo kubwa. Isipokuwa kama lilivyo swala la waziri mkuu mstaafu Lowassa, wananchi wameamua kulifumbia macho na kama kawaida yetu kutafuta mchawi mwingine hali mchawi tunaye na tunakula naye meza moja.