Maazimio ya Kamati Kuu ya CHADEMA Sept 10, 2012

Maazimio ya Kamati Kuu ya CHADEMA Sept 10, 2012

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeonyesha picha za mnato na video zinazoonyesha jinsi Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Television cha Channel Ten, Daudi Mwangosi, alivyouawa.

Picha hizo zilionyeshwa jana jijini Dar es Salaam, wakati wa kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kilichohudhuriwa pia na waandishi wa habari. Kikao hicho cha Kamati Kuu kilikuwa ni cha dharura na kilifunguliwa na kuongozwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.
Wakati picha hizo zikionyeshwa wazi wazi, viongozi wa CHADEMA na waandishi wa habari, walishindwa kujizuia kwani baadhi yao walijikuta wakiangua vilio wakionyesha kusikitishwa na jinsi Mwangosi alivyouawa.
Katika tukio hilo, Mbowe ni kati ya waliolia na ilifika wakati akanyanyuka kutoka meza kuu na kwenda nje ya ukumbi, ili asiendelee kushuhudia Mwangosi alivyouawa.
Wakati picha hizo zikionyeshwa kwa zaidi ya masaa mawili, askari polisi walioshiriki kumuua Mwangosi walionekana wazi wazi na pia Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda, alionekana pia eneo la tukio akishuhudia Mwangosi akiuawa.
Kwa mujibu wa picha hizo, mwandishi wa habari aliyeanza kukamatwa na askari polisi na kupata kipigo ni Godfrey Mushi wa Gazeti la Nipashe.
Picha hizo za video zilionyesha kuwa, baada ya Mushi kukamatwa, Mwangosi alikwenda kumuokoa mwenzake huyo na alipofika eneo la tukio, askari hao walianza kumpiga na hatimaye kumuua mbele ya Kamanda Kamuhanda.
Picha hizo zinaonyesha kuwa, kabla Mwangosi hajauawa, polisi mmoja alipitisha bunduki yake miguuni kwa polisi mwenzake kisha Mwangosi akauawa.

CHANZO: GUMZO LA JIJI
 
"Operesheni MOVEMENT FOR CHANGE M4C,Inaendelea kadiri ya ratiba ilivyopangwa katika utaratibu uleule uliokuwepo awali.Inarejea Iringa Siku si nyingi.Na kamati kuu Imetoa msisitizo MAALUM kwa jimbo mojawapo singida,ambapo wamesema watatumia helcopita,magari,pikipiki na baiskeli na miguu,na badala ya kupita vijijini kama majimbo mengine,Chadema wanasema kwa sababu maalum katika jimbo hilo watapita kitongojikwa kitongoji,ili kufunza adabu baadhi ya viongozi (msisitizo ni wa msoma MAAZIMIO.jimbo hili laweza kuwa la Mwigullu Mchemba,kadiri ya wanahabari waliokuwepo)"

Yaani ugomvi binafsi wa Mbowe na Mwigulu umezaa sera rasmi ya CHADEMA. Wanachama wa CHADEMA wanatumiwa kama fimbo ya mbowe kuonyesha ufahari kwa maadui zake!!!
 
''Kutokana na mgogoro wa muda mrefu mkoani mwanza uliosababisha meye wa chadema kuvuliwa umeya kinyume na utaratibu na kwa njama za CCM na Serikali,na bahati mbaya sana kwa kushirikisha madiwani wa CHADEMA,KAMATI KUU imewavua UANACHAMA madiwani wake wawli 1 ADAMU CHAGULANI wa kata ya IGOMA na HENRY MATATA wa KITANGIRI, PIA uongozi wote wa CHADEMA mkoa wa mwanza Umevunjwa.''

Vigogo wa CHADEMA wakiwa na kashfa zinaishia magazetini. Madiwani wanafukuzwa mara moja. Hili lilifanyika Arusha, limejirudia Mwanza. What about vigogo? Haya ya kuvua vidagaa na kuacha makambale si ndio tunayokataa kila siku???
Hii inamaanisha mtu kama Mwakyembe angekuwa CHADEMA angekuwa kashafukuzwa kwa kuyumbisha serikali ya chama chake, hata kama ni kwa maslahi ya taifa!!!
 
''TBC TAIFA Television na Redio ni hatari kwa taifa,kwa kubobea kupotosha umma juu ya matukio mengi.Hivyo CHADEMA Inatangaza mgogoro na TBC na inaelekeza na kuomba wanachama ,wapenzi,na wananchi wote wapendao ukweli na haki,kuisusia TBC''

TBC ni rasilimali ya watanzania wote. Kama utendaji wake hauridhishi inapaswa kuishinikiza serikali kufanya marekebisho kama jinsi inavyofanywa kwenye taasisi nyingine. Kuhujumu TBC ni kuhujumu uchumi wa taifa.
TBC imeajiri watanzania wangapi? Ikifa hao watanzania waishi vipi?
TBC imegharimu kiasi gani cha kodi za wananchi? Ikifa hizo kodi zimepotea.
TBC inachangia pato la taifa.
TBC pia hutoa elimu. Ikumbukwe kuwa TBC haijaspecialize kwenye habari za siasa tu. Hii tabia ya kuona siasa ni muhimu kuliko mambo mengine yote haifai.

CHADEMA mlianza kususia Bunge, sasa TBC, mmeshatangaza ugomvi na usalama wa Taifa, ugomvi na jeshi la wananchi. Hizi zote ni dalili za kutokuwa na nia njema na nchi yetu na kukosa uzalendo...
 
waje na redio na gazeti lao la CHADEMA. Hyo ndo njia mbadala.
 
Hivi bado kuna watu wanaangalia TBC na kusoma gazeti la Uhuru!! Mi nilishaacha huku siku nyingi. Na Clouds nasikiliza Jumapili asubuhi tu kwa sababu ya Kibonde
 
Naupongeza sana msimamo wa kuendelea kuchukua maamuzi magumu unao fanywa na Chadema! Ni chama ambacho daima kinaonyesha njia na wengine wanajaribu kufuata na hata kushindwa.

Ushauri wangu.

Chadema isinge ishia kutoa tamko tu kwa ajili ya kutokuwa na imani na tume ya Nchimbi au kumuomba raisi kuunda mahakama maalumu ya kuchunguza vifo, hii ni kwa sababu si mara ya kwanza na serikali haijawahi kuunda mahakama hiyo na watu wameendelea kufa (Siombei) huenda pia wakauwa tena.

Ilitakiwa moja ya azimio la kamati kuu ni kuunda tume huru ya kuchunguza vifo kwa kuhusisha wanaharakati wa haki za binadamu na wabobezi wa maswala la kiuchunguzi, hao wote wangefanya kazi hiyo kwa ajira maalumu ya kipindi cha muda fulani kwenye mikoa yote ambayo mauwaji yametokea hata kuanzia mwaka 2001 mpaka sasa. Ili kuwa na profile ya kiuchunguzi ya vifo vyote.

Wapenda haki kama sisi tungewekewa akaunti maalumu kwa ajili ya kuchangia fedha kuwezesha kamati teule hiyo.

Kuhusu TBC1 na TBC taifa.

Kamati kuu ingekuwa bold tu kusema inawakataza kutangaza habari zozote za Chadema, mbaya au nzuri na kuweka zuio hilo kisheria kama zipo sheria zinazo ruhusu hivyo japo natambua haki ya kikatiba ya kutoa na kutafuta habari (Ibara ya 18). Lakini wakati huohuo kueleza mpango mkakati wa kuwa na TV station pamoja na redio ya chama ambayo itakuwa inatoa habari za kweli tofauti na zile za Tbccm.

Hitimisho.
Yoyote mwenye akili timamu anaweza kuuona umakini wa chama kupitia maazimio hayo, maana yamekata mpaka kiu ya wachukia usaliti.

Sent from BlackBerry 8520 authorized by JamiiForums.
 
Hivi bado kuna watu wanaangalia TBC na kusoma gazeti la Uhuru!! Mi nilishaacha huku siku nyingi. Na Clouds nasikiliza Jumapili asubuhi tu kwa sababu ya Kibonde

mi napenda sana TBC na clouds ndo usiseme nyinyi chadema mna matatizo
 
Hivi Chadema wanaisusiaje TBC sasa kwa mfano? Kinacholeta mantiki kwangu ni TBC kuisusia Chadema kwa kutotangaza habari zake na siyo kinyume chake.

ilitangaza wakristo ni wengi kuliko waislamu shenz yake data walipata wapi ilitaka kuwachonganisha kama sms za uchochezi 2010
 
wenye digital receivers (decoder au receiver za dish za kawaida) mni-PM niwaelekeze jinsi ya ku-delete channel maana nilijifunzia wakati nai-delete TBC1 na TBC2 kutoka kwenye Startimes Decoder na receiver ya dish sebuleni kwangu kama miezi 8 iliyopita.

weka hapahapa, utawa PM wangap?
 

  1. ''Operesheni MOVEMENT FOR CHANGE M4C,Inaendelea kadiri ya ratiba ilivyopangwa katika utaratibu uleule uliokuwepo awali.Inarejea Iringa Siku si nyingi.Na kamati kuu Imetoa msisitizo MAALUM kwa jimbo mojawapo singida,ambapo wamesema watatumia helcopita,magari,pikipiki na baiskeli na miguu,na badala ya kupita vijijini kama majimbo mengine,Chadema wanasema kwa sababu maalum katika jimbo hilo watapita kitongojikwa kitongoji,ili kufunza adabu baadhi ya viongozi (msisitizo ni wa msoma MAAZIMIO.jimbo hili laweza kuwa la Mwigullu Mchemba,kadiri ya wanahabari waliokuwepo''.


Nipo Singida tangu jana.Leo,majira ya mchana, katika pita pita zangu mitaani, nilikutana na dogo mmoja maeneo ya Kanisa la Roman Catholic,akiwa amevaa kofia yenye rangi ya bendera ya CHADEMA.Baada ya kumwita,na kuanzisha mazungumzo,nilimuuliza ikiwa yeye ni mwana - CHADEMA ama la.Baada ya kusita kidogo-bila shaka kwa sababu za kiusalama-na baada ya kumweleza kuwa aondoe shaka kwa kuwa nami ni mwana CHADEMA, akakiri kuwa ni kweli yeye ni mwanachama wa CHADEMA na kwa msisitizo zaidi alitoa kadi yake mfukoni na kunionyesha kwa kujiamini kabisa.Akanieleza kuwa anatoka jimbo la Iramba Magharibi na kuwa huko atokako vijana wamehamasika na wako tayari kwa maabadiliko.Akinieleza''Kaka ,ikiwa wewe ni kiongozi katika chama zungumza na viongozi wenzako ili mje Iramba kufanya mikutano mtuongezee hamasa maana kule kuna mwamko mkubwa na CCM ina wakati mgumu''
Nikiisha kumfahamisha kuwa mimi si kiongozi katika chama na kwamba ni nilikuwa napita tu hapa mjini nilimsihi awe na subira maana M4C ipo karibu na kuwa tungepata jawabu la uhakika baada ya kupata maazimio ya Kamati Kuu.
Sina shaka kuwa dogo mwana-CHADEMA amefurahia sana azimio namba 8.

 
Hili ni tamko la 70 toka mwaka uanze lakini hakuna hata moja linalofanyiwa kazi na serikali imekuwa kama ngonjera, sasa mtajuaje kama wafuasi wa Chadema hawatazami TBC 1.
 
saafii sana na hongera kamati kuu kwa maamuzi yaliyofikiwa!sasa mapambano yaendelee kwa nguvu zaid!GOD bless Africa and Tanzania as well..!
 
The same old story.

Ninawaasa wananchi masikini kutokuwa mbele kwenye hayo maandamano ili na wao viongozi wapeleke misiba kwenye nyumba zao. Iweje wajiite wapigania ukombozi lakini wanaouwawa na kujeruhiwa ni masikini tu na sio wao viongozi?
Ndugu "Tume ya Katiba", kwani PoliceCCM (JMM - Jeshi la Mauaji la Magamba) huwa hawawaoni viongozi wa CDM? Si wangewafyatulia risasi siku moja?
Yaani hata mkipindisha mada UKWELI NI HUU: "Either kwa kutumwa au kwa kujipendekeza wenyewe, Police uua kwa niaba ya CCM"
 
too light tamko... a sign of fatigue and frustration, no mention of many critical matters

anyway, safari bado ndefu
 
Back
Top Bottom