Maazimio ya Kamati Kuu ya CHADEMA Sept 10, 2012

Maazimio ya Kamati Kuu ya CHADEMA Sept 10, 2012

[h=3]
[/h]

1.Uwajibikaji wa kisiasa wa viongozi wa serikali na idara zake.,Waziri Emmanuel Nchimbi,IGP Mwema,Paul Chagonja,RPC Morogoro na Kamanda wa FFU,na RPC IRINGA na Kamanda wa FFU wajiuzulu na au wafukuzwe kazi

2.RPC Morogoro na Iringa,makamanda wa FFU Morogoro na Iringa,na maaskari waliouwa wakamatwe mara moja na kufunguliwa mashitaka

3.Rais aunde tume huru ya uchunguzi wa vifo tata katika matukio ya kisiasa.1.ARUSHA vifo 3.IGUNGA,vifo vingi havijulikani bado,3.ARUMERU MASHARIKI,vifo 5, 4.SINGIDA kifo 1, MOROGORO na IRINGA
chadema haitatambua wala kushirikiana na kamati batili ya NCHIMBI.

4.Msajili wa vyama vya siasa John Tendwa ni mtu hatari kwa taifa kwa kauli tata anazozitoa.anashirikiana na au anajipendekeza kwa CCM na Serikali yake.CHADEMA tangu sasa haitafanya kazi na Tendwa wala kufanya mawasiliano naye ya kiofisi.Labda kama atagundua makosa yake na kuomba msamaha,chadema itatafakari namna ya kufanya naye kazi tena.

5.TBC TAIFA Television na Redio ni hatari kwa taifa,kwa kubobea kupotosha umma juu ya matukio mengi.Hivyo CHADEMA Inatangaza mgogoro na TBC na inaelekeza na kuomba wanachama ,wapenzi,na wananchi wote wapendao ukweli na haki,kuisusia TBC

6.Jeshi la Polisi lijue kuwa Maandamano ndiyo siasa yenyewe na mikutano ya hadhara ni lazima kwa mawasiliano ya umma na siasa.kuzuia vitu hivyo ni kunyima wananchi haki yao ya kikatiba ya uhuru wa kukusanyika na kutoa maoni,pia kupata habari na taarifa

7.Operesheni MOVEMENT FOR CHANGE M4C,Inaendelea kadiri ya ratiba ilivyopangwa katika utaratibu uleule uliokuwepo awali.Inarejea Iringa Siku si nyingi.Na kamati kuu Imetoa msisitizo MAALUM kwa jimbo mojawapo singida,ambapo wamesema watatumia helcopita,magari,pikipiki na baiskeli na miguu,na badala ya kupita vijijini kama majimbo mengine,Chadema wanasema kwa sababu maalum katika jimbo hilo watapita kitongojikwa kitongoji,ili kufunza adabu baadhi ya viongozi (msisitizo ni wa msoma MAAZIMIO.jimbo hili laweza kuwa la Mwigullu Mchemba,kadiri ya wanahabari waliokuwepo)

8.Kutokana na mgogoro wa muda mrefu mkoani mwanza uliosababisha meye wa chadema kuvuliwa umeya kinyume na utaratibu na kwa njama za CCM na Serikali,na bahati mbaya sana kwa kushirikisha madiwani wa CHADEMA,KAMATI KUU imewavua UANACHAMA madiwani wake wawli 1 ADAMU CHAGULANI wa kata ya IGOMA na HENRY MATATA wa KITANGIRI, PIA uongozi wote wa CHADEMA mkoa wa mwanza Umevunjwa.

Imesomwa na Mwenyekiti CHADEMA Taifa
 
[h=3]Maazimio Ya Kamati Kuu Ya Chadema[/h]

Mingoi
''We ulitegemea nini na umeshasema ulimkuta kanisani tena Roman catholic''

Wewe ni mwepesi sana sana.
Dalili ya mtu mwepesi ni kuogopa/kushindwa kuandika aya mbili ama tatu.Uwezo wako ni sentensi moja tu.Halafu umejibanza katika kundi la ''Great Thinkers''!!
Huwezi kuwa mtu makini kwa visentesi vya reja reja.
Any way.Ningekuwa nimekutana na dogo maeneo ya msikitini ningesema na hata kama ingekuwa maeneo ya Polisi ningesema.
Pomoja na ukweli kuwa mimi si mwandishi wa habari nilikuwa nakamilisha zile ''who'',''where'',''why'',''how'' and ''what''.
 
The same old story.

Ninawaasa wananchi masikini kutokuwa mbele kwenye hayo maandamano ili na wao viongozi wapeleke misiba kwenye nyumba zao. Iweje wajiite wapigania ukombozi lakini wanaouwawa na kujeruhiwa ni masikini tu na sio wao viongozi?

Wewe unaishi Tanzania gani? Waliopigwa mapanga kwenye uchaguzi mdogo Mwanza mbona walikua ni wabunge Kiwia na Machemuli. Hatudanganyiki wala hatuogopi mpaka kieleweke.
 
Huyu mzee **** sana, watu wa mwanza wawachague kina Adam chagulani na Henri Matata.
Yeye akae Dar na kamati yake wawatoe!
Naamini sasa Yale maneno ya Adam kwa dr.slaa
"uongozi wa chadema wa ngazi ya juu una uvivu wa kufikiri"
 
Mimi ni mkazi wa Igoma niliepiga kura kwa chagulani kwa dhati kabisa kwa kutuwakilisha Kama ambavyo amrtuwakilisha.
Lakini nasangaaa hawa wenye Chama waliokaa daresalaam wamechukuwa fursa ya Kuona sisi ni wajinga kwa kumchagua Adam na wao ndio wanajua sana na wanamjua zaidi ya sisi tunao ishi na kufanya harakati zetu za kimaendeleo hapa katani na bwana chagulani.
Kingine cha kushangaza watu wengine ambao si wakazi wa kata yetu wana support hili.
Tuko na Adam chagulani Kuanzia mwanzo mpaka Mwisho.
Hatuwezi kupangiwa au kuendeshwa na watu flani flan ambao wako dareslam na wakae watupangie sisi chakufanya.
Huu ni utumwa
 
Sisi wakazi wa Igoma mwanza, tulichagua Adam chagulani kuwa ndo mwakilishi wetu katika ngazi ya kata. Kwa juhudi zake,fikra, ushirikiano pamoja na wananchi, kwa uwazi na kutomuogopa wala kujipendekeza kwa Mtu na kwa ujasiri wa kukemea ovu kwa Mtu yeyote.
Hatukuchagua tuongozwe na Chama Bali tulichagua Mtu si Chama.
Kwa hiyo sisi wakazi wa Igoma tutaendelea kuwakilishwa na Adam chagulani tu mpaka hapo mambo yatakapobadilika kwa Adam kukataa maswala ya udiwani kwa hii misimu 2 inayokuja mbeleni kwetu mungu akipenda
 
Huyu mzee **** sana, watu wa mwanza wawachague kina Adam chagulani na Henri Matata.
Yeye akae Dar na kamati yake wawatoe!
Naamini sasa Yale maneno ya Adam kwa dr.slaa
"uongozi wa chadema wa ngazi ya juu una uvivu wa kufikiri"

Uvivu wa kufikiri una maana nyingi sana, hata wewe kaa kwanza ufikiri kwa muda kisha urudi unaweza kuandika tofauti.
 
ushauri.......ikiwezekana tuwahamishie ze comedy kwenye kituo kingione cha tv ili nivunje uhusiano na tbc kabisaaaaaaaaaaaaaaaaa
hao comedy wana umuhimu gani katika harakati za kuleta mabadiliko kaka
 
Mimi ni mkazi wa Igoma niliepiga kura kwa chagulani kwa dhati kabisa kwa kutuwakilisha Kama ambavyo amrtuwakilisha.
Lakini nasangaaa hawa wenye Chama waliokaa daresalaam wamechukuwa fursa ya Kuona sisi ni wajinga kwa kumchagua Adam na wao ndio wanajua sana na wanamjua zaidi ya sisi tunao ishi na kufanya harakati zetu za kimaendeleo hapa katani na bwana chagulani.
Kingine cha kushangaza watu wengine ambao si wakazi wa kata yetu wana support hili.
Tuko na Adam chagulani Kuanzia mwanzo mpaka Mwisho.
Hatuwezi kupangiwa au kuendeshwa na watu flani flan ambao wako dareslam na wakae watupangie sisi chakufanya.
Huu ni utumwa
hoja ya mtu kuwa juu ya chama hapa ndipo tunashindwa kuielewa
 
Operesheni MOVEMENT FOR CHANGE M4C,Inaendelea kadiri ya ratiba ilivyopangwa katika utaratibu uleule uliokuwepo awali.Inarejea Iringa Siku si nyingi.Na kamati kuu Imetoa msisitizo MAALUM kwa jimbo mojawapo singida,ambapo wamesema watatumia helcopita,magari,pikipiki na baiskeli na miguu,na badala ya kupita vijijini kama majimbo mengine,Chadema wanasema kwa sababu maalum katika jimbo hilo watapita kitongojikwa kitongoji,ili kufunza adabu baadhi ya viongozi (msisitizo ni wa msoma MAAZIMIO.jimbo hili laweza kuwa la Mwigullu Mchemba,kadiri ya wanahabari waliokuwepo)
nimeamini mwigulu ni jeshi ala mtu mmoja

Sawa naunga mkono 100% wakamatwe na wengine wafukuzwe kazi. JE?
1. Ni nani huyo atakayewakamata?
2. Ni nani huyo atakayewafukuza kazi?
3. Iwapo hawatakamatwa na wala kufukuzwa kazi CDM itafanya nini? Wasiwasi wangu ni kwamba CDM ikaishia kubwekabweka kama Mbwa muoga na mwisho na mwisho ikaishia kutingisha mkia?
 
Uvivu wa kufikiri una maana nyingi sana, hata wewe kaa kwanza ufikiri kwa muda kisha urudi unaweza kuandika tofauti.

Mimi nilianza kufikiri mwanzo kabisa wakati napiga kura yangu ya kumchagua Adam kuwa mwakilishi wangu katani.
Huyu Babu wa chadema ametu cost sisi wakazi wa kata hii na ametudharau maamuzi yetu na mapendekezo yetu ya Adam kuwa mwakilishi wetu.
 
Sio neno, kakae ufikiri kwa muda. Hapa umejibu haraka sana, hujatafakari mambo mengi bado. Nina imani kabisa ukifikiria kwa upana wake utapata jibu zuri sana tena utafanya maamuzi mazuri sana.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimepitisha maazimio saba, mojawapo likitaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali (IGP), Said Mwema, na Mkuu wa Operesheni na Mafunzo wa Polisi, Kamishna Paul Chagonja, kujiuzulu nafasi zao mara moja kutokana na mauaji ya raia katika mikoa ya Morogoro na Iringa kutokea mikononi mwa jeshi hilo, ambalo lipo chini ya usimamizi wao.

Kimesema iwapo waziri huyo pamoja na viongozi hao wa jeshi hilo watashindwa kuwajibika, basi Rais Jakaya Kikwete, awafukuze kazi mara moja.

Wengine ambao wametakiwa na chama hicho kujiuzulu mara moja kwa tuhuma hizo, ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda na Mkuu wa askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Mkoa wa Morogoro.

Pia kimetaka askari waliosababisha mauaji ya raia wasio na hatia katika mikoa hiyo wakamatwe na kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya mauaji.

Chama hicho pia kimeazimia kutoshiriki shughuli zozote zitakazosimamiwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, hadi atakapoondolewa katika nafasi yake na kuteuliwa msajili mwingine.

Maazimio hayo yalipitishwa na Kamati Kuu ya Chadema katika kikao chake maalum kilichofanyika jijini Dar es Salaam juzi, ambacho pamoja na mambo mengine, kilijadili hali ya siasa nchini kufuatia mfululizo wa mauaji yanayofanywa na jeshi hilo katika shughuli za chama hicho.

Pia kilijadili mipango ya baadhi ya viongozi wa serikali ya kudhibiti Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) kwa mbinu haramu.

JK AANDIKIWA BARUA

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akisoma maazimio hayo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, alisema Kamati Kuu imeamua kumuandikia barua Rais Kikwete kumtaka achukue hatua za utekelezaji kwa mujibu wa mamlaka yake na kwa mujibu wa Katiba ya nchi.

“Iwapo serikali haitazingatia, Chadema itawaongoza wananchi kwa njia za kidemokrasia ikiwamo maandamano ya amani kushinikiza hatua za haraka kuchukuliwa kwa maslahi ya Taifa,” alisema Mbowe na kuongeza:

“Tutaitisha maandamano ambayo hayajawahi kutokea katika nchi hii. Tutatangaza tutakapokuwa tayari. Haki ya Mungu hatutanii.”
Alisema anashangaa kuona Nchimbi akishangaa kuona Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, akiwa huru, wakati waziri huyo, IGP Mwema, Chagonja, makamanda hao wa polisi, wakuu hao wa FFU pamoja na askari hao ndiyo wanaostahili kuwajibika kwa kuwa ushahidi kuhusiana na tuhuma dhidi yao uko wazi.

Mbowe alisema kwa maslahi mapana ya Taifa, Rais Kikwete anapaswa kuunda tume huru ya kiuchunguzi ya kimahakama kuchunguza vifo vilivyotokea katika mazingira tata katika mikoa ya Arusha (Arusha Mjini na Arumeru), Singida, Morogoro na Iringa, kama ambavyo Chadema wamekuwa wakisisitiza siku za nyuma.

Alisema Chadema haiitambui kamati iliyoundwa na Waziri Nchimbi kuchunguza mauaji ya mwandishi wa habari, Daudi Mwangosi, kwa kuwa haina msingi wa kisheria na kwa hiyo, hawatatoa ushirikiano wowote kwa kamati hiyo.

TENDWA KUSUSIWA

Kamati Kuu pia imemtangaza Tendwa kuwa ni adui wa demokrasia na hafai kuwa katika nafasi aliyonayo, kutokana na utendaji dhaifu, unaoegemea upande mmoja na wa kipropaganda unaoonyeshwa naye.

“Kamati Kuu imeazimia kuwa pamoja na kuendelea kuheshimu sheria ya vyama vya siasa, Chadema haitashiriki shughuli zozote zitakazosimamiwa na John Tendwa hadi hapo atakapoondolewa katika nafasi yake na kuteuliwa msajili mwingine,” alisema Mbowe.

Alisema Tendwa amekuwa na kauli tata kuhusu vyama vya siasa nchini, ambazo haijulikani kama anashinikizwa au anajipendekeza.

“Huyu ni mtu hatari. Ajiuzulu au awajibishwe. Hatutafanya kazi yoyote na John Tendwa. Hatutachukua amri ya John Tendwa.
Tutaheshimu sheria. Tutakuwa tayari kuchukua maelekezo ya karani kuliko ya John Tendwa.

Akituita hatumsikilizi hadi atakapoomba radhi. Vinginevyo hatutakwenda kwenye mikutano yake. Na ajaribu kufuta Chadema. Siyo Tendwa hata Kikwete jaribu kufuta Chadema,” alisema Mbowe.

Alisema pia Kamati Kuu inalihimiza Jeshi la Polisi kusimamia, kufuata, kuheshimu na kusimamia kwa haki sheria zinazoongoza shughuli za vyama vya siasa, ikiwamo kifungu cha 11 cha Sheria ya Vyama vya Siasa inayotoa fursa kamili kwa vyama vya siasa kufanya mikutano na maandamano kama sehemu ya kazi ya uenezi ya vyama hivyo.

Mbowe alisema Kamati Kuu imeazimia pia kuwa Operesheni ya M4C iendelee na kazi zake kwa kufuata kikamilifu ratiba iliyopitishwa na Baraza Kuu na Kamati Kuu katika vikao vya awali, ikiwa ni sehemu ya kutimiza dhima yake ya kuleta uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganaizesheni thabiti kwa maendeleo endelevu ya Tanzania.

YAVUNJA UONGOZI, YATIMUA MADIWANI

Alisema pia Kamati Kuu imepokea taarifa ya kamati iliyoundwa na Katibu Mkuu wa chama kuchunguza chanzo cha mgogoro wa chama mkoani Mwanza na imeamua kuwavua uanachama madiwani wawili; Adam Chagulani (Kata ya Igoma) na Henry Matata (Kata ya Kitangiri) kwa kukiuka kanuni na maadili ya chama ikihusisha tuhuma za ufisadi.

Mbowe alisema Chadema itakuwa tayari kuwajibika kwa lolote litakalotokea huko mbele kufuatia uamuzi wao dhidi ya madiwani hao.
Kamati Kuu pia imeuvunja uongozi wa chama mkoa huo kutokana na uzembe uliofanyika katika eneo lake la kazi na kwamba, utaratibu wa kuweka uongozi mpya utafanyika.

Alisema ‘madiwani’ hao walishapewa onyo na karipio, hivyo walikuwa chini ya uangalizi na kwamba, kabla hatua ya juzi ya Kamati Kuu walipewa pia nafasi ya kujieleza.

Mbowe alisema uamuzi huo wa Kamati Kuu ni onyo kwa viongozi wote wa Chadema kwamba, chama hakitaweza kumvumilia mtu yeyote anayeonekana kukwamisha tumaini la Watanzania kufanikisha ukombozi wa mabadiliko ya kimfumo na kiutawala kwa kukikabidhi chama hicho madaraka mwaka 2015.

CHANZO: NIPASHE

Good decisions,however I have some recommendation
Kuhusu Singida naamini ni kule kwa Mwigulu, waende na zile video alizokuwa akimwaga matusi,,,am happy kwamba wataenda kitongoji kwa kitongoji, wasisahau kufanya follow up ya mara kwa mara katika jimbo hili ili kumtia adabu huyu bwana mdogo.

Kuhusu TBC, kwa sababu imesusiwa kwa kufuata vikao halali, nashauri M4C inapoendelea wawatangazie wananchi kutoiangalia wala kusikiliza Televisheni hiyo, vilevile radio yao, maana nayo kama ingekuwa ni mtu tungeita FISADI,,,,mpaka watakapoona na kukiri kosa lao ikiwa ni pamoja na kujirekebisha;

Kuhusu Chagulani,ni maamuzi yenye afya kichama,,,shida ya huyu bwana amakuwa OVER AMBITIOUS, so wakati mwingine giza halioni yeye huona mwanga tu,,,,ana roho ya kimapinduzi ila HEKIMA, BUSARA NA UVUMILIVU vimemkosa,,,,madhara aliyokiletea chama hasa baada ya kuitisha saini ili kumng'oa meya ambaye anajua fika ni wa CHADEMA ni makubwa sana, sana...

Kuhusu kuvunja uongozi wote wa Mkoa wa Mwanza, it has come at a right time maana CCM mtaji wao mkubwa ni Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla, CCM walishaanza kuwaweka mfukoni hawa jamaa ili kukidhoofisha Chama. Infact shida kubwa ilikuwa ni Mushumbusi....kiukweli alishaanza kupoteza mvuto wa CHADEMA Kanda ya Ziwa.....

Kuhusu Msajili wa Vyama vya Siasa, well done Kamati Kuu....The man is not RATIONAL AND HE IS VERY INCONSISTENT tena anatakiwa kushitakiwa soon,,,,aliwahi kusema atavifuta vyama visivyokuwa ACTIVE na sasa anasema atavifuta vyama ambavyo viko ACTIVE na hasa anakilenga CHADEMA

Generally, maamuzi nimeyakubali na kuyaunga mkono....UKOMBOZI SI LELEMAMA

LONG LIVE CHADEMA, LONG LIVE MAKAMANDA
 
I love CDM with all my heart!!! Sasa ni muafaka nijiandikishe maana nilishakata tamaa na siasa za Tanzania na kubaki mshabiki tu. Ntashabikia mpaka lini? Bravo M4C, long live CDM.
 
Back
Top Bottom