Maazimio mangapi ya mwaka mpya umeshayavunja?

Execute

JF-Expert Member
Sep 21, 2022
3,000
7,285
Kuna maazimio mazito niliyaweka lakini wapi nishapoteza mengi tu. Nilisema sitakunywa soda na nimeshakunywa tano, nilisema sitatumia sukari na nishainywa.

Nilisema sigusi nje tayari kuna mmoja alijileta. Yaani tafrani tupu.
 
Nashukuru Mungu sijafanya zinaa toka mwaka uanze. Mungu ajaalie niendelee hivyo hivyo.

Nililipia gym ili nianze tizi la kupungua na kuahidi kuanza kula kiafya.
Gym nimeenda siku moja tu, tarehe moja January. Tumbo limejaa ndi hapa nilipo kwa ubwabwa, maharage ya nazi, kuku wa kukaanga na lita moja ya juisi ya miwa.
Mungu nisaidie.
 
Nimeazimiq kuanzia mwaka huu kuishi miaka 120 nikiwa na nguvu. Sasa niko kwenye reverse process ya kula anti aging foods kioaumbele kikiwa ni matunda nafaka na mbogamboga.
Na nasoma lifestyle ya maeneo ambayo watu wanatoboa 100 bila nguvu huku nikiwakimbia watu hasi. Hadi sasa naenda vizuri ila kuna misimamo niliyojiwekea mingine bado haijastabikize najikuta naanguka ila sirudi nyumq. Kwa sasa nimeweka plan ya miaka 25 ya kwanza.
 
Mimi huu mwaka niliamua kabisa kua mwaka wangu utaanza tarehe 1 mwezi wa nne.
Kwaio tukutane huko.
 
Kwa ufupi ni kuwa wote mlioshindwa kusimamia malengo yenu ni mnakosa self-discipline.
 
Back
Top Bottom