Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,277
- 105,480
Maaskofu wana lao jingine, hii issue ya impartiality haina nguvu, kwa sababu mtu unaweza kuwa impartial na ukaenda kushiriki katika vikao vya wagombea wote. Kwani watu wote wanaoenda katika mikutano ya Kikwete ni CCM ? Wote watampigia kura? Wote wanaoenda kwenye mikutano ya Slaa ni CHADEMA ? Wote watampigia kura ? Hakuna watu wanaokwenda kwenye mikutano yote ?
Swala la futari, "kufuturu" na mtu haina maana ni lazima uwe umefunga, mbona watanzania tulioishi kwa ujirani na indeed undugu na kuoleana kati ya wakristo na waislam tunaona kila siku waislam wanaalika wakristo katika futari ? Mbona tunajua kwamba ukarimu kwa waislam ni jambo la thawabu kama ulivyo kwa wakristo ?
Kwa hiyo, swala la impartiality halipo, wangempenda wangeweza kwenda na kusema wako open kwenda kwa mgombea yoyote.Kanisa halikatai mtu. Swala la kufuturu halipo, kufuturu na mtu si lazima uwe muislam, na wala si lazima hata ufunge.
Sasa baada ya kuona kwamba hayo mawili si issues, tujiulize, kwa nini maaskofu wanakataa kukutana na Kikwete ?