Maaskofu wasusia mwaliko wa JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maaskofu wasusia mwaliko wa JK

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Luteni, Sep 4, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Sep 4, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Maaskofu wasusia mwaliko wa JK

  Saturday, 04 September 2010 21:33
  *Ni kushirikiana naye kula futari

  MAASKOFU wa makanisa ya Kikristo na wachungaji mkoani Mbeya walioalikwa kula futari (kufuturu) na Rais Jakaya Kikwete katika Ikulu ndogo alipokuwa katika ziara za kampeni hivi karibuni, walikataa kwa maelezo kuwa hawawezi kushiriki naye kwa kuwa ni mgombea wa urais.

  Habari ilizozipata Mwananchi Jumapili zinaeleza kuwa maaskofu na wachungaji hao walimgomea Rais Kikwete Septemba Mosi, mwaka huu wakati wa ziara yake mkoani Mbeya.
  Gazeti hili lilifanya juhudi kumtafuta Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba kutoa ufafanuzi wa taaarifa hizo jana.

  Hata hivyo alipopatikana kuzungumzia suala hilo Makamba alisema kwa kifupi, "hilo mimi sijui, silijui hilo".

  Kwa mujibu wa mwaliko huo ambao Mwananchi Jumapili iliuona, viongozi hao walitakiwa kufika Ikulu ndogo saa 12 jioni mjini Mbeya kufuturu pamoja na Rais Kikwete.

  Baada ya kupokea mwaliko huo, viongozi hao wa dini walisema kufuturu na Rais Kikwete wakati huu wa kampeni kungeweza kuvunja uaminifu wao kwa waumini kwa vile Kikwete ni sawa na wagombea wengine wa urais wanaostahili kupatiwa haki sawa.

  Habari hizo zimedai kuwa mbali ya maaskofu na wachungaji wa dini mbalimbali takribani 40 walioalikwa kula futari hiyo, mwaliko huo pia uliwahusu viongozi wa dini nyingine.

  Viongozi hao wa dini walisema mwaliko huo haukuwa na manufaa yoyote kwa viongozi wa kikiristo ambao hawakufunga hivyo wasingeweza kushiriki futari inayopaswa kuliwa na ndugu zao Waislamu waliofunga.

  Hii ni mara ya kwanza katika uchaguzi huu viongozi wa dini kutakaa mwaliko wa rais Kikwete.

  "Sisi maaskofu mkoani Mbeya ambao tulialikwa juzi (Jumanne) kwenye futari Ikulu ya Mbeya tumetafakari pamoja na wenzetu ambao hawakualikwa kuwa kitendo hiki ni rushwa ya chakula".

  "Tunakilaani vikali kitendo hiki tumejiuliza kwa nini tualikwe kwa futuru sisi ambao hatuko kwenye mfungo? Tena tumechukizwa sana na mgombea, kufanyiwa zindiko uwanjani na machifu wakati amefunga," ilieleza sehemu ya waraka wa maaskofu hao kwa Mwananchi Jumapili.

  Akiwa katika Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya wazee wa kimila (machifu) wa Usafwa mkoani humo walimvisha Kikwete mgolole, kumpa kiti cha kichifu pamoja na mkuki kama ishara ya kumkubali na kuahidi kuwa wananchi wote wa Mbeya watampigia kura Kikwete.

  Mmoja wa Maaskofu aliyepata nafasi ya kuzungumza na Mwananchi Jumapili alisema wameugomea mwaliko huo na kuufananisha na rushwa akieleza kuwa wao hawakupaswa kualikwa kipindi hiki ambacho jamii nzima ya watanzania inawatazama viongozi wa dini na kutaka kujua wameegemea upande upi.

  Askofu huyo ambaye aliomba jina lake lisitajwe kwa kuwa si msemaji wa umoja wao, alisema ni vyema viongozi wa madhehebu ya dini wakawa makini katika kipindi hiki cha kampeni.

  Kwa mujibu wa mwaliko huo uliowataka waalikwa wote kuwa nadhifu waalikwa hao walitakiwa kufikisha jibu kwa mpambe wa rais Ikulu iwapo watahudhuria au la.

  Askofu wa Kanisa la Pentekoste Evangelisti, Zebadia Mwanyerere Mwakatage alipohojiwa alisema kuwa hakupata mwaliko huo, lakini akasema kwamba hata angeupata asingekwenda kwa kuwa kitendo cha kualikwa na rais akiwa mgombea hakikustahili.

  Mwakatage alisema ni makosa viongozi wa dini kushiriki kwenye mialiko ya wagombea uongozi na kwamba, Kikwete anatumia kofia yake akijua kuwa yeye ni mgombea sawa na wengine hali ambayo askofu huyo alisema ingempa shida iwapo angehudhuria.

  Mwenyekiti wa Umoja wa Wakristo Mkoa wa Mbeya, Askofu John Mwela wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Nyanda za Juu Kusini alisema anaungana na msimamo wa maaskofu wenzake na wachungaji waliokataa kuitikia mwaliko huo kwa kuwa kwa kufanya hivyo wangekuwa wanapingana na msimamo walionao wa kutompendelea mgombea yoyote.

  Askofu Mwela alisema alipatiwa kadi ya mwaliko iliyochelewa kumfikia na kwamba hata angeipata mapema asingeweza kwenda kwa kuwa hakufunga Ramadhani na kwamba, kuhudhuria hafla hiyo ingempa shida kwa waumini wake kwa vile hatakiwi kushabikia upande wowote wa siasa.

  “Naunga mkono maamuzi ya wenzangu waliokataa kwenda Ikulu, kama waliliona hilo ni vyema tukawa na msimamo, tatizo huyu ni mgombea sawa na wengine na isitoshe ingekuwa tumealikwa kwenye dhifa hapo tungeenda kula chakula sio kufuturu hatukufunga sasa ningeenda kufanya nini huko,” alisisitiza Askofu Mwela.

  Kiongozi huyo wa madhehebu ya kikiristo Mkoa wa Mbeya aliwataka waumini wa madhehebu hayo kuwa makini kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi mkuu na kuwahimiza kuhudhuria kwenye mikutano ya vyama vyote kuwasikiliza wagombea ili kuchagua viongozi bora.

  Askofu wa Kanisa Katoliki, Evaristo Chengula alipotafutwa kutoa maoni yake kuhusu mwaliko huo wa Ikulu ilidaiwa kuwa amesafiri nje ya mkoa huo sambamba na maaskofu wengine Alinikisa Cheyo wa kanisa la Moraviani na Thomas Daminius Kongoro wa Pentekoste Assembless Of God(PAG) wote hawakuweza kupatikana kutoa maoni yao au kuthibitisha kama walikuwa miongoni mwa waalikwa.

  Umoja wa makanisa ya kikiristo unaunganisha madhehemu manne ya Jumuiya ya Kikiristo Tanzania(CCT), Makanisa ya Kikatoliki (TEC), Jumuiya ya Kipentekoste (PCT) na makanisa huru ambayo, Mwenyekiti wake ni Askofu Mwela wa Anglikani.
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Sep 4, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Inawezekana kwa sababu weshapata mgombea wao wanaemuunga mkono...labda...{haya ngumi zije sasa}
   
 3. P

  Paul S.S Verified User

  #3
  Sep 4, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  umezipata wapi hizo habari wewe
   
 4. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #4
  Sep 4, 2010
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Hata Mwananchi wameandika ila ukibonyeza link inaleta 404 error message.
   
 5. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #5
  Sep 4, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kila mahesabu JK anayopiga kura hazitoshi! kuchakachua itakuwa nooma! waislamu na wakristo matatani duh! sasa anataka kuomba nguvu ya makanisa? au ni nini haswa kilichomsibu private citzen to be bwana JK
   
 6. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #6
  Sep 4, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  awaalike maamuma wenzie watamsaidia
   
 7. terrell

  terrell Member

  #7
  Sep 4, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmmh! Jamaa anajaribu kila njia aonekane ni mtiifu kaumia safari hii.
   
 8. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #8
  Sep 4, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Aliwaalika lini,
  wapi
  kwa ajili gani?
  source?
  (isije ikawa aliwaalika kwa futari au sala ya taraweh hao maaskofu)
  fanya homework yako vyema kabla hujapost shekhe.
   
 9. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #9
  Sep 4, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,953
  Likes Received: 1,509
  Trophy Points: 280
  Kwani hao maaskofu walifunga,kwanza hawajazoea kula futari wamezoea "mafufu"na imbalaga
   
 10. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #10
  Sep 5, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  hahaaa mkuu nenda kule darfu ukakutane na wale jamaa wenye imani kali, utawaweza lakini?
   
 11. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #11
  Sep 5, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,205
  Trophy Points: 280
  Siku ya kufa nyani miti yote inateleza, kwa waislamu bado ana deni wanamdai Mahakama ya Kadhi huku nako mambo ndiyo yameanza kuwa hivyo, TUCTA wamenuna uso wa mbuzi, afya nayo sisemi, mpinzani wake ndiyo anazidi kupiga za uso sijui masikini atakimbilia wapi yetu macho.
   
 12. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #12
  Sep 5, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  asianguke tu jukwaani
   
 13. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #13
  Sep 5, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera sana kwa Maaskofu.

  Gazeti hili lilifanya juhudi kumtafuta Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba kutoa ufafanuzi wa taaarifa hizo jana.

  Hata hivyo alipopatikana kuzungumzia suala hilo Makamba alisema kwa kifupi, "hilo mimi sijui, silijui hilo".

  Hii ni mara ya kwanza katika uchaguzi huu viongozi wa dini kutakaa mwaliko wa rais Kikwete.

  "Sisi maaskofu mkoani Mbeya ambao tulialikwa juzi (Jumanne) kwenye futari Ikulu ya Mbeya tumetafakari pamoja na wenzetu ambao hawakualikwa kuwa kitendo hiki ni rushwa ya chakula".

  "Tunakilaani vikali kitendo hiki tumejiuliza kwa nini tualikwe kwa futuru sisi ambao hatuko kwenye mfungo? Tena tumechukizwa sana na mgombea, kufanyiwa zindiko uwanjani na machifu wakati amefunga," ilieleza sehemu ya waraka wa maaskofu hao kwa Mwananchi Jumapili.
   
 14. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #14
  Sep 5, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Hivi mie ngoja niulize tangu lini Mkuu ameanza kufunga?
   
 15. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #15
  Sep 5, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  'Viongozi wa Dini' na CCM wote ni tabaka tawala tu, they care very little to what happens to the common mwananchi hawawezi kuwa na jipya..Nikionacho ni kuwa wanafanya sarakasi kipindi hiki katika kutafuta ushawishi ili waendeleze status quo baadaye..they are all manipulating witches.
   
 16. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #16
  Sep 5, 2010
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,656
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Na Mashekhe vis-a-vis CUF/Lipumba et. al. jee? Mbona Slaa hajafanya jitihada zozote za ku-patronize Maaskofu?
   
 17. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #17
  Sep 5, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Maaskofu wasusia mwaliko wa JK Saturday, 04 September 2010 21:33

  *Ni kushirikiana naye kula futari
  Mwandishi Maalum, Mbeya
  MAASKOFU wa makanisa ya Kikristo na wachungaji mkoani Mbeya walioalikwa kula futari (kufuturu) na Rais Jakaya Kikwete katika Ikulu ndogo alipokuwa katika ziara za kampeni hivi karibuni, walikataa kwa maelezo kuwa hawawezi kushiriki naye kwa kuwa ni mgombea wa urais.

  Habari ilizozipata Mwananchi Jumapili zinaeleza kuwa maaskofu na wachungaji hao walimgomea Rais Kikwete Septemba Mosi, mwaka huu wakati wa ziara yake mkoani Mbeya.
  Gazeti hili lilifanya juhudi kumtafuta Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba kutoa ufafanuzi wa taaarifa hizo jana.

  Hata hivyo alipopatikana kuzungumzia suala hilo Makamba alisema kwa kifupi, "hilo mimi sijui, silijui hilo".

  Kwa mujibu wa mwaliko huo ambao Mwananchi Jumapili iliuona, viongozi hao walitakiwa kufika Ikulu ndogo saa 12 jioni mjini Mbeya kufuturu pamoja na Rais Kikwete.

  Baada ya kupokea mwaliko huo, viongozi hao wa dini walisema kufuturu na Rais Kikwete wakati huu wa kampeni kungeweza kuvunja uaminifu wao kwa waumini kwa vile Kikwete ni sawa na wagombea wengine wa urais wanaostahili kupatiwa haki sawa.

  Habari hizo zimedai kuwa mbali ya maaskofu na wachungaji wa dini mbalimbali takribani 40 walioalikwa kula futari hiyo, mwaliko huo pia uliwahusu viongozi wa dini nyingine.

  Viongozi hao wa dini walisema mwaliko huo haukuwa na manufaa yoyote kwa viongozi wa kikiristo ambao hawakufunga hivyo wasingeweza kushiriki futari inayopaswa kuliwa na ndugu zao Waislamu waliofunga.

  Hii ni mara ya kwanza katika uchaguzi huu viongozi wa dini kutakaa mwaliko wa rais Kikwete.

  "Sisi maaskofu mkoani Mbeya ambao tulialikwa juzi (Jumanne) kwenye futari Ikulu ya Mbeya tumetafakari pamoja na wenzetu ambao hawakualikwa kuwa kitendo hiki ni rushwa ya chakula".

  "Tunakilaani vikali kitendo hiki tumejiuliza kwa nini tualikwe kwa futuru sisi ambao hatuko kwenye mfungo? Tena tumechukizwa sana na mgombea, kufanyiwa zindiko uwanjani na machifu wakati amefunga," ilieleza sehemu ya waraka wa maaskofu hao kwa Mwananchi Jumapili.

  Akiwa katika Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya wazee wa kimila (machifu) wa Usafwa mkoani humo walimvisha Kikwete mgolole, kumpa kiti cha kichifu pamoja na mkuki kama ishara ya kumkubali na kuahidi kuwa wananchi wote wa Mbeya watampigia kura Kikwete.

  Mmoja wa Maaskofu aliyepata nafasi ya kuzungumza na Mwananchi Jumapili alisema wameugomea mwaliko huo na kuufananisha na rushwa akieleza kuwa wao hawakupaswa kualikwa kipindi hiki ambacho jamii nzima ya watanzania inawatazama viongozi wa dini na kutaka kujua wameegemea upande upi.

  Askofu huyo ambaye aliomba jina lake lisitajwe kwa kuwa si msemaji wa umoja wao, alisema ni vyema viongozi wa madhehebu ya dini wakawa makini katika kipindi hiki cha kampeni.

  Kwa mujibu wa mwaliko huo uliowataka waalikwa wote kuwa nadhifu waalikwa hao walitakiwa kufikisha jibu kwa mpambe wa rais Ikulu iwapo watahudhuria au la.

  Askofu wa Kanisa la Pentekoste Evangelisti, Zebadia Mwanyerere Mwakatage alipohojiwa alisema kuwa hakupata mwaliko huo, lakini akasema kwamba hata angeupata asingekwenda kwa kuwa kitendo cha kualikwa na rais akiwa mgombea hakikustahili.

  Mwakatage alisema ni makosa viongozi wa dini kushiriki kwenye mialiko ya wagombea uongozi na kwamba, Kikwete anatumia kofia yake akijua kuwa yeye ni mgombea sawa na wengine hali ambayo askofu huyo alisema ingempa shida iwapo angehudhuria.

  Mwenyekiti wa Umoja wa Wakristo Mkoa wa Mbeya, Askofu John Mwela wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Nyanda za Juu Kusini alisema anaungana na msimamo wa maaskofu wenzake na wachungaji waliokataa kuitikia mwaliko huo kwa kuwa kwa kufanya hivyo wangekuwa wanapingana na msimamo walionao wa kutompendelea mgombea yoyote.

  Askofu Mwela alisema alipatiwa kadi ya mwaliko iliyochelewa kumfikia na kwamba hata angeipata mapema asingeweza kwenda kwa kuwa hakufunga Ramadhani na kwamba, kuhudhuria hafla hiyo ingempa shida kwa waumini wake kwa vile hatakiwi kushabikia upande wowote wa siasa.

  “Naunga mkono maamuzi ya wenzangu waliokataa kwenda Ikulu, kama waliliona hilo ni vyema tukawa na msimamo, tatizo huyu ni mgombea sawa na wengine na isitoshe ingekuwa tumealikwa kwenye dhifa hapo tungeenda kula chakula sio kufuturu hatukufunga sasa ningeenda kufanya nini huko,” alisisitiza Askofu Mwela.

  Kiongozi huyo wa madhehebu ya kikiristo Mkoa wa Mbeya aliwataka waumini wa madhehebu hayo kuwa makini kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi mkuu na kuwahimiza kuhudhuria kwenye mikutano ya vyama vyote kuwasikiliza wagombea ili kuchagua viongozi bora.

  Askofu wa Kanisa Katoliki, Evaristo Chengula alipotafutwa kutoa maoni yake kuhusu mwaliko huo wa Ikulu ilidaiwa kuwa amesafiri nje ya mkoa huo sambamba na maaskofu wengine Alinikisa Cheyo wa kanisa la Moraviani na Thomas Daminius Kongoro wa Pentekoste Assembless Of God(PAG) wote hawakuweza kupatikana kutoa maoni yao au kuthibitisha kama walikuwa miongoni mwa waalikwa.

  Umoja wa makanisa ya kikiristo unaunganisha madhehemu manne ya Jumuiya ya Kikiristo Tanzania(CCT), Makanisa ya Kikatoliki (TEC), Jumuiya ya Kipentekoste (PCT) na makanisa huru ambayo, Mwenyekiti wake ni Askofu Mwela wa Anglikani.

  Source: Maaskofu wasusia mwaliko wa JK
   
 18. K

  Keil JF-Expert Member

  #18
  Sep 5, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Uko sahihi kabisa mkuu, maana mambo yao wakati mwingine hayaeleweki. Wakati hawa wanasusa futari, mwenzao kule Tabora amewataka Prof. Lipumba na Dr. Slaa wasiwe wanataja jina la Kikwete kwenye mikutano yao ya kampeni. Sasa ninachojiuliza, kwani kutaja jina la Kikwete ni kosa?

  Ukitafakari kwa makini sababu ya Askofu huyo kutaka jina la Kikwete lisitajwe, unakuta anafanya damage control. Maana mtu mwingine ukimwambia serikali hii ina mapungufu haya na haya, hajui kwanza serikali ni nini na nani mwenye mamlaka ya mwisho kwenye serikali hiyo. Lakini ukitaja serikali ya Kikwete, ndipo wengine wanafunguka macho.
   
 19. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #19
  Sep 5, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  na commenta za wachangiaji huko kwenye gazeti ni hizi, inaonekana wakristo mwaka huu unataka kuufanya huu uchaguzi wa wakristo na waislam(ila nnaamini si wakristo wote wenye mawazo mgando kama haya)
  0 #7 msema Kweli 2010-09-05 07:04 kudhibitisha ninayoyasema juzi niliteka sms kutoka kwa maaskofu kwe waumin wao inasema hivi "SMS TOKA MEZA KUU; wapendwa katika bwanawakristo,m aaskofu wamepinga uchaguzi mkuu kufanyika jumapili,CHADEM A wametuunga mkono, hilo jambo la baraka na pia kura zetu hakuna kuipa CCM ya kikwete anaewaendekeza waislam wenzake kwa kuwapa vyeo, OIC na mahakama ya kadhi,Tukijipan ga tutaing'oa CCM kwani kura za waislam wenzake zimegawanyika CCM na CUF na wengine wanapinga kupiga kura hilo ni baraka kwetu, tuzidishe maombi kwa kristo mungu mkuu na mwokozi wetu ili Kikwete na waislam wenzake wazidi kugawanyika, mungu bariki wakristo mungu bariki tanzaia"
  Quote

  0 #6 msema Kweli 2010-09-05 06:56 KWELI SASA IMEFAHAMIKA WAZI KABISA KWAMBA MAASKOFU WANA MPANGO NA PADRI MWENZA SLAA, LAKIN NIWAFAHAMISHE KWAMBA MIPANGO YENU INAFAHAMIKA NA KAMPENI MNZAOPIGA MAKANISAN ZA KUMCHAGUA SLAA HAZITAFANIKIWA
  POLEN SANA MAASKOFU
  Quote

  0 #5 OMI 2010-09-05 06:32 sI WASEME TU HAO MAASKOFU KUWA WANAMUUNGA MKONO SLAA KWA KUWA NI ALIKUWA ASKOFU MWENZAO ALIESTAAFU SENIOR BEACHALAR ASIE OA MPKA HIILEO WASISINGIZIE BURE KAMA NI RUSHWA YA CHAKULA WANA LAO HAO MAASKOFU
  Quote

  0 #4 desire 2010-09-05 05:59 HONGERENI MAASKOFU,VIONGO ZI WA DINI KUTWA KUWA KWENYE MAGETI YA MAFISADI INAPUNGUZA HESHIMA YAO KWA WAUMINI,FUTARI NI FUTARI TU HATA UKIFUTURU MAGIMBI NYUMBANI KWAKO KULIKO KWENDA KUFUTURU IKULU NA WASHIRIKINA MAZINDIKO MCHANA MCHANA NDANI YA MCHANA WA RAMADHANI SUBHANALLAH YA RABBBI..MIE BINAFSI YANGU SIWEZI KUSWALISHWA MSIKITINI NA KIONGOZI ANAERAMBA RAMBA MIGUU YA WATAWALA KWA SABABU UKIWA KARIB NA WATAWALA WAKIKOSEA WATAONA AIBU KUWAKEMEA
  Quote

  +1 #3 Prince 2010-09-05 05:51 Mbona kama huelewi ndugu yangu,hao tayari wameshasema na kutoa msimamo wao ambao ni halali kwani sasa hivi Kikwete sio Rais ni mgombea wa URAIS hivyo hiyo ni Rushwa ya wazi,kikwete kuhudhulia sherehe za kikristo ni wajibu yeye kama mkuu wa nchi na kama amealikwa ila kwa wakatti huu naddhani walichofanya ni sawa,big uuuuuuuuuuuuuup maaskofumnajua kazi yenu
  Quote

  +1 #2 Ronald 2010-09-05 05:47 Yusufu, hiyo haikuwa sherehe ya Kiislam, ilikuwa ni kufuturu. Hawa maaskofu na wachungaji walishapata breakfast, lunch, na kahawa ya mchana alafu wanaitwa kufuturu kwani wamefunga? Msimamo wa maaskofu ni sahihi kwani kikwete ni mgombea kwa kipindi hiki na kuhudhuria mwaliko wake binafsi (siyo km rais) inaweza kuchukuliwa kuwa kanisa/misikiti inamu-endorse Kikwete.
  Quote

  -1 #1 yusuf 2010-09-05 05:13 Jee hizi ndizo sifa za Maaskofu? Hawataki maaskofu kuonesha kuwa wao hawana ubaguzi baina ya dini? Huko hawakuitwa kwaajili ya chakula kama wahisivyo kutokana na kauli zao. Ni wazi kuwa hapa pana chuki za dini zinazopaliliwa na hawa jamaa. Mbona Kikwete daima tunamuona akihudhuria mara nyingi akihudhuria matokeo ya sherehe za kikristo, au ndio mkuki kwa nguruwe?
  Quote
   
 20. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #20
  Sep 5, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  yeah inawezekana kabisa... hasa ukizingatia kwamba hata wewe huwezi kwenda kula kwa mtu anayekuchafua kila sekunde ya mungu aliyotupa!!! dhambi ya udini imekua kubwa sana tanzania na serikali hii imechangia sana
   
Loading...