Maaskofu wasusia mwaliko wa JK
Saturday, 04 September 2010 21:33
*Ni kushirikiana naye kula futari
"Tunakilaani vikali kitendo hiki tumejiuliza kwa nini tualikwe kwa futuru sisi ambao hatuko kwenye mfungo? Tena tumechukizwa sana na
mgombea, kufanyiwa zindiko uwanjani na machifu wakati amefunga," ilieleza sehemu ya waraka wa maaskofu hao kwa Mwananchi Jumapili.
Akiwa katika Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya wazee wa kimila (machifu) wa Usafwa mkoani humo walimvisha Kikwete mgolole, kumpa kiti cha kichifu pamoja na mkuki kama ishara ya kumkubali na kuahidi kuwa wananchi wote wa Mbeya watampigia kura Kikwete.