Eeh Bwana eeh!. Nimeamini msemo usemano huwezi kumlaani aliyebarikiwa.
Jana nilikuwa Mwanza. Nilishangaa sana kugundua nilichokigundua kuwa ni athari ya hotuba ya Dr. Slaa kwa Watanzania. Niliyoyaona na kuyasikia, yalinipa kukumbuka (KWA WALE WASOMAJI WA BIBLIA) habari za "NAMNA ADUI WA WATU WA MUNGU WALIVYOTUMIA NGUVU,FEDHA NA MAMLAKA KUTAFUTA WATU WA KUWALAANI WATU WA MUNGU LAKINI BADALA YA KUWALAANI, WALIWABARIKI NA KUWAGEUZIA LAANA HAO WALIOKUSUDIA LAANA KWA TAIFA LA MUNGU. NILIKUMBUKA HABARI ZA "PUNDA WA BALAMU".
Kila kwenye mkusanyiko niliokuwa nikikutana nao, nilikuta agenda kubwa ni hotuba ya Dr. Slaa. na la ajabu ni namna wakazi wengi wa jiji la Mwanza walivyokuwa wakijiapiza kwamba "CCM NI ILE ILE, MAGUFULI NI CHOKAA ILIYO JUU YA KABURI AMBALO NDANI YAKE KUNA MAITI ILIYOOZA".
kwa nyakati mbali mbali, katika makundi ya mazungumzo walihojiana na KUAFIKIANA KWAMBA HAKUNA LOLOTE JIPYA NA LA MAANA ALILOLIONGEA DR. SLAA ZAIDI YA YALE YALE YA MIAKA NENDA YANAYOFAHAMIKA AMBAYO KAMA ANGELIKUWA NA UCHUNGU WA TAIFA, ALITAKIWA YEYE NA MWAKYEMBE, WAPELEKE KESI HIYO MAHAKAMANI BADALA YA KULALAMA KWA WANANCHI KANA KWAMBA WANANCHI NI MAHAKAMA.
"Huyu mzee, hana hoja ngeni sana sana kipya alichokionyesha ni HASIRA, JAZBA, DHARAU NA KIBURI!.
1. Walihoji, kama Dr. Slaa alijua Lowasa ni mbaya na anatakiwa kupimwa akili, kwa nini alikwenda KUMTAFUTA NA KUMKARIBISHA Chadema? Tatizo la Slaa siyo uchafu wa Lowasa bali ni yaliyotokea baada ya Lowasa kuteuliwa kugombwa uraisi kama mabadala wa Slaa.
2. Slaa aliandaaje mkutano na uwaandishi wa habari huku hana cha kusema hadi asubiri kuletewa na Mwakyembe? Bila shaka huyu Slaa aliongea ya Mwakyembe kwa niaba ya ccm.
3. Mwakyembe na ccm kushindwa kusema wao na badala yake kumtumia Slaa, ni dalili kwamba hawana ujasiri wa kuyasema waliyomsakizia slaa ayaseme. Kama chama kinahcounda serikali kinashindwa kusema hoja hadi kitafute mkandarasi, kimejiondolea sifa ya kusimamia serikali.
4. Slaa na Mwakyembe, habari ya Richmond miaka yote waliijua, kwa nini walishindwa kuisukuma ili hatua stahiki zichukuliwe badala yake Slaa akaenda mbele zaidi ya kumshawishi Lowasa ajiunge naye, na sasa kuibua hoja hizi baada ya Slaa kukatwa? Hoja hii inatumika kwa visasi. Wnasema hawako tayari kutumika kama fimbo ya kulipa visasai vya mtu yeyote. Wao CCm iondoke kwanza.
5. Slaa kumwogopa Lowasa na kutaka kutulazimisha tuiache ccm madarakani huku akijua ni ccm ni hatari kuliko lowasa, bila shaka hajitambui na hayupo tena kwa maslahi ya Watanzania.
6. Mwakyembe kwenda na taarifa za Richmond kuzipeleka kwa Slaa, na Slaa kuungana na viongozi wa ccm kina Sita na Mwakyembe, kulalamika kuhsu Lowasa na richmond kwa wananchi, wakati wakijua sehemu sahihi ya kulalamika ni mahakamani, WANATUFANYA WATANZANIA WAPUMBAVU WA KUTUCHANGANYA HUKU WAKIFICHA UKWELI.
7. Serikali ya Ccm kushindwa kumfikisha mahakamani Lowasa na watuhumiwa wengine wa ufisadi, badala yake kuishia kulalamika mitaani, wote ni wapuuzi wasiofaa kuitwa viongozi wa nchi. Hawawezi kusimamia haki za wananchi.
8. Dr. Slaa kuwaita CCM NI CHOO CHA MAVI, na Lowasa ni Kinyesi kilichoopolewa kwenye choo, ni kuzidi kuididimiza ccm na kumpigia kampeni Lowasa. WAMEAMUA KUMCHAGUA LOWASA AMBAYE NI KINYESI KILICHOOPOLEWA KUTOKA KWENYE CHOO CHA MAVI, KULIKO KUCHAGUA CHOO CHA MAVI!.
9. Kimbelembele cha Ccm kumshangilia Slaa, baada ya kumpinga na kumpiga na kiasi cha kumjeruhi akisimamia sera za CHADEMA, imedhihirisha Slaa amewauza Watanzania na imedhihirisha uharamia wa ccm kutumia rushwa na madarka vibaya katika kutaka kuwaumiza Watanzania.
10. Wananchi wa Mwanza, sasa wanajua Slaa na Ccm ni wamoja, na hawana loloe la maana lenye maslahi kwa Watanzania. Maandamano fake ya vijana walioandaliwa na ccm ili wajifanye ni CHADEMA, watu walisema ni sawa na ngoma za "BULABO", na "MALEBA YAKE". Mtanisaidia tafsiri sahihi ya BULABO NA MALEBA ni kitu gani.
11. Slaa kushindwa kuzungumzia mawizi mengine yaliyofanywa baada ya kuondoka Lowasa, ni dhahiri huyu kanunuliwa na ccm ili aongee lugha ya ccm na si ya Watanzania.
12. WAMESEMA SLAA NENDA SALAMA, KAZI ALIYOIFANYA WANAIHESHIMA LAKINI AKIENDELEA KUTUMIWA N AKINA MWAKYEMBE, ATAKUWA ANATANGAZA VITA YA YEYE BINAFSI DHIDI YA UMMA.
WAKAZI WA MWANZA HAWAKO TAYARI KUTUMIWA NA SLAA KWA KUSHIRIKIANA NA CCM ILI KUHUJUMU UKOMBOZI.
KWA HILI CCM IMEJIABISHA, WALITEGEMEA DR. SLAA ATAWASAIDIA BADALA YAKE BILA KUTEGEMEA AMEZIDI KUWAWEKA KATIKA HALI MBAYA ZAIDI.
CCM HAMTAWEZA KULAANI MPANGOWA UKOMBOZI WA MUNGU KWA WATANZANIA KWA KUMTUMIA SLAA, LIPUMBA, KUTENGENEZA MAANDAMANO NA KADI ZA BANDIA, AHADI ZA HEWA N.K. MUNGU ALISHAWAKATAA NA HAKUNA KITAKACHO WASIMAMISHA TENA.