Maaskofu waipinga CHADEMA...

Maaskofu waipinga CHADEMA...

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Posts
36,967
Reaction score
68,834
Askofu KKKT atahadharisha uanzishwaji vikundi vya ulinzi

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma, Amon Kinyunyu, amesema kitendo cha viongozi wa vyama vya siasa ya kuamua kujianzishia vikundi vya ulinzi wa kujilinda kwenye vyama vyao, ni ishara tosha ya kuhatarisha amani ya Taifa.

Askofu Kinyunyu amesema viongozi wa siasa wanaoanzisha vikundi vya namna hiyo ni kuashiria jinsi gani walivyokosa heshima kwa Mungu na kwa mamlaka ya serikali ambayo ina ulinzi na usalama unaolinda nchi kwa ujumla.

Alitoa kauli hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa miradi ya mifumo ya miundombinu ya watoto ikiwamo ya maji, madarasa na vyoo vya kisasa iliyodhaminiwa na shirika la Compassion International Tanzania kwa kushirikiana na washirika wenza kutoka kwenye Makanisa ya Huduma ya Mtoto iliyofanyika katika viwanja vya Kanisa la Tag Miyuji mjini hapa.

Askofu Kinyunyu alisema kitendo cha vyama hivyo kuanzisha vikundi vya kujilinda, ni ishara ya kuleta machafuko ya amani ya nchi.

Pia alisema kitendo hicho kitawafanya vijana waliopo katika vyama hivyo kuendelea kuchukiana badala ya kupendana.

Alisema viongozi wa kisiasa hawana budi kutambua kuwa kwa kuanzisha vikundi hivyo ni kuzidi kujenga uhasama mkubwa utakaoiumiza jamii isiyohusika wakiwamo watoto, wanawake, wazee na walemavu.

"Hapa wanatakiwa kujua kuwa kitendo hicho ni ishara tosha inayoashiria kuanzisha vita ambayo washirika wakubwa ni vijana tunaowategemea kushika madaraka mbalimbali ya kiserikali na ya kisiasa," alisema.

Askofu Kinyunyu amewataka viongozi wa vyama vya siasa kuheshimu amani iliyopo iliyobarikiwa na Mungu tangu kuumbwa kwa ulimwengu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Compassion Intenrational Tanzania (CIT) hapa nchini, Mchungaji Joseph Mayala, alisema kitendo hicho ni sasa na uwekezaji kwa vijana wawe na roho ya ukatili badala ya upendo na amani.


Source: Home

NB:

..Askofu Mkuu wa KKKT Malasusa naye ametoa kauli inayoelekea kuwananga CDM.

..soma hapa chini:Home
 
Asanteni maaskofu, msg sent ila sidhani kama itafanyiwa kazi na hawa watu maana vichwa vyao vigumu sana.
 
Alitakiwa kwenda mbali zaidi ya hapo kama ameamua kuacha altare na kujiingiza kwenye siasa.
Alitakiwa avitaje vikundi kwa majina, vilianza lini, na vinayemtumikia ni nani!.

Ni ukosefu wa umakini kulaumu vikundi vya ulinzi huku akiacha vacuum ya ulinzi katika vyama, wakati anajua wazi yanayotendeka na walinzi rasmi-Polisi.
Huyu alitakiwa aombwe aongelee suala la Mwangosi kwanza, ndipo athubutu kulaani vikundi vya ulinzi.
Hapa ndiyo utajua mipaka ya kazi hizi inamaanisha nini!
 
Leo ndo hao maaskofu wamezinduka?! Napata mashaka sana na jinsi walivyogutuka. Wanalamikia kikosi kinachoboreshwa wakati vilivyokomaa hawavizungumzii? Makubwa!!!
 
Haya yoote wanaongea hawakujua kama kulikua na kikosi cha ugaidi na mauaji kinaitwa "Green Guard" na washukuru Mungu Red Brigade imewekwa wazi na viongozi wa CHADEMA, ingekuwa na nia mbaya wangejificha. Lakini wamejulisha wananchi kwamba sasa ni wakati wa kujilinda...dhidi ya uonevu wa kundi linalolindwa na serikali green guard.

Sasa hapo wangeweza kuona mwanzilishi wa chuki nchini ni nani.
 
NADHANI huyo askofu amekurupuka na hajui maana na dhana YA kuanzidhwa kwa hicho kikundi. Cdm NI vizur waandar press conference na kutuambia malengo na madhumuni YA kikundi hicho
 
Wanapinga vikundi vyote vya ulinzi. Inamaana hata green guard. Hakuna aliposema green guard ni halali.
 
Mbona sijaona mahali amewasema CHADEMA. Mi naoma kasema vyama vya siasa maana yake hata CCM na CUF wana vikundi vya ulinzi hivyo ni angalizo kwa vyama vyote na sio CHADEMA kama unavyotaka kuaminisha. Rudia hiyo habari vzr na usimlishe huyo askofu maneno
 
Mbona wao wameongea na Bosi wa Jeshi la Polisi Nchini kuhusiana na suala hilo hilo ambalo leo kiunafiki wanawapinga Chadema au misaada ya Sheikh Abdallah Lowassa inaanza kulipa kistaili?Nchi hii haishiwi Wanafiki!!
 
kanisa lilianzishwa kabla ya green guard. walipaswa kukemea green guard kwanza. inashangaza maaskofu kutoa matamko yenye harufu zote kuwa wamepewa mlungula na kuambiwa 'semeni hivi'
 
Nashukuru huyo askofu amesema hayo maana ukimiya wao ungehusishwa na CHADEMA kuwa chama cha kidini.........yote ya yote CHADEMA wanatakiwa kutoa maelezo zaidi na ufafanuzi makini juu ya hili suala maana naona maadui wanatafuta pa kushikia.
 
Hivi kujilinda ni kuvuruga amani?, haya nayo maajabu haya.

Haki ya kujilinda haihitaji ruhusa ya kutoka popote, tutajilinda na mazoezi ya ukakamavu tutafanya.
Wakati viongozi wangu wapendwa wa CHADEMA wakipanga namna ya kuendesha suala hilo, mimi mwenyewe kuanzia kesho naanza kufanya mazoezi ya ukakamavu kwa ajili ya kujilinda, kama ni kosa wanikamate basi.
 
Back
Top Bottom