Maaskofu wa mitaani, mjipime

Maaskofu wa mitaani, mjipime

.

Queen Esther

Yaan we ndo huelewi kabisa.
Huwa sipend kuchangia mijadala ya aina hii ila naomba nikueleweshe kidogo.
kauli ya kwamba hawa wote ni watumishi wa Mungu si kweli.
Ukweli ni kwamba Mmoja ni mtumishi wa Mungu na mmoja si Mtumishi wa Mungu AU pia inawezekana wote wakawa si watumishi wa MUNGU.
Nakuachia wewe ung'amue yupi ni mtumishi wa kweli na yupi si mtumishi wa kweli.
Usiwe na imani ya woga. usiogope adhabu au ghadhabu ya Mungu kama unasimamia ukweli.
Usiogope kumsema mtu anayejiita mtumishi wa Mungu kama anaendana kinyume na utaratibu wa Mungu.
USIWE MWOGA. SPEAK YOUR MIND.
Kwa akili ya kawaida tu jiulize mtumishi mmoja hawezi kutumwa na Mungu Mmoja kwenda kumtukana Mtumishi mwingine wa Mungu huyo huyo kuwa ni mpuuzi,mjinga, hafai, aende akalime aache utumishi......na matusi mengine mengi anayodai katumwa na Mungu awataarifu waumini zake.
Kwa logic ya kawaida kabisa hawa wawili hawawezi kuwa watumishi wa MUNGU MMOJA.
think.open your mind. mtafute Mungu ndani ya Moyo wako.usibabaishwe na wababaishaji na mwisho kabisa achana na IMANI ya WOGA. Hata Mungu aliyekupa free will na thinking capacity akakuweka huru kwa kifo cha Mwanae Msalabani HAPENDI IMANI YA WOGA.[/QUOTE]

Hector!!!!
The battle is The Lord. Who am I to judge the servants of the most high?

As long as wote wanamuhubiri Kristo iwe kwa hila iwe kwa kweli; mwenye kuwahukumu ni Bwana. Mimi siijui mioyo yao. Kwanini uisaidie kazi ya Bwana? Soma habari za yule mtu aliyesaidia Sanduku la agano lisianguke nini kilimpata? Angalia kisikupate.

Sio uoga ni maonyo tu mpendwa. Jambo hili lina maana kubwa ktk ulimwengu wa roho. Be careful!!!!

Queen Esther[/QUOTE]

sina cha kuogopa as long as i am breathing free air.
ila ukweli utabaki pale pale mmoja wapo kati ya Pengo na Gwajima si mtumishi wa Mungu wa kweli.
hii ni logic ya kawaida hatuna haja ya kunukuu vifungu vya biblia.
na hii si hukumu kwa sababu sijasema yupi si mtumishi wa Mungu bali nimesema wote wawili hawezi kuwa watumishi wa Mungu Mmoja.
 
Hector!!!!
The battle is The Lord. Who am I to judge the servants of the most high?

As long as wote wanamuhubiri Kristo iwe kwa hila iwe kwa kweli; mwenye kuwahukumu ni Bwana. Mimi siijui mioyo yao. Kwanini uisaidie kazi ya Bwana? Soma habari za yule mtu aliyesaidia Sanduku la agano lisianguke nini kilimpata? Angalia kisikupate.

Sio uoga ni maonyo tu mpendwa. Jambo hili lina maana kubwa ktk ulimwengu wa roho. Be careful!!!!

Queen Esther[/QUOTE]

sina cha kuogopa as long as i am breathing free air.
ila ukweli utabaki pale pale mmoja wapo kati ya Pengo na Gwajima si mtumishi wa Mungu wa kweli.
hii ni logic ya kawaida hatuna haja ya kunukuu vifungu vya biblia.
na hii si hukumu kwa sababu sijasema yupi si mtumishi wa Mungu bali nimesema wote wawili hawezi kuwa watumishi wa Mungu Mmoja.[/QUOTE]

Hector,
Mpuuzi na mjinga sio matusi, ni maneno ya maonyo. Soma vifungu vifuatavyo:-
Zaburi 49:10, 92:6, Mithali 12:1; Yeremia 4:22 na 10:8

Queen Esther
 
We unaonyesema baado hujui Ukristo ndo maana hujajua umeandika nini zaidi ya kufurahisha hadhira. Hii inaonyesha we si wa Kiristo. Me sikukubaliana na alichofanya Pengo kwa 100%. Ni msaliti wa Maagano. Kama sehemu ya jopo la maamuzi hakusitahili kukana yaliyokubalika.

Huku ni kujipendekeza kwa CCM.

Anasitahili kukaywa.

Parokia zote za Makanisa ya Katoliki yalitangaza walaka ule. Yeye alikuwa wapi??

Sijui watu mkoje yaani we unaona gwajima alikuwa sahihi kuporomosha matusi yote hayo?
Siku zote huwezi kumaliza tatizo kwa kutengeneza tatizo alichokifanya Gwajima ni kufuata usemi wa Fid Q kuwa Dawa ya mpumbavu ni kuwa mpumbavu zaidi yake' Gwajima ni mpumbavu mara 1000 kuliko Pengo....
 
hizi taarifa amelazwa kwa presha umezitolea wapi?!

Chanzo Mtanzania...

ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima jana alizimia na kisha kukimbizwa hospitali wakati akihojiwa Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
Gwajima ambaye alijisalimisha kituoni hapo saa 8:22 jana mchana akiitikia wito wa polisi uliomtaka kufika kutokana na tuhuma za kutoa lugha chafu dhidi ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Waandishi wa Mtanzania Jumamosi waliokuwa kituoni hapo wanaeleza kuwa walimuona Gwajima akitolewa kutoka katika chumba cha mahojiano akiwa amebebwa.
Kwa mujibu wa waandishi hao Gwajima ambaye alikuwa amebebwa na maofisa wa polisi alipelekwa moja kwa moja kwenye gari aina ya Noah kwa ajili ya kumpeleka hospitali.
Tukio hilo lililotokea majira ya saa 3:16 usiku lilikuja katika kipindi kisichozidi dakika saba tangu askofu huyo alipoonekana akiwa ameshikiliwa na wasaidizi wake kuelekea msalani huku yeye mwenyewe akiwa amejishika kichwa.
Wakati akipelekwa hospitali, msafara wake ulikuwa ni wa magari mawili mojawapo likiwa ni aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili PT 1848 na Noah yenye namba za usajili T 215 BEM.
Akizungumza na gazeti hili kituoni hapo, mwanasheria wa askofu huyo, John Mallya alisema wakati wakiwa katika mahojiano, alisema anahisi kizunguzungu na baadaye akaishiwa nguvu na akawa amefumba macho.
Mallya alisema baada ya hali hiyo kutokea, polisi walimchukua na kisha kumpeleka katika hospitali ya Jeshi la Polisi iliyoko Kurasini, Dar es Salaam.
Wakati Mallya akiwasiliana na gazeti hili majira ya 4:30 usiku alisema kuwa walikuwa wakifanya mchakato wa kumuhamishia katika hospitali ya TMJ kutokana na yake kutokuwa nzuri.
“Siwezi kujua tatizo ni nini na siwezi kuzungumza chochote kuhusu hilo maana hayo ni mambo ya kitabibu” alisema Malya.
Ilipotimu saa 4:41 Waandishi wa gazeti hili ambao nao walifika katika hospitali hiyo ya Jeshi la Polisi walishuhudia Gwajima akitolewa katika hospitali hiyo ya Jeshi la Polisi na kisha kupakizwa katika gari maalum la kubebea wagonjwa lenye namba DFP 6309.
Wakati hayo yakitokea taarifa nyingine zilizolifikia gazeti hili zilidai kuwa; kwa muda wote akiwa katika mahojiano, Gwajima alikuwa hajala chochote hali ambayo iliibua wasiwasi kwamba huenda ilichangia kubadilika kwa afya yake.
Polisi mmoja aliyekuwa katika chumba cha mahojiano aliwaeleza waandishi wetu kwamba Askofu Gwajima alipoteza fahamu muda mfupi baada ya kuhojiwa kuhusu mali anazozimiliki.
Awali wakati Gwajima alipowasili kituoni hapo mchana kabla ya kuhojiwa alizungumza na waandishi wa habari ambapo alikiri kutoa lugha chafu dhidi Kardinali Pengo.
Gwajima ambaye alifika kituoni hapo saa 8:22 mchana alisema kauli yake hiyo ambayo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii aliitoa kutokana na Kardinali Pengo kuwageuka wenzake ambao ni Baraza la Maaskofu Tanzania linalounganisha Wakatoliki, Pentekoste na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kukubaliana kwa pamoja kuwa hawataki Mahakama ya Kadhi.

Alisema maaskofu wote walikubaliana kuhusu tamko hilo na kisha kulisaini lakini anamshangaa Kardinali Pengo ambaye pia alisaini kuwageuka.

“Mimi kama kiongozi wa kiroho nikaona nimkemee kiongozi mwenzangu wa kiroho aache mambo ambayo si mazuri. Hakuna maneno ya kashfa ambayo nimeyatoa. Niliyotoa ni neno la Mungu linalotumiwa kumwongoza mtumishi wa Mungu,” alisema Gwajima.

Alisema anashangaa kuitwa polisi kwani hajatukana polisi na ndio sababu akaitika wito na kufika.

Gwajima alifika polisi akitembea kwa miguu kutokana na foleni kali iliyokuwepo barabarani huku akiwa ameongozana na Mwanasheria wake John Malya pamoja na baadhi ya wachungaji, waumini wa kanisa hilo na wengine waliotajwa kuwa ni walinzi wake.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Kamishna Suleimani Kova alisema Mchungaji Gwajima ametii amri ya Jeshi hilo kama alivyotakiwa.

Kova alisema baada ya kufika kituoni hapo alielekezwa kwenda kumuona Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam SACP Costantine Massawe.

Akitaja tuhuma zinazomkabili Mchungaji Gwajima, Kova alisema ni pamoja na kumkashifu na kumtukana hadharani kiongozi wa Kanisa Katoliki Kardinali Pengo.

“Taratibu za kuhojiwa zimeshaanza kwa mujibu wa sheria na mtuhumiwa atapewa haki zote anazostahili ikiwemo kuwa na ndugu yake wa karibu, rafiki anayemwamini au wakili wake. Kama ilivyokawaida utakusanywa ushahidi kutoka pande zote za shauri hilo ili kubaini ukweli wa jinsi tukio hilo lilivyotokea,” alisema Kova.

Kova alisema baada ya hapo hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kupata maoni ya kitaalamu na ya kisheria ili kuhakikisha kwamba haki inatendeka.

“Ili ufanisi upatikane katika upelelezi wa shauri hili ni muhimu kupata ushirikiano kutoka kwa kila atakayetakiwa kulisaidia Jeshi la Polisi kukamilisha haraka upelelezi wa shauri hilo ambalo limepata mvuto mkubwa kwenye jamii,” alisema Kova.

Katika video na sauti zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii hasa What’s App, Gwajima alirekodiwa akiwa kwenye ibada ya kanisa lake akitumia lugha zisizokuwa na staa kwa Kardinali Pengo akimtuhumu kuwa ni msaliti kwani amekwenda kinyume na Taasisi ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Baraza la Makanisa ya Kipentekoste (CPCT) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kwa kuwataka waumini waisome Katiba Inayopendekezwa kisha wapewe uhuru wa kupiga kura ya “ndiyo” au “hapana” tofauti na vyombo hivyo vyenye dhamana ya kuongoza dini ya Kikristo vilivyotaka waumini waipigie kura ya “hapana”.
 
Si kujipima tu,bali waache tabia ya kuuvuruga ukatoriki kwa visingizio vya kijinga.
Na waache pia tabia ya kujifanya wagonjwa baada ya kuojiwa ili eti wadroo attention ya huruma ya watu na kuhurumiwa na dola.
Ni upumbavu kujifanya wajuaji kwa kipindi kifupi tu cha utumishi wao na pia waache kutumia uchawi na mazingaombwe ili kuvuta waumini.
Sitoshangaa kama na wao wakipekuliwa ili jamii ijue kama na wao wanatumia viungo vya albino katika mambo yao ya utumishi.
 
Lazima ujuwe kwanza maana ya uwakilishi

Facts tu mkuu, haya mengine yatajifia natural death. Bahati mbaya mmeamua kukurupukia na kushabikia tena kwa mihemko zile kauli za Gwajima zisizo na staha hata kidogo. Kaeni na fanyeni tafakari ya kina kuhusu kauli ya Kardinal. Nguvu na ujasiri wa kupingana na Maaskofu wenzake umejikita kwenye mantiki ipi na katika ukweli gani. Ukifanya hayo kwa dhati ya moyo wako utabaini heri tupu ndani yake. Kwa heri....
 
Si kujipima tu,bali waache tabia ya kuuvuruga ukatoriki kwa visingizio vya kijinga.
Na waache pia tabia ya kujifanya wagonjwa baada ya kuojiwa ili eti wadroo attention ya huruma ya watu na kuhurumiwa na dola.
Ni upumbavu kujifanya wajuaji kwa kipindi kifupi tu cha utumishi wao na pia waache kutumia uchawi na mazingaombwe ili kuvuta waumini.
Sitoshangaa kama na wao wakipekuliwa ili jamii ijue kama na wao wanatumia viungo vya albino katika mambo yao ya utumishi.
Tetesi za ushirikina zipo
Hasa yule "Askofu" karibu na Mlimani City.
 
Hao wengi ni wale Yesu aliowaita manabii wa uongo. Wanachokitafuta ni fedha na publicity. Bahati mbaya wanavipata na wanasiasa wanajipanga foleni kuwafuata! Huyo Gwajima anawezaje kujilinganisha na pengo si kwa elimu, hekima wala ufahamu wa mambo ya dini ya kikristo!

Gwajima ni muhuni,kichaa au mwehu!Hatupaswi hata kumjadili tutajidharilisha.Yeye sio msemaji wa Wakristo waliotamka.Angali unyoaji wake wa nywele,uvaaji,setup ya lips zake,body mobility awapo madhabahuni au jukwaani utapata picha halisi kuwa n kichaa.Ungekuwa mjadala kama naneno hayo angetamka Malasusa au Mokiwa lakn Gwajima???Achana na kibaka huyo.
 
Nimejaribu kufikiri kila kona kutafuta njia ya kuukubali uaskofu wa Gwajima nimekosa. Jamani eeh. Huyu jamaa ni tapeli
 
Sijui watu mkoje yaani we unaona gwajima alikuwa sahihi kuporomosha matusi yote hayo?
Siku zote huwezi kumaliza tatizo kwa kutengeneza tatizo alichokifanya Gwajima ni kufuata usemi wa Fid Q kuwa Dawa ya mpumbavu ni kuwa mpumbavu zaidi yake' Gwajima ni mpumbavu mara 1000 kuliko Pengo....
Sasa hivi nadhiri inamhukumu "Askofu"Gwajima , na ndio maana polisi walipoanza kudadisi "utakatifu" wake, nafsi ikashindwa kuvumilia.
Hizi nafsi zetu dhaifu na zenye dhambi, tusizipambanishe na roho mtakatifu, tuziombee tupone.
 
Wapitisheni Ntungamo Major seminary wapate brush kidogo.Inawezekana wanadhani uaskofu ni kuvaa kofia
 
Sijui watu mkoje yaani we unaona gwajima alikuwa sahihi kuporomosha matusi yote hayo?
Siku zote huwezi kumaliza tatizo kwa kutengeneza tatizo alichokifanya Gwajima ni kufuata usemi wa Fid Q kuwa Dawa ya mpumbavu ni kuwa mpumbavu zaidi yake' Gwajima ni mpumbavu mara 1000 kuliko Pengo....

Hawa jamaa sijui wanapewaga nini wakienda huko kwa Gwajima. Maana wakirudi akili zao zinapotea kabisa. Wanapoteza uwezo wa kufikiri.
 
Gwajima ni muhuni,kichaa au mwehu!Hatupaswi hata kumjadili tutajidharilisha.Yeye sio msemaji wa Wakristo waliotamka.Angali unyoaji wake wa nywele,uvaaji,setup ya lips zake,body mobility awapo madhabahuni au jukwaani utapata picha halisi kuwa n kichaa.Ungekuwa mjadala kama naneno hayo angetamka Malasusa au Mokiwa lakn Gwajima???Achana na kibaka huyo.

Nimekupenda ghafla
 
Back
Top Bottom