Maaskofu Katoliki watoa waraka tena | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maaskofu Katoliki watoa waraka tena

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Madabwada, Feb 17, 2010.

 1. Madabwada

  Madabwada JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2010
  Joined: May 8, 2009
  Messages: 537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Na Joseph Sabinus
  Tanzania Daima

  KANISA Katoliki nchini limeibuka tena na kutoa waraka kwa waamini wake kuhusu namna bora ya kushiriki uchaguzi mkuu ujao na safari hii likitoa maswali mazito kwa wagombea ambayo waumini wao wanapaswa kuyazingatia.

  Waraka huo umo kwenye ujumbe wa Kwaresima wa mwaka huu, walioutoa hivi karibuni na kusainiwa na maaskofu wa majimbo yote 31 nchini, wakiongozwa na dhamira kuu isemayo “Ninyi ni Chumvi ya Dunia…” (Mt 5:13).

  “Kama tunavyofahamu, nchi yetu iko katika mchakato wa uchaguzi mkuu, utakaofanyika Oktoba 2010. Uchaguzi huo utatupatia viongozi wapya: madiwani, wabunge na rais wa nchi yetu.

  “Uchaguzi huo ni tukio la kijamii na vile vile ni tukio la kisiasa. Ni tukio ambalo Wakristo wote wanapaswa kushiriki kama wajibu wao. Historia yatwambia kwamba, ushiriki wa Wakristo katika mambo ya ulimwengu umekuwa wa namna tofauti katika kipindi cha zaidi ya miaka 2000,” ilisomeka sehemu ya waraka huo.

  Kwa mujibu wa waraka huo wenye kurasa 30, namna moja ya Wakristo kushiriki katika masuala ya kiulimwengu ni kwa njia ya kushiriki katika masuala ya kisiasa kwa kuwa wanaposhiriki katika masuala ya kisiasa wanatimiza wajibu wa kiraia.

  Katika ujumbe huo wa Kwaresma mwaka huu, maaskofu hao wanasema uchaguzi huo ni tukio la kijamii na la kisiasa, hivyo Wakristo wote hawana budi kushiriki kikamilifu ili kutimiza wajibu wao.

  Kwa upande wa wagombea watakaojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi, waraka huo umewataka kujiuliza wanataka kuwafanyia nini Watanzania ili wawe na maisha bora yanayompendeza Mwenyezi Mungu.
  “Tunaomba sana na kuwasihi wale wote wanaogombea katika nafasi hizo za uongozi wafikiri na kutafakari kwa makini ni kitu gani kimewasukuma ili kuchukua hatua hiyo? Wanataka kwa moyo wao wote kuwatumikia Watanzania ili kila mtu katika jamii yetu apate hadhi yake ya kiutu ambayo ni stahili yake?” ulihoji waraka huo.

  Aidha, maaskofu hao wamewataka wagombea wote kujiuliza kama kweli wana nia ya dhati ya kuwasaidia Watanzania ili kila mtu apatiwe mahitaji msingi ya kumwezesha kuishi maisha yanayomstahili mwanadamu, pamoja na kuwa tayari kuzifanya rasilimali za nchi yetu kuwa kwa ajili ya manufaa ya wote.

  “Wakati tunawahimiza waamini wote kushiriki katika zoezi zima la uchaguzi, tunaomba vile vile wale watakaoshiriki katika kuchagua, wawahoji na wapime udhati wa nia ya wagombea kwa kufuata vigezo vya hadhi ya utu wa mwanadamu na tunu za kimaadili.

  “Kamwe msichague mtu kwa sababu ya shinikizo, wala kwa sababu ya rushwa, au ubaguzi wowote ule kwani kwa kufanya hivyo mtakuwa mnakosea mbele ya Mungu. Muwachague viongozi mkiwa mmeongozwa na dhamiri safi mbele ya Mungu na hivyo muwachague viongozi ambao wataliongoza taifa hili kwa kujali maslahi ya wote na ambao watatusaidia kujenga jamii yenye upendo, umoja, haki na amani,” inasomeka sehemu ya waraka huo.

  Maaskofu hao wamesisitiza kuwa, kamwe binadamu hawezi kutenganishwa na Mungu na wala siasa haiwezi kutenganishwa na maadili.

  “Hili ndilo jambo ambalo Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambaye mchakato wa kumtangaza Mwenyeheri unaendelea, alitufundisha kwamba siasa lazima ijengwe katika misingi imara ya kanuni thabiti za kimaadili zinazopaswa kuwa ndiyo mhimili wa maisha katika jamii,” walisema maaskofu hao.

  Walisisitiza kuwa katika kipindi hiki ambacho nchi ipo katika mfumo wa vyama vingi vya siasa, waumini wana haki ya kujiunga na kushiriki katika kuchagua ama kuchaguliwa ili kutimiza wajibu wao.

  Walisisitiza kuwa hali hii ya kuwapa uwezo na haki ya kushiriki uchaguzi kupitia vyama mbalimbali vya siasa, haiwezi kuchanganywa na hali ya kushindwa kutambua na kuchagua kanuni za kimaadili na tunu za msingi zinazojali hadhi ya utu wa binadamu.

  Wamekwenda mbali na kusema kuwa, demokrasia ya kweli ambayo uchaguzi ni sehemu tu ya kielelezo chake, itafaulu endapo tu itajengwa juu ya uelewa sahihi wa nafsi ya binadamu.

  Walitahadharisha kuwa ushiriki wa Wakristo katika siasa na hasa katika uchaguzi ujao, haupaswi kuipuuzia kanuni hii vinginevyo ushuhuda wa imani ya Kikristo ulimwenguni na muungano unaopaswa kuwepo kati ya yale ambayo Wakristo wanayaamini na maisha yao ya kawaida hautakuwepo.

  “Huenda badala ya kuwa chumvi inayokoleza katika jamii, mara nyingine mmekuwa kama chumvi isiyo na ladha kwa kuwa chanzo cha uozo katika jamii. Au wakati fulani na katika mazingira fulani mmekuwa ndiyo chanzo cha kueneza ubinafsi, uchu wa madaraka na hata wa mali?” walisema maaskofu hao katika waraka huo.

  Miezi kadhaa iliyopita, maaskofu Wakatoliki hao walitoa waraka wa kichungaji uliovuta hisia za wengi ukiwa unatoa elimu kwa waamini wake juu ya namna ya kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao na kuwapata viongozi bora kwa njia sahihi.


  nb: wanajamvi .... aliyenao aturushie jamvini pls ...
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,231
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  HII Imeshatolewa na member anaeitwa Analyst leoleo, na iko hewani...tusome threads jamani!
   
 3. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #3
  Feb 17, 2010
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Dini haina msaada zaidi yaku-influence siasa for its own self-preservation. Tanzanians should not subscribe to this kind of nonsense, regardless of the faith. None of them have a sincere motive at heart. Unfortunately, ndio ukweli.. (History reveals all..)
   
 4. Madabwada

  Madabwada JF-Expert Member

  #4
  Feb 17, 2010
  Joined: May 8, 2009
  Messages: 537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  noted!

  MDBD
   
 5. M

  Mende dume Member

  #5
  Feb 17, 2010
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wasemayo ni maneno mema, lakini watutake radhi kwa maoni yao mwaka 2005, kuhusu chaguo la mungu. which we bought without checking the facts, i.e. how could mungu choose a person from this religion or belief and then reveal the choice in another and different group! secondly how come this Mungu is so wrong to give a country an unguided misile that hits within the country for its self distruction?
   
 6. M

  Magezi JF-Expert Member

  #6
  Feb 17, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,916
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  syo vibaya kwani ni elimu ya uraia
   
 7. Kabuche1977

  Kabuche1977 JF-Expert Member

  #7
  Feb 17, 2010
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 463
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ni kitu cha kushangaza mtu ambaye ni JF expert member halafu anatukana ndani ya wana JF, man please hii ni tank-thinking place sio sehemu ya kuongelea mambo ambayo hayana miguu wala mikono, au jina lenyewe ni symbol ya jinsi ulivo----------you can be a bull still not smart.
  kanisa lina wajibu wa kuelimisha waumini wake kuhusu mambo yahusuyo malimwengu ikiwemo siasa, sasa sioni kama kuna ubaya wa kuanza kuelimisha kuhusu jinsi ya kuchagua viongozi wao kuanzia ngazi zote halafu ikafuata maada nyingine, what is wrong with that??? au wewe ndo wale wale mpinga Kristo na maaendeleo, hatukuhitaji mtu kama wewe kwenye think-tank yetu kama huna mawazo yanayojenga (constructive ideas)
   
 8. B

  Bull JF-Expert Member

  #8
  Feb 17, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha jazba mkuu, hapa hajatoukanywa mtu, suala la ushoga makanisani sio matusi kuyazungumza , kumbuka mkutano wa usenge kanisani ulifanyika Tanzania, kama ilikuwa matusi kwanini wachungaji walilidadisi na wengine kuwa member na kupractice usenge

  Kumbuka niwajibu wa kanisa kuongoza wafuasi wake kwenye utata mkubwa wa jambo kama hili kuliko siasa, kwasababu swala la usenge nil kiroho na siasa ni la kijamiii

  Watoe waraka wa kuwaelimisha wafuasiwake kuhusu usenge, whether wafuasi wake wawe ******* au la!!

  Bro; free your mind!!
   
 9. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #9
  Feb 17, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 30,307
  Likes Received: 29,018
  Trophy Points: 280
  sidhani kama suala la ushoga huko kanisani kwao linatuathiri WATZ in general kwa sababu wana uhuru wao kuamua jinsi ya kuendesha kanisa lao,but im sure 100% hili la uchaguzi,as you know ni haki yako kikatiba,linamhusu/kumgusa/kumfaidisha kila MTZ bila kujali muislam,mkristo,mpagani
   
 10. Kichwa

  Kichwa Senior Member

  #10
  Feb 17, 2010
  Joined: Mar 15, 2007
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Swala la ushoga ni Anglican au katoliki?
   
 11. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #11
  Feb 17, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,754
  Trophy Points: 280

  I dont think if your contributon could have been valueless without the bolded words.May you grow up bro/sister! Just keep pace with modern civilized society of information and technology with self respect as human being at heart!
   
 12. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #12
  Feb 17, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,482
  Likes Received: 457
  Trophy Points: 180
   
 13. m

  mubi JF-Expert Member

  #13
  Feb 17, 2010
  Joined: Feb 3, 2010
  Messages: 330
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Homosexuality, kwa mimi ninavyojua haliko Catholic, wakatoliki tuna sakramenti 7, hatuhubiriwi tupractice homosexuality. Kwa taarifa yako hiyo ni dhambi.
   
 14. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #14
  Feb 17, 2010
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  What are you on about dude? The Catholic church paid off over a billion dollars in compensation for the Molestations that its priests have carried out..on BOYS.. Shame.. and the Pope refuses to apologize to the faithful.shame shame shame. Tanzania haitoendelezwa na dini wala siasa zakidini. We need science..period.
   
 15. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #15
  Feb 17, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Hongera sana Kanisa katoliki..Mwendo huo huo mpaka kileweke.
   
 16. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #16
  Feb 17, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,624
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  These are some of the weak arguments that never sink into my cerebral. Why reject facts based on the bad history of the narrator! That is wrong and wrong again!

  What they say is correct and perfect like any offender who helps the court to convict another offender. The past wrong cannot deny them a chance to say the today’s truth.

  Najua wanaofaidika na siasa uchwala hawataki kabisa elimu kwa wapiga Kura.
   
 17. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #17
  Feb 17, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 30,307
  Likes Received: 29,018
  Trophy Points: 280
  kaka,
  kwenye RED hapo....hao wote walioendelea pamaoja na science SIASA SAFI imeplay part kubwa sana..eg UK,USA to name few
  huwezi ku-by pass siasa ili uendelee,tatizo ni siasa gani tunafuata,siasa yetu chafu.
  kuhusu Catholic church priests molestation hao ni individual sio policy/mafunzo ya Catholic church
  Go back to the point of this thread.....elimu ya uraia ni muhimu kama serikali haitoi acha taasisi nyingine zitoe iwe msikiti au kanisa watu wana haki ya kuelimishwa haki zao
   
 18. Omulangi

  Omulangi JF-Expert Member

  #18
  Feb 17, 2010
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 1,028
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Lakini suala la ushoga si la watu wa pwani bwana? na je mnasemaje kuhusu ushoga unaofanywa waarabu hata kwa wake zao? Mbona mambo haya yanawakumba wakatoliki na waislamu pia. Mimi nafikiri mwisho wa ulimwengu unakuja haraka na walawiti wote waislamu kwa wakristo hata waliomo humu JF watachomwa vibaya kama wale wasodoma walivyofanyiwa.
   
 19. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #19
  Feb 18, 2010
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Najiuliza ungeskia Lowassa ndio ameandika huu waraka sijui ungetoa comment gani. And religion def does more harm than lowassa to people's judgments, its a sad fact. Kitu ambacho kinaweza mfanya mtu amuone muafrika mwenzake sio mtu au kafiri waaina fulani hakifai kwa maendeleo. Sikatai kuwa ni sehemu ya msingi wa maisha yakitanzania. Lakini itakuwa hatari sana kuruhusu dini zianze kuinfluence kiasa in such a direct way. Coming from the one institution that has outlived every other one in the history of man ( most of the time by way of extreme cruelty and inquisition) kwanini waongee leo? Mbona hatukuskia chochote kuhusu ufisadi wakati wa Mkapa.. mbona walikua kimya?lol Jamani jamani.. hizi imani hizi tusiziingize kwenye siasa..
   
 20. B

  Bull JF-Expert Member

  #20
  Feb 18, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Swal la USENGE makanisani ni kansa kubwa na inaathiri jamii na kuongeza kasi za ukimwi na pia nikosa la kuenda jela!

  Chakushangaza makanisa wamelikalia kinymwa swalal hili la laana, sio tu nilaana kwa dini ya ukiristo bali pia kwa taifa, niwajibu wao watoe waraka mkubwa wa kuwaelimisha wachristo athari na laana ya usenge, badala ya kutoa nyaraka za kisiasa kila baada ya miezi sita na huku kanisa likigawanyika kuhusu mchezo huu wa usenge.

  Wako wenye mawazo pungufu hapa jf, tukiongelea swala la usenge kanisani wanasema tunatukana, tuna mapepo, Je wale wachungaji walio jadili wakafanya kikao kikubwa Tanzania 2009 na huku wakitumia gharama kubwa hivi nao wanamapeop?

  Say samething church, Shame on you !!!!!!!!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...