Waraka wa Maaskofu unabagua mambo

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,316
12,615
Serikali imetwangwa barua Waraka na Maaskofu kupinga mkataba wa bandari. Ingawa Baraza hili haliko kisheria kufanya jambo la nchi kama hilo lakini limefanya hivyo baada ya kujiridhisha kuwa serikali, Bunge na mahakama wametenda kosa kwenye mkataba huu. Waraka kama huu ulionekana tena wakati wa hoja ya kuwepo kwa kadhi Tanzania.

Mimi huwa najiuliza maswali kuhusu nguvu hizi za Maaskofu kwanini hazikutumika kupinga Mwl. Nyerere kuifuta serikali ya Tanganyika, kutaifisha baadhi ya shule zao za kanisa kuwa za serikali, wala kupinga nchi kutaifisha mali za serikali kama nyumba, mashirika ya umma na migodi yetu.

Mbona kama waraka hizi zinatolewa zaidi kwenye awamu fulanifulani TU?
 
Wakati wa Magufuli hukuona waraka wowote toka TEC? Umejaa huku JF.

Tatizo lenu mnaendeshwa na mahaba ya dini yenu, hamtaki mama yenu aguswe hata akikosea wazi, hilo haliwezekani, sio kwa Tanganyika hii ya leo.

Kama hamtaki aguswe, muondoeni ikulu muende nae Makunduchi halafu muone kama yupo atakayehangaika nae.
 
Kwahiyo Magufuli alipuuza waraka? Kumbe hauna maana yoyote
 
Kwanini waraka haukutoka wakati serikali inaruhusu vyama vingi 1992 wakati 80% wa wananchi walikataa?
 
jana Gerson Msigwa kushatangaza Serikali inaendelea na Mkataba wa ukodishaji wa Bandari

kuna watu hawaamini maana walidhan utulivu wa Serikali hii ni ishara ya kuwaogopa

inanikumbusha ile mijadala na nyaraka za mahafidhina ya Kikomunist machawa ya Nyerere yaliyokuwa University of Dar es salaam miaka ya mwisho ya 1980s yaliyopinga kwa nguvu zote kuupiga chini Ujamaa, kile kimya cha Ally Hassan Mwinyi yakatafsiri anawaogopa na watambabaisha, hata Nyerere mwenyewe alikuja kujua kupitia gazeti la Mfanyakazi na uhuru aliishia kupiga makelele na kutukana kupitia kitabu chake maarufu cha Hatima yetu na Siasa za Tanzania
 
Serikali imetwangwa barua waraka na Maaskofu kupinga mkataba wa bandari. Ingawa Baraza hili haliko kisheria kufanya jambo la nchi kama hilo lakini limefanya hivyo baada ...
Zinatolewa kwa awamu zipi? Zitaje ili twende saw!!
 
Wakati wa Magufuli hukuona waraka wowote toka TEC? Umejaa huku JF.

Tatizo lenu mnaendeshwa na mahaba ya dini yenu, hamtaki mama yenu aguswe hata akikosea wazi, hilo haliwezekani, sio kwa Tanganyika hii ya leo.

Kama hamtaki aguswe, muondoeni ikulu muende nae Makunduchi halafu muone kama yupo atakayehangaika nae.
Wajinga hawa.
 
jana Gerson Msigwa kushatangaza Serikali inaendelea na Mkataba wa ukodishaji wa Bandari

kuna watu hawaamini maana walidhan utulivu wa Serikali hii ni ishara ya kuwaogop...
Maendeleo ya kwelikweli ya nchi yataletwa na Rais mpagani au asiyekuwa mkristo. Wakoloni na watesi wetu wamejifisha na kujibanza kwenye madhabahu ya makanisa. Dini hii waliileta wao hivyo wanajua Kwanini waliiteta.
 
Serikali imetwangwa barua waraka na Maaskofu kupinga mkataba wa bandari. Ingawa Baraza hili haliko kisheria kufanya jambo la nchi kama hilo lakini limefanya hivyo baada...
Kabla ya kuwashambulia Maaskofu wa kanisa Katoliki hebu waambieni viongoze wenu huko misikitini waache kujikomba kwa viongozi wa serikali.

Tuliwaona kipindi cha JPM sifiasifia ilikuwa hadi kwenye mikutano ya campaign. Kusifia ni sawa lakini kukosoa ni kuchanganya dini na siasa?

Kama shule na hospital za kanisa katoliki zinawauma na nyie jengeni za kwenu siyo kusubiri mjengewe hadi misikiti. Wivu umewajaa, subirini kuletewa tende na nyama za ngamia toka Uarabuni.
 
Wakati wa Magufuli hukuona waraka wowote toka TEC? Umejaa huku JF.

Tatizo lenu mnaendeshwa na mahaba ya dini yenu, hamtaki mama yenu aguswe hata akikosea wazi, hilo haliwezekani, sio kwa Tanganyika hii ya leo.

Kama hamtaki aguswe, muondoeni ikulu muende nae Makunduchi halafu muone kama yupo atakayehangaika nae.
Utaondoka wewe, Mama bado yupo sana
 
Maendeleo ya kwelikweli ya nchi yataletwa na Rais mpagani au asiyekuwa mkristo. Wakoloni na watesi wetu wamejifisha na kujibanza kwenye madhabahu ya makanisa. Dini hii waliileta wao hivyo wanajua Kwanini waliiteta.
Sio yataletwa na Rais Muislam mkuu?
 
Wakati wa Magufuli hukuona waraka wowote toka TEC? Umejaa huku JF.

Tatizo lenu mnaendeshwa na mahaba ya dini yenu, hamtaki mama yenu aguswe hata akikosea wazi, hilo haliwezekani, sio kwa Tanganyika hii ya leo.

Kama hamtaki aguswe, muondoeni ikulu muende nae Makunduchi halafu muone kama yupo atakayehangaika nae.
Mama yupo sanaaaa, yaani Mungu akipenda ni mpaka 2030, uhai, umri na afya vikiwepo

Pole sana, dawa ni kuvumilia tu, vinginevyo ni maumivu tu ya kujitakia
 
Wakati wa Magufuli hukuona waraka wowote toka TEC? Umejaa huku JF.

Tatizo lenu mnaendeshwa na mahaba ya dini yenu, hamtaki mama yenu aguswe hata akikosea wazi, hilo haliwezekani, sio kwa Tanganyika hii ya leo.

Kama hamtaki aguswe, muondoeni ikulu muende nae Makunduchi halafu muone kama yupo atakayehangaika nae.
Wewe utaishi na maumivu mpaka siku ya mwisho ya Rais SSH pale ikulu. Una bitterness mbaya, utakuwa mtu mmoja mdini sana lakini unaona udhaifu wa wengine bila ya kujitazama mwenyewe kwanza.
 
Serikali imetwangwa barua waraka na Maaskofu kupinga mkataba wa bandari. Ingawa Baraza hili haliko kisheria kufanya jambo la nchi kama hilo lakini limefanya hivyo baada ya kujiridhisha kuwa serikali, Bunge na mahakama wametenda kosa kwenye mkataba huu. Waraka kama huu ulionekana tena wakati wa hoja ya kuwepo kwa kadhi Tanzania.

Mimi huwa najiuliza maswali kuhusu nguvu hizi za Maaskofu kwanini hazikutumika kupinga Mwl. Nyerere kuifuta serikali ya Tanganyika, kutaifisha baadhi ya shule zao za kanisa kuwa za serikali, wala kupinga nchi kutaifisha mali za serikali kama nyumba, mashirika ya umma na migodi yetu.

Mbona kama waraka hizi zinatolewa zaidi kwenye awamu fulanifulani TU?
Zimetoka nyaraka nyingi sana kuhusu bandari.Naona huu wa Maaskofu una nguvu sana.Yaani haupoi.
Au kwa kuwa maaskofu walisali na kufunga kabla ya kuutoa?
 
Serikali imetwangwa barua Waraka na Maaskofu kupinga mkataba wa bandari. Ingawa Baraza hili haliko kisheria kufanya jambo la nchi kama hilo lakini limefanya hivyo baada ya kujiridhisha kuwa serikali, Bunge na mahakama wametenda kosa kwenye mkataba huu. Waraka kama huu ulionekana tena wakati wa hoja ya kuwepo kwa kadhi Tanzania.

Mimi huwa najiuliza maswali kuhusu nguvu hizi za Maaskofu kwanini hazikutumika kupinga Mwl. Nyerere kuifuta serikali ya Tanganyika, kutaifisha baadhi ya shule zao za kanisa kuwa za serikali, wala kupinga nchi kutaifisha mali za serikali kama nyumba, mashirika ya umma na migodi yetu.

Mbona kama waraka hizi zinatolewa zaidi kwenye awamu fulanifulani TU?
Umeandika "....wala kupinga nchi kutaifisha mali za serikali kama vile nyumba, mashirika ya uma, migodi yetu...."

Nchi inataifishaje mali za serikali?
Japo niko nje ya TEC, naona Wana HAKI kutoa waraka kwa waumini wao wakati wowote. Maudhui ya huo waraka ndiyo kitu muhimu, siyo historia ya awamu za uraisi na nyaraka za TEC.
Suala la kuwapa DP W ukiritimba (monopoly) wa bandari zote za Tz baharini na maziwani na udhibiti wa"logistics" zote nyeti kwa uchumi sio la kuchukulia kiwepesi wepesi kwa sababu tu ya kuwepo bunge la chama kimoja.
 
Back
Top Bottom