Maaskofu Katoliki mnawaambia vijana wa Kitanzania waliopo Italia warudi nyumbani wakimaliza masomo, mna ajira za kuwapa?

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
13,824
18,568
Maaskofu Katoliki wamemaliza hija Roma na pia mkutano wao na Baba Mtakatifu.

Baada ya hapo wamekutana na watanzania waishio Italia hasa katika jiji la Roma wakiwepo wanafunzi.

Wakiongozwa na askofu mkuu Nyaisonga, maaskofu wamewaasa vijana hao kurudi nyumbani Tanzania mara wamalizapo masomo yao.

Je. maaskofu mnajua kadhia ya ajira iliyopo Tanzania kwa sasa? Au mna ajira za kuwapa hao wasomi wetu pindi warudipo au baadaye mtawaambia ombeni Mungu atawasaidia?
 
Warudi tu, we huoni madhira wanayopata wale waafrika waliokuepo Ukraine na Urusi? Baada ya masomo warudi bongo kuhusu ajira zipo tu

Their safety is more important maana huko ni kama mkimbizi hauna haki/guarantee 100% ya kua protected ikifika vipindi vya emergencies
 
Yeah, Maaskofu wanao uhalali wa kusema hivyo kama viongozi, lakini kwa Watanzania waishio Italia ambao ndo walikuwa kwenye kikao hicho wazingatie usemi "Akili za kupewa, ongezea na za kwako". Nimemaliza.
 
Ni hisia tu hizi.
Warudi tu, we huoni madhira wanayopata wale waafrika waliokuepo Ukraine na Urusi? Baada ya masomo warudi bongo kuhusu ajira zipo tu

Their safety is more important maana huko ni kama mkimbizi hauna haki/guarantee 100% ya kua protected ikifika vipindi vya emergencies

Sitaki kutia neno, maana komenti yako ipo kihisia zaidi.
 
Aah ndo hivo mkuu, kama Wako assured na safety wabaki waendelee na maisha ila kama ni otherwise warudi tu makwao ,
Je, huko makwao ndo wako assured na safety? Mbona inaonekana ni kama umeshasahau kwamba usalama wako unaanza na ww mwenyewe? Kumbuka na ya huku e.g. juzi kati hapa tulikuwa na matukio Kibiti, Mtwara na yale ya watu kutekwa au kupotea, viroba vyenye miili ya watu ufukweni, bila kusahau magenge ya "panyarodi" n.k. n.k. Utauficha wapi uso wako?
Ni kheri uzingatie tu kwamba Maisha ni popote.
 
Mkuu atleast upo nchini kwako unapewa first priority ya protection

Kasome Civics kidogo, afu nakupa reference ya Ukraine-Russia war
 
Mkuu atleast upo nchini kwako unapewa first priority ya protection

Kasome Civics kidogo, afu nakupa reference ya Ukraine-Russia war
Mhh, mkuu;Unasema nchini kwako unapewa first priority! ??? Kwani wale wakimbizi ndani ya makambi yaliyo Kigoma Tz. hawakutokea nchini kwao?
Je, kinachoendelea huko Sudan hakijatoshea kukupa mwanga kuhusu hoja yako eti uko nchini kwako na utapewa first priority ya protection? Hebu kumbuka kinachoendelea Congo DRC , basi walau kumbuka kwa jirani yetu Kenya na Alshabab. Usijidanganye; likitokea la kutokea hakuna cha eti umesoma na kuielewa civics, una degree cjui vyeti gani - unatimka na unatimkia unakokujua mwenyewe.
Vita baina ya Ukraine na Urusi wapo wakimbizi zaidi ya 700,000(laki saba) ambao wengi wao ni vijana wasomi wa Urusi na wengine ni matajiri wameikimbia nchi yao Russia na kujitafutia hifadhi huko Poland, Belarus, Latvia, Slovakia na wengine wamefikia hadi Ufaransa, Ujerumani n.k.n.k. Sasa kwa Wale waliomini (kama ww) eti wapo na ni nchini kwao ndo hao wanakamatwa kwa nguvu (mobilised)na kupelekwa vitani frontline hata bila ya mafunzo ya kijeshi ya kutosha - na wanauawa wengi sana.
 
Hivi ni Kwa nini huyo kiongozi wenu hua mnamuita mtakatifu ?🤔🤔🤔
Kwani kuitwa mtakatifu ni kosa au ni kero kwako? Ni ruksa hata ww unaweza tu kujiita mtakatifu hakuna shida na wala sio tusi na wala hutoshtakiwa mahakamani.
BTW: Anaitwa mtakatifu kwa nafasi aliyonayo ndani ya Kanisa Katoliki.
Wewe kama ikikupendeza unaweza pia usimwite mtakatifu. Uwe na amani.
 
Back
Top Bottom