Maandamano yanayoendelea USA ni sawa na kufunga goli baada ya kipenga cha mwisho

Allan8

JF-Expert Member
Sep 18, 2014
235
703
Poleni na harakati za kila siku. Ni matumaini yangu kuwa nyote mu wazima wa afya.

Basi kama kichwa cha habari kilivyo mimi binafsi ninaona marehemu hakutendewa haki. Wakati jamaa amewekewa goti juu ya shingo yake na askari Nina imani kulikuwa na mashuhuda mbalimbali eneo la karibu.

Je, walishindwa vipi kumsaidia jamaa wakati ule akiwa bado hai?

Najua walikuwa wanachukua picha za tukio lile.

Baada ya kufuatilia baadhi ya sheria za vyombo vya ulinzi niligundua kuna moja inasema ni marufuku kumbugudhi polisi akiwa amemuweka mtu chini ya ulinzi.

Pia, swali linakuja, waliogopa kufanya vile kwa sababu ya sheria ile, Je ujasiri wa kuandamana hadi kuchoma kituo cha polisi waliupata wapi? Nahisi walitakiwa wafanye vile jamaa akiwa hai/hajafa bado ingekuwa nzuri zaidi.
Binafsi naona wameamua kukata pua ili kutengeneza sura. Nawasilisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…