Cash Generating Unit
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 13,284
- 39,513
Dunia inazidi kushuhudia mabadiliko taratibu huku macho ya wengi yakielekezwa Ufaransa ambapo waandamanaji wakizidi kuongezeka kwa kasi.
Baada ya Macron kupandisha umri wa kustafu kutoka 62-64 imezua maandamano lakini inasemekana na kupanda kwa gharama za maisha kumepelekea watu wazidi kuandamana.
Tunashuhudia jinsi polisi walivyo makatiri wakiua na kuwatesa raia ambao wanadai haki zao huku media zao zikiwa kimya kama hawaoni kinachoendelea. Hii ndo demokrasia wanayotuhubiria?
Maandamano ya Iran west walikua bega kwa bega na waandamanaji lakini sababu imetokea kwenye bustani yao wapo kimya hata haki za binadamu wamesahau.
Miji ya Ufaransa karibu yote maandamano yameshika kasi sana kuna mapigano baina ya raia na polisi huku wengine wakimtaka Macron kujiuzulu.
Acha tuone hatima ya Macron maana kila siku hali inazidi kuwa mbaya. Mlitamani sana haya mambo yatokee Russia ila kibao kimegeuka.