Maandamano ya Wapenda Ufisadi yamedorora | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maandamano ya Wapenda Ufisadi yamedorora

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SG8, Mar 16, 2011.

 1. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,198
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Nimewasikilia na kuwaangalia wanaojiita wapenda amani. Nimegundua kumbe ni watu wwachache tu ndio wanaopenda ufisadi wa CCM. Nawashauri CDM wasiwajibu hao vibaraka ila wao iwe "Chadema mwendo mdundo, fichua mafisadi". Mwaka huu tutaona mengi bali huo ni mwanzo wa mapambazuko
   
 2. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  nimeyaona kupitia tbc1 daaaaa, kweli watanzania wameamka... hongera sana wana dar...
   
 3. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0


  CCM bado wanadhani watu wako zama zile za "inama nikupe pipi" hata kama kiuno kinauma......

  People now are beyod where they are, far beyond....hatuangalii tena sura za watu, tunaangalia njaa zetu
   
 4. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Hakukuwa na watu "wenye akili timamu". Ni wapigadebe wa manzese, wapuuzi flan "wa ccm", ccm B na vijana waliokuwa kazini kuuza maji, lambalamba nk. Nimegundua tu dawa ya Babu wa Loliondo ina nguvu si mchezo!? Mrema amepata nguvu sana. Najipanga nimpeleke anko.
   
 5. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  walisema ni maandamano ya vijana wapenda amani lakini nimeona vizee vimejaa..halafu hik chama makao makuu yake yako wapi maana mimi ndiyo juzi nimekisikia
   
 6. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  wangekuwa wanajua habari yao imekwisha wasingejiaandamisha. Tatizo hawajitambui hata chembe
   
 7. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kama dar wamepata watu kiasi hicho wang'e kuwa mikoani wangekomea viongozi...
   
 8. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #8
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  LICHA YA ADUI HATARI ITAKAYOIUA CCM KWA HARAKA ZAIDI NDANI KWA NDANI HIVI KARIBUNI, CHAMA HIKI KIKO MBIONI KUJITWISHA MIZIGO MIPYA KUMBEBA LOWASA NA HASA KUFANYA MAUAJI YA SAUTI PINZANI KISIRI KUSAFISHA NJIA

  Kama uliwahi kufikiria kwamba CHADEMA ndicho adui mkubwa itakayoiua CCM basi kumbe kweli huelewi kabisa siasa za taifa hili zilivyo lakini hivi sasa kundi dogo ndani ya CCM linaloshikilia uhai wa chama hiki kiko mbioni 'KUSAFISHA NJIA KWA NAMNA YOYOTE ILE mmoja wao kushaka dola 2015.

  Kwa wadadisi wa mambo, adui mkubwa zaidi na wa kutisha ajabu tayari yuko chumbani kwao CCM na hivi karibuni italipuka kuliko KINU CHA NYUKLIA CHA JAPAN na kutuma mionzi itakayoifuta kabisa CCM bukia chama cha upinzani namba 4 baada ya NCCR-Mageuzi hapa nchini.

  Kwa kugusia tu kwa uchache; adui namba moja na hatasri mno hadi hivi, kwa haki kabisa kwa misingi ya kichama walichojiwekea, ni kwamba kule Wa-Tanzania Visiwani wanakiona CCM kama Chama kilichowasaliti kushika dola baada ya Mhe Benjamin Mkapa.

  Hakika jambo hili la USALITI WA CCM KWA WATANZANIA VISIWANI ni tishio kubwa hivi sasa ambapo majina zaidi kutoka Bara yaendelea kutajwa KUMRITHI Mhe Kikwete ambaye naye kwanza hata hatima yake bado haiko wazi kwa umma wa Tanzania.Kwa jinsi mambo yalivyo nchini itakavyolipua Naona baada ya CCM kuwatapeli Wa-Tanzania Visiwani nafasi ya kugombea Urais, katika ule mpango wao maalum wa SIASA ZA KUKABIDHIANA UONGOZI WA NCHI KWA ZAMU KWA WATOTO WA WAKUBWA tu Bara na Visiwani.

  Kitendo cha kikundi fulani kujipenyezea fedha haramu kupitia kwa akina Rostam Aziz na Edward Lowasa katika dakika za majeruhi kushawishi maamuzi kumtosa Mhe Salim Ahmed Salim (ambaye alipendwa sana bara na kuaminiwa mno na CCM-Mwalimu Nyerere) kule Dodoma, ndipo jini dume lenye vichwa viwili lilipozaliwa na kuleta salamu za maangamizi kwa hiki chama kilichowahi kupata umaarufu wa miaka mingi sana na kuaminiwa wa wengi nchini.

  Miongoni mwa hizo salamu ni pamoja na (1) Wana-Mtandao badala ya Wana-CCM (ambao nao walikujakugawanyika mbele ya safari na kuwa (i) Wanamtandao Walaji (MAFISADI WA HIVI LEO) na Wanamtandao Waliwa ambao nao mahasibu yao mazito na yanayo nuka mno tutakuja kuyaelezea siku nyingine humu, (2) Wana-CCM Bara ambao lao ni kuwatumia baadhi ya Wana-CCM maswahiba kutoka Visiwani wakiwachezesha kama mchezo wa CHESS au DRAFT KISIASA ili kuzuia Wa-Tanzania wa kawaida Bara na Visiwani kuwa na maamuzi yoyote juu ya nani awaongoze isipokua tu maamuzi yote yatatoka siku zote kwa hii CCM Bara tu kwa sura zima ya Jamhuri yetu ya Muungano Tanzania.

  Sasa kwa ujio wa CHADEMA na kuendelea kupendwa sana kwa chama hiki na azma yake ya KURUDISHA UONGOZI WA NCHI MIKONONI MWA WANANCHI WENYEWE kote Bara na Visiwani, na haya madai Moto Moto ya sisi Vijana kutaka Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi kote ndani ya taifa letu tayari zimekua ni mwiba mchungu katika ngozi ya kikundi hiki cha WAJANJA WACHACHE Wana-CCM Bara ambao mpaka hivi sasa, kwa mujibu wa habari nyeti za ndani sana chumbani mwao, kila ramani ya kisiasa wanalolichora linagoma kabisa, fedha walizokwisha wekeza kwenye juhudi hizi zote Bara na Visiwani zakumbwa na hatari za wazi mno na migawanyiko kuongezeka kila kukicha kati yao.

  Hata nako ndani ya kikundi hicho cha hao Wajanja wachache Wana-CCM kumeibuka nako Migawanyiko mikali ya KI-KANDA kwa namna ambayo hata juhudi gani zifanyike hakuwezekani kupatanishwa kitu hata wakafanya kazi kwa pamoja.

  Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani ya CCM katika ujumla wake, hali si shwari hata kidogo mle!! Wapo hata wale ambao, kwa ufinyu tu wa mawazo, wamefikia mahala wamependekeza MAJINA 15 ya baadhi ya watu mashuhuri na tishio kwa maslahi yao KUUAUA. Lini wauawe na kwa MTINDO GANI usioweza kuleta tafrani kwa kile wanachokiita 'Tishio la Nguvu ya Umma' kutokuweza kuwakumba.

  Japo tatizo letu Wa-Tanzania tuliowengi ni mpaka tushikishwe jambo kiganjani ndio tuamini na wakati mwingine kugutuka kukiwa kumechelewa sana, miongoni mwa HAYO MAVUNO YA MIKONO YA KI-SHETANI tayari wameorodheshwa baadhi ya vinara wa kupinga madhambi ya CCM kwa njia mbali mbali nchini.

  Kati ya watu wanaolengwa wamo (i) baadha ya viongozi tishio kwa kinyang'anyiro cha kiti cha urais 2015 waliomo ndani na nje ya hicho kikundi cha Rostam Aziz na Edward Lowasa. Pia, (ii) wapo baddhi ya viongozi wa serikali za wanafunzi nchini, (iii) baadha ya Wana-JF ambao wametajwa kama 'wakorofi na waharibifu', (iii) baadhi ya viongozi wa dini katika kanda fulani ambao wameelezewa kuwa na 'vinywa pana' na kuonekana kukisaidia CDM, (iv) wafanyabiashara wanaohofiwa kukifadhili CHADEMA hivi sasa na (v) na baadhi Wanataaluma wanaoonekana kujitolea kukisaidia CDM ki-mikakati ambayo hadi sasa yaelezewa KUKIDHOOFISHA MNO hiki chama tawala.

  Sasa chama hiki chaonekana kubuni (1) mkakati mpya wa UONZOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA kukabidhiwa kwa zamu ile ile ila safari hii ni NDANI KWA NDANI TANZANIA BARA na vile vile ni (2) kwa KUZINGATIA AMA URAFIKI, UJIRANI AU UDINI kufanya hivyo.

  Hata hivyo nako mambo si yenyewe baada ya wale wafadhali wa Uarabuni (Libya, Misri na Iran) nazo kukumbwa na matatizo kibao, yale yanayoendelea na yale ambayo yatalipukia kwao miezi michache ijayo; kikundi hiki ndani ya CCM kimechanganyikiwa kupindukia kwani kwani ufadhili wao hauna uhakika tena huku wananchi tukiendelea kulishikilia bando DOWANS na mianya mingine itakayotumika kuchota kodi zetu kuyatekelezea haya yote.

  Dawa ya yote haya wanayopangwa kutekelezwa kwa mikono ya giza ni (1) kuhakikisha kwamba kila mmoja wetu anageuka kuwa mlinzi wa mwenzie dhidi ya juhudi hizi hatari, (2) kusimama kidete kwa KUSISITIZA Katiba Mpya ya Wananchi na Tume Huru ya Uchaguzi kupitishwa Bungeni mwezi ujao, (3) kuendelea kuhakikisha kwamba UTEUZI WA JOHN MIMOSE CHEYO kushika tena ile kamati kule bungeni haiwi tena kichochoro tena cha Mafisadi kujichotea fedha kununulia kura na kutekelezea mambo machafu huku Cheyo akijifanya hajaona kitu kwenye vitabu vyetu!!
   
 9. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kwa kweli ilikua aibu nimeona na vitoto vilikuwepo watu walikuwa wachache hadi tbc walikuwa wanaona aibu kuonesha umati wakabaki kuonesha wazungumzaji tu.
   
 10. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #10
  Mar 16, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,198
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Mkuu nakubaliana na wewe. TBC1 wameishia kumwonyesha Mrema na wenzie. nchi hii mazingaombwe matupu. hata kule Kigoma watu wanahesabika tu kwenye mikutano ya wale wenzetu wa"upinzani B"
   
 11. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #11
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Kumbe leo kulikuwa na maandamano!
   
 12. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #12
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Haswaa tena yamefanyika kwenye jiji lenye wakazi takribani 5 mil lakini ukiyaona maandamano yenyewe hata tung'efanya maandamano kwenye ubalozi wa nyumba kumi tunge washinda....
   
 13. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #13
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,918
  Trophy Points: 280
  Wale walioandaa tamasha wachukulie kuwa hili ni fundisho,hata watu wakijitokeza kwa wingi siku ya tamasha lao haitakuwa kwasababu ya ujumbe wao bali burudani tu.(This is olny if tukio hili ni tofauti na lile lililoandaliwa na clouds na wengineo.)
   
 14. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #14
  Mar 16, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Ndo kwanza nafahamu habari hii, kumbe waliandamana?
   
 15. only83

  only83 JF-Expert Member

  #15
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Wakome na watukome watanzania...
   
 16. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #16
  Mar 17, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,269
  Trophy Points: 280
  Jamani hivi mimi niko Dar es salaam ipi? mbona maandamano ya kanda ya ziwa tulikuwa tunapata taarifa ya mafanikio yake na picha? au mtoa mada aliona msafara wa watu wanaoelekea makaburini kuzika yeye ndio akazani ni maandamano?
   
 17. Gerald

  Gerald JF-Expert Member

  #17
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  MWENYEKITI wa chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustino Mrema, amewaonya Watanzania wasiichezee amani iliyopo kwa kuwa ikitoweka, watajuta.

  Akizungumza na umati wa vijana, Dar es Salaam jana, Mrema aliyekuwa mgeni rasmi katika mkutano huo, alisema dalili zilizopo za kuvunjika amani, ziliwahi kutokea katika baadhi ya nchi ambazo sasa hazikaliki.

  Katika mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya Bakhresa Manzese, alisema dalili hizo, ikiwemo ya maandamano yanayodaiwa kuwa ya amani, ziliwahi kutokea katika nchi kama Madagascar na Somalia ambako sasa hakutawaliki.

  Huku akishangiliwa na vijana hao katika mkutano huo wa amani uliokuwa na kaulimbiu: ‘Amani yetu bado tunaipenda’, Mrema alitoa mfano wa vurugu zilizotokea nchini Madagascar zikiongozwa na kiongozi wa upinzani, Andry Rajoelina ambazo zimeifanya nchi hiyo isitawalike.

  Kwa mujibu wa Mrema, Rajoelina alitumia udhaifu na matatizo ya wananchi wakaanza maandamano kama yanayofanyika Tanzania wakafanikiwa kumtoa Rais wa nchi hiyo, Marc Ravalomanana madarakani lakini sasa kuna vurugu tupu.

  Alisema matukio kama hayo pia yalifanyika Somalia ambako sasa ni zaidi ya miaka 10 hakuna serikali na kuongeza kuwa hata Zanzibar, CUF walianza hivyo hivyo kwa maandamano na matokeo yake watu wakafa na wengine kupata elemavu wa maisha.

  Mrema alisema wakati watu wakiendelea kuishi na ulemavu huku wangine wakiwa wamepoteza ndugu zao huko Zanzibar, leo kiongozi wa upinzani, Maalim Seif Sharif anakula sahani moja na Rais Mohamed Shein.

  Aliwashangaa wanaosema kuwa amenunuliwa na CCM kwa kutetea amani ya nchi na kufafanua kwamba tatizo lililopo mtu akitetea nchi yake na kupingana na baadhi ya fikra za watu, anaonekana kibaraka.

  Alitamba kwamba yeye ni kiongozi wa upinzani aliyewahi kupata kura nyingi kuliko kiongozi yeyote wa upinzani nchini mwaka 1995, alipopata asilimia 28 ya kura zote na kuongeza kuwa, wakati akibezwa chuo kimoja cha Afrika Kusini, kimemtunukia Shahada ya Heshima ya Uzamivu (PHD).

  Katika mkutano huo ulioandaliwa na Kamati ya Vijana Watanzania Wapenda Amani (KVT), Rais wa Vyuo Vikuu nchini, Mathias Kipala na Mwenyekiti wa chama cha Updp, Rajab Mrisho, walilaani maandamano ya chama cha Chadema na kuonya hali inaweza kuwa kama katika ajali za mabomu za Gongo la Mboto na Mbagala.
   
 18. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #18
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Picha hamna? Hata humu jamvini hakuna aliyeshiriki au?
   
 19. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #19
  Mar 17, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  kwani si nilisikia haya maandamo yamepigwa stop na mandagu kisa yataleta msongamano wa magari...tena kulikoni??
   
 20. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #20
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Mrema alisharudi kutoka Loliondo?
   
Loading...