Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 97,072
- 136,485
Kama UKUTA wakinywea na mwishowe kutokufanya hayo maandamano yao ambayo wamepanga kuyafanya hiyo tarehe 1 mwezi ujao, basi mheshimiwa MWENYE ENZI, MTUKUFU rais Magufuli atakuwa amepata ushindi mkubwa sana.
Hayo maandamano yasipotokea atakuwa kafanikiwa kuwatisha wananchi katika kutofanya yale ambayo hayampendezi yeye.
Na huu ndo utakuwa mwanzo tu. Huko mbeleni ikitokea kuna jambo ambalo halimpendezi yeye binafsi basi hatosita kutumia vyombo vya dola kuwatisha watu ili waache kufanya walichokuwa wamepanga kufanya.
Hiyo ndo Tanzania mpya. Tanzania ya MWENYE ENZI, Mtukufu rais John Pombe Joseph Magufuli [nahisi pia tutalazimishwa kuyatumia majina yake yote manne la sivyo wataokiuka watatafutwa na kuadhibiwa, hata kama wapo mitandaoni].
Na nyie wachora vikatuni nahisi dawa yenu inakorogwa huko maabara. Kama mkiendelea kumchora vibaya MWENYE ENZI, MTUKUFU rais John Pombe Joseph Magufuli basi siku zenu zinahesabika.
Yakiwatokea ya kutokea msije lalama eti sikuwaambia! Shauri yenu.
UPDATE:
Raundi 1.
Magufuli 1, UKUTA 0.