Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,050
- 79,395
Hamjambo!
1. Ingawaje ni Siku iliyobeba kumbukumbu zenye huzuni, maumivu na damu za watu. Lakini pia ilikuwa Siku muhimu kwa taifa letu.
2. Siku ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa miaka na miaka tangu mababu zetu. Walikuwa wakiisubiri Siku Ile ambayo ingefuta aibu, manyanyaso, kejeli na uteja ambao tuliushuhudia kwa miaka nenda Rudi.
3. Hakuna kauli inayoumiza kama ukisikia taifa lako linadharauliwa ma mataifa mengine. Watu wako wanadharauliwa na watu wa mataifa mengine.
4. Oooh! Watanzania ni waoga! Hivi unajua maana yake hiyo? Taifa lenye mamilioni ya wanaume, lenye wasomi, lenye majeshi ati linaambiwa watu wake ni waoga. Unajua maana yake?
5. Ukiambiwa wewe ni muoga inamaanisha huwezi kujipigania, huwezi kujitetea, unaogopa. Mtu yeyote anaweza hata kukushika makalio hapo. Ukabaki unatiatia huruma na kusema unamuachia Mungu. Ujinga tuu.
5. Wanaweza kuja watu watano wageni wa mataifa mengine wakaonea watanzania na watanzania wakashindwa kufanya chochote. Uoga! Uoga huleta wanafiki nafiki. Uoga huleta lawama, malalamiko.
6. Oooh! Hao unaoongoza ni wafu. Dadeki! Yaani Sisi ni wafu. Unajua hizo kauli zimekuwa zikizunguka Sana tangu tukiwa watoto. Mbaya zaidi mpaka wazee wetu wanahadithia hizo kauli zimeanza mpaka wakati wa Baba wa taifa.
7. MO29 ilikuwa Siku ya Watanzania kufuta uteja, kejeli na dharau. Na kuzaliwa kizazi kimya, taifa jipya, mtazamo mpya wa ujasiri na taifa ambalo watu wake wanaweza kujitetea, kupambana hata kama hawana silaha.
8. Ni Siku ambayo tuliokuwepo Zama hizi tutajivunia katika maisha yetu. Hata vizaI vijavyo vitatupa heshima.
9. Sasa tunalo taifa. Sasa tunaweza kusema tuna nguvu KAZI. Tunavijana.
10. Hii ni kiashiria elimu tuliowapa vijana inafanya KAZI. Vijana wanajitambua. Wanaweza kulinda taifa lao na kulipigania.
11. Vyombo dola na usalama sasa vinaweza sasa kujitamba kuwa vinalinda watu hasa. Watu wenye utambuzi. Halilindi watu waoga tena kama ilivyokuwa inasemwa na mataifa mengine.
12. Ndugu zangu, Upole na uoga sio sifa njema kwenye dunia ya Leo. Ukiambiwa mpole kwenye dunia ya Leo wanamaanisha umwoga na unaonewa.
12. Kwa sasa mataifa kama Kenya Kimya! Watani zetu Wakenya wamebaki kutusimanga kwa kingereza Jambo ambalo halituumizi lakini utani wao uliokuwa unatuumiza ni kutuona sisi ni mang'ombe, waoga, wafu tusiojitambua.
13. Now we have people.
14. Nakumbuka MO29 asubuhi Mzee mmoja mwanaccm alinikuta nimekaa kijiweni. Alikuwa anawasiwasi Sana.
15. Akaniuliza hivi watu watatoka? Nikamwambia Sijui. Nikamwambia lakini wewe si no CCM. Akanijibu ndio na kura nimepiga. Akinionyesha kidole chake.
16. Nikamwambia SASA kwa nini unataka maandamano? Akaniambia huku machozi yakimlenga lenga. Akasema, tunatukanwa Sana. Miaka mingi tunaonekana Sisi waoga. Mataifa mengine yanatudharau.
17. Kiukweli alinifanya nishangae. Nikamtazama nikiwa nimetekewa na jibu lake. Sikutegemea kabisa. Akaongeza, natamani vijana watoke waondoe laana ya sisi wazee wao"
18. Niwaambie nilijihisi kulia. Aliongea kwa hisia Sana. Hapo ni kabla ya muda wa tukio.
Niligundua kuwa watu wengi Siku Ile walitamani maandamano yawepo. Wengi. Lakini sio kwa fujo, uharibifu na mauaji.
19. Walitaka kuonyesha kuwa Watanzania sio Wafu.
Walitaka kuonyesha Watanzania na sisi sio waoga. Tunaweza kutetea haki na kuelezea mambo yetu wenyewe.
20. Hicho ndicho baadhi ya wazee, wamama walikuwa na mtazamo huo.
21. Binafsi nilimuomba Mungu sana Siku zile. Na isingetokea ningekuwa disappointed.
22. Ingawaje wapo waliokufa, waliumizwa, walioharibiwa Mali zao, waliobaki yatima, wajane na wagane.
23. Lakini Siku ile isiwe Siku ya kukumbukwa kwa kushindwa au kuleta mpasuko katika nchi. Iwe Siku ya kukumbukwa kwamba taifa letu lilizaliwa upya.
24. Roho mpya na fikra mpya ilizaliwa.
25. Matusi, kejeli, na dharau zilikufa na kukomeshwa rasmi. Kwa sasa sisi ni taifa lenye heshima. Watu wanaoheshimiwa mpaka na majirani zetu.
26. Tusiliangalie Jambo hili katika Mrengo Hasi tuu. Bali tuangalie na Chanya pia.
27. Nafahamu bado kuna mambo ambayo ni tatizo ikiwemo upatikanaji wa Haki kwa baadhi ya maeneo hasa haki za wanasiasa.
28. Najua hatuwezi kutatua matatizo yote kwa usiku mmoja.
Hatuwezi kuwa waadilifu kwa Siku au mwaka mmoja. Kila Jambo linawakati wake.
29. Kama tumeipata heshima na kuondoa kejeli na dhihaka na dharau zilizodumu kwa miongo na miongo. Na Leo hii tunaheshimika kwamba Watanzania sio Wafu tena, sio waoga tena. Ni Imani Yangu kuwa hata haya matatizo mengine tunayoyalalamikia yataondoka.
30. Sisi sio waoga tena. Sisi sio Wafu. Sasa no taifa la watu wenye nguvu, ujasiri na maamuzi magumu kwa maslahi ya vizazi vyetu.
Nimemaliza, mwenye swali anaweza kuuliza.
TaikonMaster
Kwa sasa, Kawe Ukwamani, Dar es salaam