Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,468
- 23,745
Maswali
1. Je waliwatoa hao masheikh siku hiyo?
2. Sheikh Kassim ilikuaje akakosekana kwenye maandamano aliyoyanzisha akawa arusha akielekea Nairobi "kwenye matibabu"?
1. Je waliwatoa hao masheikh siku hiyo?
2. Sheikh Kassim ilikuaje akakosekana kwenye maandamano aliyoyanzisha akawa arusha akielekea Nairobi "kwenye matibabu"?
Mwaka wa 1993 ulikuwa mwaka mzuri sana kwangu kwani katika miezi 12 nilikuwa nimesafiri mara tatu tena ukichukulia kuwa mwaka wa 1991/92 nilikuwa Uingereza.
Nilikwenda Harare na ulikuwa mwezi wa Ramadhani.
Nilikaa Harare kwa majuma matatu na nikafika hadi Bulawayo.
Nikaenda Lusaka Zambia.
Niliporudi nikaenda Ufaransa nikawa Le Havre na Paris na safari ya kurudi nikapita London nikasali Eid Kubwa Regent Park Mosque hapo London kisha nikaenda Cardiff nikarudi Dar es Salaam.
Wakati huo Bunge liko Karimjee linaunguruma na sakata la Rais Mwinyi kuruhusu Zanzibar kuingia Organisation of Islamic Conference (OIC) na aliyehusika alikuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Ahmed Hassan Diria.
Barua za Kiuchungaji zinashambulia serikali ya Rais Mwinyi pamoja na magazeti yote hata yale ya Chama na Serikali.
Rais Mwinyi akajikuta hana wa kumtetea ila Sheikh Kassim bin Juma Imam Mkuu wa Msikiti wa Mtoro Mwinyi Mangara na ndani ya serikali akifarajiwa na Prof. Kighoma Ali Malima.
Hotuba za Ijumaa za Sheikh Kassim kwenye membar ya Mtoro zilitikisa nyoyo za Waislam na serikali nzima.
Siku ya Ijumaa msikiti unajaa hadi nje kufikia Mtaa wa Livingstone.
Waziri wa Mambo ya Ndani na Makamu Waziri Mkuu alikuwa Augustine Mrema.
Kulikuwa na makaratasi ya "uchochezi," yakimwagwa misikiti yote ya Dar es Salaam yaliyokuwa yakiandikwa na "waandishi wasiojulikana," yakijibu Barua za Kiuchungaji.
Wachina wana msemo, "May you live in interesting times."
Hizi nyakati zilikuwa za kipekee kabisa hazikupata kutokea hata wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika.
Hii safari yangu ya Ufaransa ilikuwa imenifanya nipitwe na mengi ya mjini.
Niliporudi nikaenda Zanzibar kushughulikia mambo fulani kuhusu OIC mimi na mwenzangu mmoja.
Tulipokuwa ndani ya chombo tunarejea ndiyo tukapata taarifa kuwa Waislam wamevunja mabucha ya nguruwe baada ya sala ya Ijumaa.
Rais Mwinyi kwa hofu akasema wale waliovunja mabucha ya nguruwe "nguvu za dola ziwaangukie."
Hiki ndicho kilichokuwa kinasubiriwa.
Usiku mmoja hadi kufika asubuhi masheikh na wahadhiri wa Kiislam wakakamatwa.
Waislam wakahamaki taarifa ikatoka kuwa wakutane Msikiti wa Mtoro kujadili kuwatoa masheikh walipokuwa wamewekwa rumande Central Police.
Katika kikao kile cha Mtoro siku ya Jumapili asubuhi msikiti ulijaa vijana hakuna sheikh hata mmoja aliyehudhuria.
Allah amenijaalia kuona kwa macho yangu matukio makubwa katika historia ya Waislam wa Tanganyika.
Mjadala ulikuwa mkali vijana ndani ya msikiti wakidai kuwa uamuzi wowote utakaofikiwa siku ile utoke kwenye Qur'an na Sunna hapatakiwi rai ya mtu binafsi.
Kikao hiki bila kuuma maneno kilikuwa kikao cha vita.
Sijapata kuona hamaki kwa Waislam kama niliyoshuhudia siku ile.
Ndipo Sheikh Waziri Ramadhani akasimama na kusema, "Ndugu zangu Allah leo ametuletea mtihani kutuangalia kama tunaweza kusimama kuipigania dini yake.
Kama dhulma tumeshafanyiwa sana ifike mahali tuseme basi kwa kukamatwa viongozi wa Waislam ni dharau ya juu kabisa dhidi yetu.
Kila unachokiona duniani kinamtumikia Allah basi ndugu zangu tutokeni twendeni Central Police tukawatoe masheikh zetu."
Hapo ndipo yalipotokea maandamano ya kwanza ya Waislam na yalipofika Mnazi Mmoja katika hali ya jua kali ghafla wingu likatanda na mvua ikaanza kunyesha.
Maandamano yalipofika Clock Tower askari wa FFU walikuwa wanawasubiri waandamanaji hapo mapambano yakaanza.
Mabomu mengi yaliyopigwa pale moshi wake ulipeperushwa na ule upepo wa mvua.
Milango ya Central Police ambayo daima haifungwi ikafungwa kwa kuhofu ule umma ungeweza kuingia hadi ndani ya selo za polisi.
Waislam wengi walikamatwa na kufunguliwa mashtaka.
Nahitimisha kwa kusema kuwa wakati haya yanatendeka Sheikh Kassim alikuwa Arusha akielekea Nairobi kwenye matibabu.
Hii ilikuwa "turning point," katika maisha yake kwani yeye alikuwa karibu sana na serikali na iliwashangaza wengi kumuona ameigeukia.
Kama si yeye kufanya vile na kusimamia haki Sheikh Kassim Jums angepita dunia hii kama walivyopita masheikh wengi wengine kabla yake.
Ndugu zanguni msimuone ndugu yenu kakataa kuitambua haki na akawa upande wa dhulma mkamkatia tamaa.
Muombeeni dua.
Kile kibri chake cha yeye kuwa upande wa wenye mamlaka na nguvu kisituvunje moyo.
Picha ambayo hainitoki kichwani mwangu ni picha ya Sheikh Kassim Juma mwaka wa 1979 anamkaribisha Nyerere ndani ya Msikiti wa Mtoro kwenye khitma ya aliyekuwa Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir.